What's happening to SOPHIA SIMBA?

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Jamani hebu tuelezeni mbona hatujui kinachoendelea baada ya Sofia Simba kuzidiwa? NAni anaweza kuwasiliana na hospitali?
 
Jamani hebu tuelezeni mbona hatujui kinachoendelea baada ya Sofia Simba kuzidiwa? NAni anaweza kuwasiliana na hospitali?

Hope inafahamika kwamba Marehemu Salome alikuwa Naibu wake na Ugonjwa ulianza wakati mwenzake alivyopofariki ghafla,,, zaidi ya hapo tupatieni habari zaidi,,,

Wasiwasi wangu ni kwamba Ramli zitapigwa hapa za kutosha!!! haya twasubiri...
 
Naomba kujua huyu Waziri kapelekwa hospitali ipi maana mimi nilikuwa Buguruni ambako nimeshuhudia Polisi wanampiga mtuhumiwa hadharani tena kwa mashambulio kisa kakataa kutaja jina lake . Hii ndiyo Tanzania ya Kikwete .Pole Sofia Simba kwa kuumwa
 
bado hii habari haijatulia, wenye uwezo wa kuipepea tafadhalini jamani ili tuweze kujua nini ndani ya box
 
Halisi
JF Senior Expert Member

What happening to SOFIA SIMBA??????
-----------------------------------------------------------------
Jamani hebu tuelezeni mbona hatujui kinachoendelea baada ya Sofia Simba kuzidiwa? NAni anaweza kuwasiliana na hospitali?

Mkuu Halisi,

Heshima mbele mkuu, mbona hupokei simu yako mkuu....., okay the dataz.... nilizozipata karibuni, ni kwamba huyu mama ni msanii at best, alikuwa haelewani kabisa na marehemu, kwa hiyo kuhofia zile za Nchimbi, na ac alipoambiwa tu kuhusu ajali hii akajifanya kuzirai na kukosa fahamu, na kujichimbia ndani ili kukwepa zile za yeye kuwa na mkono kwenye ajali,

maana wanaowafahamu vizuri, hawaelewi kitu kabisa eti kuwa amezirai kutokana na kumpenda sana, Duh wakuu wanacheka sana kusikia huo usanii, mwambieni tu aamke aingie kwenye msiba hakuna noma!
 
Waziri Sophia Simba asema anaendelea vizuri
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ambaye amelazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal anaendelea vizuri.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili hospitalini hapo, Simba alisema kwa jana hali yake ilikuwa imeimarika kuliko ilivyokuwa juzi.

"Mimi ni mzima, afya yangu inaendelea vema," Waziri Simba aliwaambia waandishi wa gazeti hili mara tu walipoingia katika wodi alipolazwa.

Kauli ya Simba ilionyesha kutokana na kuwepo watu wengi waliofika kumjulia hali siku ya jana. Watu hao walifika ikiwa ni pamoja na taarifa za vyombo vya habari kuwa, hakuweza kuhudhuria mazishi ya Naibu Waziri wake Salome Mbatia kutokana na ugonjwa.

Baadhi ya Mawaziri waliofika hospitalini hapo kumjulia hali ni Zakia Meghji na Mary Nagu ambao walifika majira ya jioni.

Wengine waliokuwepo ni wanafamilia ambao pia walitakiwa kuondoka nje ya chumba alimolazwa kutokana na chumba hicho kuwa na wageni wengi hali iliyosababisha kukosa hewa kwa mgonjwa.
 
Halisi
JF Senior Expert Member

What happening to SOFIA SIMBA??????
-----------------------------------------------------------------
Jamani hebu tuelezeni mbona hatujui kinachoendelea baada ya Sofia Simba kuzidiwa? NAni anaweza kuwasiliana na hospitali?

Mkuu Halisi,

Heshima mbele mkuu, mbona hupokei simu yako mkuu....., okay the dataz.... nilizozipata karibuni, ni kwamba huyu mama ni msanii at best, alikuwa haelewani kabisa na marehemu, kwa hiyo kuhofia zile za Nchimbi, na ac alipoambiwa tu kuhusu ajali hii akajifanya kuzirai na kukosa fahamu, na kujichimbia ndani ili kukwepa zile za yeye kuwa na mkono kwenye ajali,

maana wanaowafahamu vizuri, hawaelewi kitu kabisa eti kuwa amezirai kutokana na kumpenda sana, Duh wakuu wanacheka sana kusikia huo usanii, mwambieni tu aamke aingie kwenye msiba hakuna noma!

Mkuu umenichekesha kweli unajua mambo yatasemwa mengi sana mimi mwenyewe binsfsi sijui ila nahisi yatasemwa mengi sana kuhusiana na hiki kifo cha huyu mama.
 
Yanayojili mwaka huu, sijui,mengi yatazungumzwa na ramli zitapigwa sana. Kulikoni huku ndani ya lichama la kijani
 
Mie nilipoona kwenye gazeti kwamba anasumbuliwa na kizunguzungu na kutapika nikajua labda mambo yamejibu kunako, tumwandalie mbeleko mwakani atakuwa ananyonyesha! Kumbe wengine mnasema......!
 
"kitime" Huyu Mama Emlazwa Kabla Hata Mzazi Ajapata Ajali,,tusimsemee Moyo Jamani,,lingine Tumpe Nfasi Apumzike,,alianza Kuumwa Alivyotoka South,labda Twaweza Sema Izi Ni Bakora Tu Za Mwneyezi Mungu Kuonyesha Jamii,
Namtakia Salamu Njema Uko Alipo Mama
 
Nakumbuka siku Zitto aliposimamishwa Bungeni kabla Mzee victim Mudhihir Zitto alipewa nafasi ya aidha kufuta hoja au kuiacha kama ilivyo naye alisema hivi namnukuu "...sisi ni wabunge tuliochaguliwa na Mungu kwa ajili ya kuwatumikia wananchi sitafuta kauli yangu kwa maslahi ya wananchi....." Hayo aliyoyasema ni mazito Mungu anayafanyia kazi.
 
Naomba kujua huyu Waziri kapelekwa hospitali ipi maana mimi nilikuwa Buguruni ambako nimeshuhudia Polisi wanampiga mtuhumiwa hadharani tena kwa mashambulio kisa kakataa kutaja jina lake . Hii ndiyo Tanzania ya Kikwete .Pole Sofia Simba kwa kuumwa
Anaumwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom