What is your "Sweetest" Childhood Memory?? THAT It made you feel So Good and Speacial!

mama used to take me to the movies....dah sitasahau,miaka ya katikati na mwisho ya 80's,..cameo,avalon,empire,empress yalikuwa yananijua kwa jina,..ukirudi kitaa watoto wenzangu walikuwa wanakoma,nitahadithia movie nzima ya kihindi hadi maneno yake...disco dancer nimeicheki kwa mara ya kwanza cinema(empire)87 au 88,..i will pass that hobby(cinema going)to my unborn child...good ol days...childhood days will always stay on my mind...thank you mama!!......
 
Scofield umenichekeshaje? yaan wewe stick za mdingi ndio "sweet" child hood memory? lol.... Dah! Nashindwa kupimia.... Napenda the fact kua umeona kua stick zilikua kwa malengo mazuri na for your own benefit.

Mi nimelelewa na mama...

I loved my mom...

J'mosi ya kila wiki asubuhi ananipeleka shopping... Not necessarily kuninunulia vitu,but hata vitu vyake mwenyewe...ila mimi companion wake... Sijui ndiyo maana nami nimedevelop hobby ya shopping?!

I wish it could come back again... Na nilikuwa mwoga wa sindano..na njia ya kwenda Mnazi Mmoja health center kutokea nyumbani,ilikuwa lazima upite "Bakhressa" pale Livingstone...kwa hiyo nikiwa na sindano za masaa tu namlazimisha kuwa anipromise tukishachoma aninunulie "ice cream",au baadaye kukaja "milk shake"...

Can't forget those moments..
 
Kitu ingine ya ODM....

Nlikuwa mtaalam wa kuweka kioo chini ya miguu ya mabinti tukijipanga mstari shuleni. Basi nikifanikiwa kujua rangi ya andawea ya binti, asiponinunulia ubuyu darasa zima watajua! Blackmail ya kitoto ilikuwa.

ODM bana.....

Wakati nikiwa timekeeper nlikuwa nafanya manjonjo mpaka naingia ofisini kwa mwalimu mkuu kusogeza saa mbele.... Kisa? Muda wa mapumziko uwahi kufika tukacheze chandimu. Walimu walikuwa wanashangaa kwanini kila siku saa ya ukutani kwa mwalimu mkuu ilikuwa inatangulia kulinganisha na saa zao...... wakaweka mtego siku ya siku nikanaswa......

Kengele ikagongwa wanafunzi wakakusanyika tayari kushuhudia ODM akitandikwa bakora kwa utovu wa nidhamu.... tena kwa walimu kupokezana.... Hawakumjua ODM vizuri masikini. Enzi hizo nasumbuliwa na ugonjwa wa kutoka damu puani..... bakora ya kwanza mzee mzima nikajiangusha chini pwaa.... damu ikatoka puani kama maji! Adhabu ikaishia hapo na kuzawadiwa kupumzishwa chini ya kimvuli....(ofkozi nikibembelezwa).

Chezeya ODM wa enzi hizo weye!

ODM una mpango gani na Ribs zangu? lol.... Umenichekesha mpaka baaas! Eheee umeacha black mailing? (naanza kuogopa kua nikitereza imekula kwangu!):hatari:

The other part ya adhab si imagine the agony the teachers felt walipoona damu!
out of curiousity nani alikua anakubembeleza pale chini ya mti? :eyebrows:
 
Kumbe wewe shida ilikua inakuja kwenye kumuongesha? lol.... Inaelekea ulikua hufai wewe! Personally utoto sijachezea sana midoli, ila nimefinyanga kweli... in fact ngoja Vaadae nitajaribu nione kama bado ujuzi upu au umehama. lol

Mdogo wangu kumbe nawe wapenda mto kama mimi? lol.... Tena mimi napenda miwili, usitake tu kujua naipanga vipi? Ila ipo so effective! lol
Hahhaahha hahahaha,nitakupm unambie style ya kupanga mito unapolala na uwepo wa big shem lol!

Asa kuna kituko kingine bana hiki mpaka kesho huwa nikikumbuka nacheka sana,
Kwanza nilikuwa napenda sana kuvaa vitu vya mama,km viatu na nguo,
Siku ya siku nakumbuka padri wetu alikuja hm,
Mie nikuwa nimelala na baba chumban asa mama akaja kumwamsha baba padri kaja baba alipotoka tu na mie nikashuka kitandan kulikuwa na tenga flan la kuwekea ngu chafu nikazana na kuibuka na brazia ya mama nikajitupia na kutoka seblen nikaenda kusimama katikati ya sebule watu walichanganyikiwa nakumbuka mama alikurupuka na kuja kuninyakua km mwewe anavonyakuwa kifaranga yani nilisabababisha bonge la aibu aisee!!!
 
ADI, afu nilipokua kua ka teen, ndo enzi hizo mabreka(break dance) yamapamba moto.
Usipoalikwa kwenye sherehe kuwa stage show unaenda kunywa sumu hapo late 80's.
 
Pamoja AD.
Kuna siku dingi aliibuka shule ghafla akanikuta juu ya mzambarau, wenzangu wako class, du kipondo chake noma mpaka nikapelekwa magomeni hospitali, nilivyopona tu nikapata tena kesi ya kumchungulia mama mwenye nyumba alikuwa anaoga, du napo nilikula kipondo mpaka mkono ukateguka.
Nilikuwa mtundu kama Mtambuzi.


Duh! Scofield wewe ndio wale watoto kwa wazazi kwa kweli ni KERO! lol....
Huyo mama ulikua unamchungulia nini ulikua wataka hapo? Mtoto ulikua na vituko wewe! hahahaha.... Eti kama Mtambuzi! ngoja nimuite akusome hapa.....

Na amini usiamini babako asingekua strong katika kukuweka sawa, ungepoteza mwelekeo wa maisha nahisi!
 


Habari wana JF…..
:poa


Ukiwa kama mtoto haijalishi uko katika hali gani, waishi mahala gani ama jamii gani... Tunakua kama malaika na the world is so wonderful in our eyes... kila kitu almost Perfect!Our elders/guardians na parents hua as if wao ndio kila kitu na what they know is absolute and perfect! Sio woote tumejaliwa kulelewa katika mazingira mazuri na conducive for a kid... wengine wamelelewa kwa mateso na manyanyaso.... Lakini regardless ya yoote hayo... Kuna kitu/vitu vile hukufurahisha as a kid and a person which sticks in your mind FOREVER... Tokana na jinsi kilivo kugusa kwa Furaha... ndani ya roho na Mwili mzima! Yaani inakufanya pamoja na kua na utu uzima huu.... you still remember once in a while....



Now ADI is interested in that "Sweet" Childhood Memory of yours.... Care to share?
Please tuendeni on Child hood Sweet Memory Lane.... And lets Enjoy the ride.



Pamoja Saana
ADI.

I do remember the times I had my report form at hand (mind you I was a bright kid) the feeling that came in my mums eyes when she opened it and later the whole house went happy because of me, tunapikiwa chips and promises of going out. I think those are the very best moments when I think of my childhood.
 
I will never forget mchezo wa baba na mama, mi nlikua baba wakat mwingine mtoto yaani nikikumbuka nataman kurudi utoton ila basi umri umekwenda.
 
aah best tym ever ya utotoni ilikua mwanzoni mwa miaka ya 90.
1.Siku tunacheza mpira wa miguu kama Yanga na Simba...wachezaji wote wanakua na a.k.a kama yalivyokua majina ya wachezaji wa Simba au Yanga...siku hizo mtaa mzima hadi wazazi wanakuja kucheck game jinsi madogo tulivyokua tunapiga mpira...

2.Siku ya kuangalia sinema ya Yesu either church au kwenye viwanja vya CCM...kipindi hicho teknolojia ya video na television ilikua nyuma sana basi siku hizo full kutoa ushamba...
3.Siku za sikukuu,suruali mchele mchele au mawingu(imekaa ka jeansa hv) halafu shati la minazi minazi hivi n chini raba mtoni au DH(dingi hana uwezo) au mokasini(kwenye ulimi zinakua zina kibrush hivi).
 
Duh! Scofield wewe ndio wale watoto kwa wazazi kwa kweli ni KERO! lol....
Huyo mama ulikua unamchungulia nini ulikua wataka hapo? Mtoto ulikua na vituko wewe! hahahaha.... Eti kama Mtambuzi! ngoja nimuite akusome hapa.....
Na amini usiamini babako asingekua strong katika kukuweka sawa, ungepoteza mwelekeo wa maisha nahisi!
Yaani AD we acha tu! nikikumbuka utoto najidharau kwa kweli namshangaa huyu hapa chini anautaka ubaba wa utotoni, naona huu ubaba wa ukubwani mgumu!

I will never forget mchezo wa baba na mama, mi nlikua baba wakat mwingine mtoto yaani nikikumbuka nataman kurudi utoton ila basi umri umekwenda.
 
acha hiyo mambo kuna mzee mmoja shamba lake lilikuwa lina maembe eh bwana tulikuwa tunajikusanya kikundi kama mtu sita hivi tukiwa na mawe yetu kabisa, halafu tuingia mzigoni, usipime yan mpaka malboro ijae. baada ya shughuli kuisha tunatafuta sehemu yenye kimvuli chini ya migomba au kahawa hakafu kazi inaanza embe moja mpaka lingine.

tikishatoka hapo basi tunaenda kuoga mtoni acha hiyo mambo ilikuwa ni balaa.


Wewe Tedo hayo matumbo yalikua yanapona? lol.... Sijui whats it with kids na kula matunda kupita kipimo! hasa ya kuiba ndio rekodi inaonesha ni matamu kweli.... Umewahi kamatwa ukala kichapo?
 
Dah kwanza kombolera it was fun...ongezea na mchezo wa kujificha ambao actually ulinifanya nifunguke kwenye mambo ya kikubwa.

Michezo ya kupigana kwa matunda pori au hata mawe (mkoa wa Mara huo)!! Kuchuma matunda kwenye mashamba ya watu ilitutokea puani..siku moja tulikimbizwa na wenyewe wakiwa mtu 5 sisi wadogo tuko kama 4 walikuwa na mbwa na panga mkononi..acha tu it was terible..lakini mwisho wa siku hawakutukamata...tulikula mbio Juma ikangaa cha mtoto.

Habari ya fimbo: za mama (R.I.P) nimekula sana ila baba (RIP) alinichapa mara moja tu nilipogoma kunyoa nywele..by the way alikuwa mpole kama mimi!!

Naomba kwanza nitoe pole za kupoteza wazazi woote wawili.... May they Rest in Peace.

Michezo mingine watoto hucheza ni ya HATARI.... Alafu na wao walizidi... Panga na mbwa? mtakua mliwaboa sana....lol.

The thing with Mchezo wa Komborela ni kua haubagui mtu, huu mchezo watoto wote waliweza cheza, it does not matter haupo athletic.
 
Umenikumbusha mbali AD nilikuwa mtoto wa getini yani shule home bac sasa ikatokea nikaenda kijijini likizo kwa mara ya kwanza bana nikakuta watoto wa kule wanakamata kobe then wanawapandia juu kama ndo vigari wee wacha kila holiday mm kijijini


Angel Karibu sana jamvini... I am humbled kua your first post umeifanya katika this tread of mine... b2t

Ni wapi huko ambako tortoises wakubwa mpaka watoto waweza kwea?
 
Naomba kwanza nitoe pole za kupoteza wazazi woote wawili.... May they Rest in Peace.

Michezo mingine watoto hucheza ni ya HATARI.... Alafu na wao walizidi... Panga na mbwa? mtakua mliwaboa sana....lol.

The thing with Mchezo wa Komborela ni kua haubagui mtu, huu mchezo watoto wote waliweza cheza, it does not matter haupo athletic.

Asante kwa pole.nafikiri walichoshwa.. na kwa kule mtu kuwa na panga ni jambo la kawaida sana.Nimekumbuka na kuogelea mtoni pia huku tukionyeshana vinyweleo vyetu kwenye nanihiii..eti tunaita m.....i. Weye mbona hujasema ulicheza ule mchezo wa kibaba na kimama,halafu mnajificha mnawaambia watoto wakalale
 
Zangu mimi zilikuwa za utundu. Nilijaliwa kujua mengi ya shule (kusoma, kuandika na kuhesabu) hata kabla ya kuanza shule, kwa hivyo nilipoanza kwenda shule walikuwa wananiboa sana, hakukuwa na kipya nilichojifunza kwa hivyo nilikuwa naona bora mchezo kuliko shule. Kwa sababu hiyo, nilikuwa siishi kutoroka na kutafuta kila kisingizio cha kutokuwepo darasani (what for, nilikuwa ninajiuliza na hakuna mtihani wowote nisiotokea wa kwanza). Baadhi ya "unforgetful advantures zangu ni:

- Siku niliyokula pilipili kwa makusudi na kuenda kliniki nikidai nina homa. Dokta kunipima, nilikuwa na sijui madigrii mangapi. Hadithi ndefu lakini uongo ule ulinilazimu kulazwa hospitali wiki moja.

- Siku niliyoaga shule kuenda hospitali, baada ya kupata dawa nikaenda na wenzangu kuangua madafu ktk minazi ya babu. Ilikuwa siku ya mwanzo kukwea mnazi...kushuka ndio ilikuwa ngoma. Nilipururuka mpaka chini nikiwa nimechunika mapaja na kifua chote. Mara hii nilirudi tena hospitali kwa sababu ya kweli kweli. Wiki mbili mahututi.

- Siku nilienda kuiba machungwa ya babu jirani. Baada ya kujaza machungwa mifukoni, ninataka kuteremka nilikwama juu ya mchungwa. Nilianza kulia mpka ikabidi mzee mwenye mali aje kuniteremsha. Nikiwa ninaendelea kulia, nilimwomba anipige yeye lakini siri ile isifike kwa baba, kwani viboko vyake...kuliko vya Mjerumani.

- Siku hizo vitabu na vifaa vyote tulipewa bure, tukimaliza mwaka tunarejesha na kupewa vyengine. Kumbe katika kitabu kimoja kulikuwa na barua aliyonijibu "mchumba wangu". Mwalimu aloikamata akatishia kumwambia baba yake ambaye alikuwa daktari wa meno. Siku ya pili daktari alikuja shule (kumbe kwa ukaguzi wa kawaida wa afya zetu) lakini mimi nilidhani ndio amekuja kunishikisha adabu. Sikuwa na raha muda wote mpaka alipoondoka. Badae mwalimu aliniita na kunionya nisizowee, kusoma kwanza mademu baadae.

- Pamoja na yote hayo walimu waikuwa wananipenda kwani nilikuwa hodari. Sikusoma darasa la 2 nikapelekwa la 3, sikusoma la 4 nikapelekwa la 5 na sikusoma la 6 nikapelekwa la
saba. Nilikuwa ninafurahia zawadi za mwanafunzi bora.
 
ODM una mpango gani na Ribs zangu? lol.... Umenichekesha mpaka baaas! Eheee umeacha black mailing? (naanza kuogopa kua nikitereza imekula kwangu!):hatari:

The other part ya adhab si imagine the agony the teachers felt walipoona damu!
out of curiousity nani alikua anakubembeleza pale chini ya mti? :eyebrows:
Hehehehe.......... Mwalimu mkuu, usiniulize jinsia yake tafazali.....
 
Hahahahah hahahah hahahahha!
ODM umeniuwa kwa kicheko,imebidi nikachekee nje lol!

Nakumbuka kuna mahali tulienda tukaletewa soda asa kikatokea kimjamaa na kikombe chake cha plastic kikawaweka juu ya meza na kuanza kutuangalia ilibidi nimmiminie mama yake alipotokea akataka kumfukuza dogo akasema mbona soda wanakunywaga wageni tu sie hatujawahi kunywa mpaka ifike iddi!!!
Ila hii yako noma babu lol!!!
Hihihihih..........usicheke sana bana, usijeachia kaushuzi mbele ya mkoloni...:photo:
 
Hihihihih..........usicheke sana bana, usijeachia kaushuzi mbele ya mkoloni...:photo:
Hahahahaha hahahahha hahahah uwiiiiiiiiiiiii mie mbavu zangu lol!
kwa hili ndio nimecheka mpaka basi ushuzi tena,
Hki ya nanni babu hujabadilika kbs,vituko vyako vya udogon nahisi vimekuwa advanced ukubwan lol!
 
Back
Top Bottom