What? Take it as the act of GOD! Really?

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Where the hell do these leaders leading our country come from???????????? Naangalia hapa mheshimiwa Seif Idd anahojiwa na Aljazeera kuhusu ajali ya meli kuzama. Nini kifanyike kuhakikisha ajali kma hizi hazitokei tena?????

" People should learn to persevere and take it as the act of God" Really??? How many stuff then we can say are the act of God?

1. Umasikini of course.......
2. Ufisadi hakika
3. Maradhi na ujingaaaa naaaaaaam yote haya ni act of God. and the list goes on and on!

Just sick and tired!!!!
 
Kinachoishangaza ni kwamba nilidhani mtu huyu angalau angekuwa na brains kidogo katika upstairs yake! Kumbe Duh!!
 
It has been written. Where? i dunno. How will i know whatever is happening to me is written? You will when you git there my son!
 
Nyambala

Huko Duniani watu wanatucheka mpaka basi!! Amejibu kama ndio ameingia serikalini leo. Kiukweli ajali hizi nyingi ni za kujitakia, hakuna usimamizi wala hawataki kujifunza kwingineko wanafanya nini kuzuia au kupunguza ajali.

Mathalani WAMAREKANI wanasema hiyo boat ilitakiwa kupakia abiria si zaidi ya 148 na isipakie mizigo,wao walieuhusu abiria karibu 300 na mizigo tani 26!!! HAPO UTASEMA NI MJPANGO YA MUNGU KWELI au ndio kukwepa lawama???
 
Last edited by a moderator:
hizo ni meli za viongozi au vivuli vyao lazima watoe kauli za kusitisha udadisi. shame!!!!!!!!!!!!!!!!
 
huko Duniani watu wanatucheka mpaka basi!! amejibu kama ndio ameingia serikalini leo. kiukweli ajali hizi nyingi ni za kujitakia.hakuna usimamizi wala hawataki kujifunza kwingineko wanafanya nini kuzuia au kupunguza ajali.mathalani WAMAREKANI wanasema hiyo boat ilitakiwa kupakia abiria si zaidi ya 148 na isipakie mizigo,wao walieuhusu abiria karibu 300 na mizigo tani 26!!! HAPO UTASEMA NI MJPANGO YA MUNGU KWELI au ndio kukwepa lawama???

Mkuu unajua nijikuta nashtuka na kushindwa kushangaa, Yaani na journo aliyekuwa anamuhoji nadhani hakuamini macho na masikio yake!!!!!!
 
Mkuu unajua nijikuta nashtuka na kushindwa kushangaa, Yaani na journo aliyekuwa anamuhoji nadhani hakuamini macho na masikio yake!!!!!!
jibu alilotarajia kutoka kwa mtu kama yeye ni mikakati ya kisayansi na inayo lenga kutuondoa kwenye ajali zisizo za lazima na zinazo weza kuzuilika yeye anasema wananchi wavumilie na wakubali kwani ni mpango wa MUNGU, KWELI?
 
wananchi wenzangu tusikubali kufanywa wajinga na hawa wanasiasa njaa. kuna maswali mengi ya kujiuliza

1. kama suala ni upepo na hali ya bahari kuwa mbaya, kwa nini iathirike meli ya skagit peke yake? ikumbukwe kua wakati ajali inatokezea, kulikua na meli nyingi katika bahari kama flying horse, kilimanjaro 3, majahazi ya tanga achilia mbali vidau vya uvuvi. sasa hivi vyote kwa nini havikuathirika

2.Pili jee mamlaka za hali ya hewa na bandari zilikua wapi hazikuona dalili ya upepo. Mbona watu wa hali ya hewa wanasema walishatoa taarifa ya upepo lakini ikawa delayed kupokewa na watu wengine?

3.Hizi meli tokea ziko marekani zilikua zinalalamikiwa kutokana na kutokuwa salama hususan umbo lake ambalo liliongezwa. pia wananchi wa huko walilalamika kuwa hizi meli (skagit na dada yake Kalama) zinayumba mno baharini, (angalia mtandao), hata hapa JF zilishajidiliwa. Jee wataaalamu wetu hawakulijua hilo?

4.Meli inasemekana ilizama saa saba na nusu, lakini chombo cha mwanzo kufika kilikua ni kilimanjaro nacho kiliwasili saa tisa na nusu, jee muda wote huu maofisa wa serikali walikuwa wapi?

5.Kwa nini nahodha na baharia wake walishindwa kuact accordingly? inasemekana boti ilikuwa katika mwendo wa kasi mno, huku inayumba na huku hali ya bahari ikiwa chafu. Lakini nahodha akatoa tangazo kwamba abiria wasiwe na wasiwasi. Ghafla meli ikazama. Jee huyu nahodha na hawa mabaharia walikua na sifa? na jee nani aliwaruhusu kuwa katika chombo hicho.
 
Hakuna mungu anayeruhusu ajali zitokee. Kwanza haya majahazi, meri, ndege, magari, n.k. si kazi ya mungu. Ni kazi yetu sisi wanadamu. Mungu alitupa miguu kutembelea, lakini akatupa na vichwa vya kufikiri na kufanya mambo ya kuiongezea miguu uwezo pale isipoweza. Kwa hiyo ajali kama hizi haziwezi kuwa mapenzi ya mungu hata kidogo. Hivi vitu tumeviumba sisi, wajibu wa kuvidhibiti na kuvitumia kwa usalama ni wa kwetu si wa mungu.

Mungu ameweka kanuni za mazingira ambazo hatuwezi kuziamua sisi. Mfano hatuwezi kusema tutazuia upepo au tufani za baharini. Hizo hutukea kwa wakati wake. Tukiingia wenyewe kwenye tufani na upepo wa bahari halafu tukazama, hapo lawama kwa mungu za nini? Tumefanya uzembe mara nyingi kwa kutojali, tukaokoka kwa kudra tu za mwenyezi mungu; sasa hiyo kudra tumeshaichukulia kuwa ndo kisingizio cha udhaifu wetu.

Kuna bahari ziko busy sana kuliko hii ya kwetu (DSM-Unguja), na kuna vyombo vingi vinapita salama; wakati hizi pepo na tufani zikiwepo vile vile. Kwa nini hapa kwetu ajali ziwe nyingi vile? ... Tukubali uzembe wetu ndo sababu namba moja!

Kwanza usalama wa vyombo vyenyewe vinavyotumika - Hii meli ilikuwa ikitumika kama kivuko tu huko ilikotoka, na ilishaacha kutumika kitambo. Tathmini ya usalama wake katika mahali ilipokuwa inatumika hadi inapata ajali haikufanyika; wenye mamlaka wakubali tu kuwa ilisajiliwa tu.

Pili, pamoja na usalama wa kutia mashaka bado uendeshaji unaotegemea zaidi kudra za mwenyezi mungu ni tatizo vile vile. Hakuna anayesema kwa uhakika wasafiri waliokuwemo ni wangapi. Uwezo wa meli hiyo tunaambiwa ilikuwa watu 250; tunaambiwa walikuwemo 290; hapo tayari tuna tatizo la kuzidisha mzigo na kutegemea kudra ya mungu.

Tatu, uwezo na utaalam wa waliokuwa wakiendesha meli hiyo nao unaingia kwenye mizania ya mashaka kwani wakati hali ya hewa ikiwa mbaya badala ya kuwaambia watu wachukue tahadhari (kwenye ndege ikitokea dharura kidogo mnaambiwa fungeni mikanda) hapa watu wanaambiwa wasiwe na wasi wasi. Hii nayo inaonesha uzoefu wa kudra za mwenyezi mungu unaotufanya tuzoeee na kuona kuwa hakuna tatizo.

Sasa ukijumlisha mtiririko wa makosa tokea kwa matumizi yasiyokuwa sahihi (kivuko kuwa meli ya maji marefu), Uchovu wa chombo chenyewe, kutojali wa wanaosajiri meli, ujinga wa wanaoendesha meli yenyewe (pengine kutokana na hali yake meli hii haikutakiwa iendeshwe kasi ile), kutotilia maanani maonyo ya hali ya hewa, n.k. bado tu tunapata ujasiri wa kumsukumia Mungu zigo hilo??? ama kweli hatujui mungu ni nani! Na kwa ujinga huu kamwe hatuwezi kufika kwake!!
 
Back
Top Bottom