What's this so-called "wrong parking" in the Dar es Salaam city?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wadau, miongoni mwa vitu vinavyonikera jijini Dar es Salaam ni kuona baadhi ya magari ya Watanzania wenzangu na hata ya wageni yakikokotwa na magari chakavu kwa kile kinachodiwa "wrong parking". Kwa uelewa wangu, kama kuna sehemu jijini inayokatazwa kupaki magari si wangeweka alama ili ionekane wazi au ndio wizi wenyewe wa kuwaibia wanye magari? Unakuta jamaa wanavuta gari lake zuri na wakati mwingine katika kulivuta wanaliharibu na kumwingizia hasara. Je, kuna sheria yoyote inayowalinda hawa wavuta magari au wanaweza kushtakiwa kama wezi wa magari maana wanavuta gari la mtu bila ruhsa yake? Naomba tujadili hii hoja maana ninakerwa sana na utaratibu huu wa kuharibu magari ya watu na kisha kuwalipisha faini. Je, wanaweza kufuangua kesi ya madai dhidi ya jiji? Asante!
 
Jana kweli nimesikia kwenye jahazi wahanga wa hili. magari yao yamevutwa walipofika kwenye hizo yard wakapata kichapo cha mbwa mwizi, mmoja alinyang'anywa kamera ambayo tayri aliitumia kupiga picha gari lake kabla halijakokotwa na lilivokuwa baada ya kuchakazwa na 'breakdown' na mwengine alikwapuliwa na dolari zake kadhaa...

Anyways ndo hasara ya kupeana tenda kimagumashi. Wanaoumia ndio hao wenye magari.

Sasa hata ukisema ukawashtaki wasiwasi wangu ni kuwa unapeleka kesi ya ngedere kwa nyani.
 
Lo! Then, tunaelekea jehanamu!
 
Back
Top Bottom