What lovers should do

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,756
Lovers should quit when their passion is at its peak, not wait until its inevitable decline. Haya maneno si mepesi. Kuna raha na ushujaa ndani yake. Si ktk mapenzi tu. Bob alikufa na umaarufu wake. Bonnie M walivunja kundi wakiwa ktk kilele cha umaarufu. Swali ni je, wenza wafanye lipi ili mapenzi yao yaliyo kileleni yasikumbane na anguko lisiloepukika? Binafsi nimekuwa mapenzini yaliyofika kileleni kisha yakaanza kuporomoka. Hata wewe! Ni sahihi kufikia muafaka ili kuuvunja?
 
Kama kweli mnapendana kiasi hicho na hadi kufikia kilele cha mapenzi na mnajua fika ni mambo gani mliyoyafanya katika mapenzi yenu hadi kufikia "the pinnacle of love" kwanini msijitahhidi na kukumbushana kila mara ili mbaki kileleni katika mapenzi yenu!? Si rahisi lakini inawezekana kama wote mkiweka juhudi kubwa katika mapenzi yenu.
 
Ni busara sana kuachia ngazi ukiwa katika peak ya heshima au maelewano, maana heshima itaendelea...Nimeshuhudia wapenzi wengi wakiachana kwa maneno makali sana kama..."Unikome kama ulivyokoma kunanihii nanihii ya nanihii..."
 
Paka Jimmy umenichekesha eti 'unikome kama ulivyokoma kunanihii nanihii ya nanihii...' wat is that nanihii if i may ask hahahahha?
 
Uachie ngazi ukiwa kileleni; anguko lake si mchezo. Sijui, lakini utajuaje kuwa sasa nipo kileleni na hivyo niachie ngazi na ni kweli kuwa nitashuka kiasi cha kuachana kwa ugomvi. Ni suala ngumu kuliko ugumu wenyewe kulitolea uamuzi. SIJUI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Paka Jimmy umenichekesha eti 'unikome kama ulivyokoma kunanihii nanihii ya nanihii...' wat is that nanihii if i may ask hahahahha?

Ha ha ha ha ha ha ha ha ukienda kwenye dictionary ya maneno ya nanihii utaona tafsiri ya kunanihii nanihii ya nanihii:rofl:
 
kwa m2 mstaarabu na msomi sioni sababu ya kuachana kwa maneno makali, kweli mkiachana kwa amani kuna shida?
Tena mnafanya na sala fupi then mnaachana, na kutakiana maisha mema...
 
mapenzi mengi yanaanguka kwa watu kuchukuliana for granted nadhani. pia kwa ile monotonous routine........wiki nzima mtu umeshajua itakuwaje hata kabla wiki haijaanza!

tunatakiwa kidogo tupeane suprises katika vitu mbali mbali ...............kwenda vacation pamoja, zawadi ndogo ndogo, hata mfumo mzima wa kufanya mapenzi unatakiwa uwe wenye kbadilika badilika ili penzi liwe jipya kila leo.
 
Back
Top Bottom