What is wrong with African football?

Sioni sababu za msingi za kupokonywa.

Timu 31 zinazoenda WC ni timu bora zaidi duniani ktk kanda wanazotoka...hivo kule hakuna vibonde, ndio maana timu za Afrika zilishawahi kugawa maumivu kwa mabingwa watetezi (ref. Cameroon vs Argentina, Senegal vs France). Hivo kigezo cha ukibonde hakipo applicable..


Thank you Mkuu!
 
Timu 32 za WC zigawanywe kiusawa katika bara zote kutokana na idadi za nchi. Vipi ulaya wapewe idadi kubwa, wakati timu "kabambe" France na Italia zimetolewa round ya kwanza? Kwa Africa ilitakiwa ziwe nchi 8. Usihisabie WC hii tuu, angalia pia na za kabla wakati Cameroun ilitinga Quarter Final.
 
timu za afrika zinatia hasira ...............timu 6 inaingia moja! Agggggrrrr wachezaji wa afrika wavivu bwana......wawaangalie wenzao wa asia, wafupi lakini stamina ya uhakika na wana moyo hasa wa kuhangaikia goli.


World cup ijayo zitakuwa tano tu kwa hiyo itakuwa tayari zishapunguzwa.........

sijajua tatizo letu ni nini bado
 
Hakuna haja ya kupunguza Africa mbona hata Europe wamechemsha,ila kuna umuhimu wa kuongeza timu kutoka South America
 
kaka ingebidi ungesubiri kwanza kabla kutoa maoni haya,si unaona kwanza hakuna timu hata 1 ya amerika kaskazini wala asia,ila afrika ipo 1,amerika kusini 4,ulaya 3,hata mimi nilikata tamaa na timu za afrika,ila sasa angalau kwa ghana i trust.
 
makocha wazuri wanatoka nchi zenye asili ya yugoslavia zamani,eg croatia,serbia,bosnia,sarajevo,herzegovina,makocha wazalendo mhhh mbado sidhanii kwa sana,kazi ya ukocha inabidi usomee sio eti kisa umecheza mpira tu u unajua kuchambua soka la! kina wenger,mourinho,ferguson wana digrii zao za ukocha wale sio longolongo.
 
Inasikitisha kuona Ghana ikiondolewa ktk dakika za mwisho. Hii si mara ya kwanza kwa timu za Africa kutolewa ktk robo fanali kombe la dunia. Ghana ndiyo time pekee ya Africa iliyoweza kubakia kabla ya kunyimwa goli na "FIFA" referee.
Swali la kujiuliza, kwanini timu za Africa hazifiki mbali ktk WC zaidi ya robo fainali? jibu, ligi zetu hazina mikiki ya nguvu kama ligi za wenzetu Ulaya, na South America. Kila mwaka tunaona timu zilezile zinawakilisha Africa. Soka ya Africa haichezwi kihalali kama za wenzetu Ulaya. Rushwa imezidi kwa mareferee, viongozi wa vilabu, National level, na viongozi wa CAF. Kila mwaka tunaona timu kubwa ndizo zinazochukuwa ubingwa. Kiukweli kabisa, Africa Chapions League inabenefit zaidi timu za West Africa na North Africa. Kila mwaka tunaona kabisa vilabu vikubwa vinapangiwa vilabu "vidogo" ktk mechi za ufunguzi ktk mechi za CAF, na Chapions League. Soka ni progress, ukicheza mechi ya kwanza, basi kuna uwezakano mzuri zaidi ktk mechi ya pili utacheza kwa uzoefu zaidi kuliko ile ya mwanzo.
CAF haina mikakati ya kuisadia Africia ktk mechi za kimataifa. Tutafute mbinu zingine zaidi za kuisadia timu za Africa, tuimarishe upinzani ktk ligi zetu za nyumbani ili tuweze kujenga wachezaji bora kama wenzetu South America na Ulaya. Is time for Africa to wake up, stop corruption in sports, and let's play fair game.
 
ukiwa shabiki wa timu za Africa unaweza kupata uchizi...........kosa alilofanya A.Gyan hadi huruma ila vijana walijitahidi hadi kufikia hapo!!!!!!mbona brazil walitolewa kwenye hatua hiyo hiyo!!!!!!
 
Yah, ukiwa na roho ndogo unaweza kukomit suisaidi. Inauma kupita maelezo. Hii inaonyesha umakini usiopangiliwa wa wachezaji wetu. Pia udhaifu wa hawa weupe kucheza netball uwanjani. Bora kujifariji kwa kusema kuwa ni wadhaifu tu na wanatumia hata mbinu chafu kujifanikisha. Pale nimewaondoa thamani uruguay
 
jana nilishangilia ghana ugonjwa wa moyo ukanirudia tena,nilishaacha kushangilia timu za afrika mimi,hadi mtaani kwangu wananiita eti mimi mzungu mweusi!,ila hata amerika kusini nao watajivunia timu 1 tu iliyopita kwa uzembe wa timu yetu toka ktk bara letu linalotupa ugonjwa wa moyo,mana sidhani kama paraguay watauweza muziki wa timu bora duniani ambao bila shaka ndio anakuwa bingwa wa fifa 2010 spain usiku huu.
 
Back
Top Bottom