What is wrong with this picture?

Mie interest yangu ni hiyo picha ya kulia ya shule. Siku zote uwa najiuliza swali hili:

"Ni kwanini viongozi wanaweza kuishi maisha ya kifahari wakati tunatoa huduma mbovu za jamii kama hiyo shule inavyoonyesha"

Hela za V8 zipo na bado tunajenga nyumba ya 1.5bilion kwa ajili ya Gavana na wasaidizi wake lakini kujenga shule hatuna hela?????? Shame on you!

Wajibu wa wawakilishi wetu ni nini? TAFAKARI

Kile kudude cha like hakipo mkuu, ila pokea like yangu,

hapo ndipo wengi huwa tunashangaa, yani bei ya V8 moja wanajenga shule na nyumba za walimu lakini wapi na bado watz tumelala tu!? sijui ni ujinga?, sijui ni ujuha? sijui tumelogwa?, yaani sielewi kabisaaaaa!
 
Picha ya kushoto,ni aiport, JK anapokelewa na VP,PM,RC DAR. Sio vibaya sasa kujadili ya kulia.. Kifupi tuna shida ya vipaumbele. Tunataka yote kwa pupa! Hivyo hatukawii kukosa yote!
 
Mbona maandiko yanaonyesha kuwa wako Perth. Huu ni uongo wa mchana kweupe. Humu ndani ni vyema mkaleta habari za ikweli kiliko kujitungia mipicha kama magazeti ya udaku! Mwishowe JF itaonekana kama kijiwe samli kijiwe vha majungu, tetesi na uongo. si vyema kuipeleka JF huko.

Acha uzembe wa kutumia akili yako, hapa issue ni tofauti ya maisha wanayoishi hawa jamaa na maisha halisi ya MTZ. Haijalishi picha imetoka PERTH ama MAGOGONI lakini ukweli ni kuwa JE TAREHE 30/10/2011 TUNAENDELEA KUWA NA WANAFUNZI KWENYE MAKUTI KAMA NGOMBE?

Miaka 50 ya Uhuru ZiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
Ukweli ni kwamba yanayotoka mdomoni mwa viongozi wetu hayafanani na matendo yao: i.e. They don't walk their talks:
 
mambo mawili amabayo mimi nayaona kwenye picha hizi
1. Uongo, kwani haiwezekani Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya nje wawe nje ya nchi moja wote wanne kwa wakati mmoja, kwa hiyo hapa sio australia bali ni bongo, ushahidi ni pamoja na kuwepo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam, pamoja na polisi wa kibongo pia wanaonekana kwenye hiyo picha ya kushoto. Uongo mwingine upo kwenye hiyo picha ya kulia, mimi ni mkazi wa Jimbo la Chalinze ambalo lipo katika Wilaya ya Bagamoyo nalijua vizuri na hakuna hata shule moja yenye hadhi kama hiyo

2. Uchochezi; ambapo mtoa mada anajaribu kugombanisha kati ya wananchi na viongozi wa serikali.
 
Hata mie nimeshtushwa na uwepo wa makamu wa rais, waziri mkuu, waziri wa mambe nchi za nje na mkuu wa mkoa wa Dar. Jambo lisiloingia akilini Rais, makamu wake, waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje kufanya safari ya pamoja nje ya nchi!! sijawahi kuiona wala kuisikia tangu Dunia hii iwepo!!
Picha ya kushoto ni ya UONGO sio PETH, AUSTRALIA ni DAR-ES-SALAAM AIRPORT

DAMN PICTURES DOES NOT HOLD WATER...

Bring us human structure on issues, not gossip...
 
Kha kumbe ni darasa nilifikiri ni banda la kuku, amaa kweli wanachadema kukesha NMC wana sababu zoooote
 
Kama mleta uzi anatudanganya picha ya Dar anatuambia ni Perth. Vipi na hiyo shule je sio ya enzi zileee za kila kitu 'adimu'?

Ni makosa kidogo ya uandishi ingawa ni picha ya rais akiwa JNIA akitoka Perth na wala haijachakachuliwa.
Inasikitisha kuona watu wanatanguliza mbele ushabiki kuliko kuangalia hali halisi ya nchi hii inakoelekea.
Nchi sasa hivi ina madeni kwa sababu mheshimiwa ameamua kufanya safari za nje kuwa kipaumbele chake
na wala hatuoni manufaa yanayotokana na safari hizo zaidi ya kutudhalilisha kwa kuwa sasa tunaowaomba
misaada wanatuwekea masharti ya kutaka kutu****ti kwa kutaka tuukubali ushoga. Hii ni aibu ya mwaka!
 
Tatizo la serikali ya CCM ni VIPAUMBELE vya msingi wamepuuza,
Badala yake ni masafari, maonesho na masherehe, kila kukicha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom