What is wrong with African football?

Saikolojia inatuathiri sana........................inferiority complex.............

Na hata ukiangalia zile nchi zenye majina makubwa kwenye soka nao wanakuwa na superiority complex inawasaidia sana...................kwa mfano ukiangalia mechi ya jana CMR na Dens........CMR hawakuwa na sababu ya kutoshinda ile gemu.....................na jamaa wa Dens alivyo-score lile goli la pili.............yaani nikama alijua tu kuwa hawa waafrika hawawezi kuzuia lile shuti dogo........na ikawa goli kweli................yaani inaudhi sana..................
 
....Nahisi kama EGYPT na kocha wao Mzalendo cud have done better than what we are seeing regarding African Teams!
 
jamani si timu za kiafrika pekee ambazo zinafanya vibaya .england ,italy,france wako mashakani kuingia round ya pili .ni uhakika ivory coast na ghana watafanya vizuri
 
Statistics za Mabao mpaka sasa hivi

1: Timu zote za Africa : Magoli Matano (5)
2: Brazil: Magoli Matano (5)
3: Argentina: Magoli Matano (5)
4: Ujerumani Magoli Manne (4)

Utaona kwamba Idadi ya Magoli ya timu zote za Africa ni sawa sawa na Magoli ya timu moja ya Amerika ya Kusini
 
aisee
hata nguvu za kukoment jamvini sina kabisaaa
kweli nimejiuliza sana hili swali,why afrika???ivi kutumia akili na fikra kwanza before miguvu kweli hatuna?(ingawa sio wote),mechi ya brazil vs ivory coast nilisikitika sana sema nilikua nataka niwachek tu mpira wa brazil,yani!!hamu sina kabisaaa nimesikitika sana...kwanini wengine wameweza na wana-improve sana tu sie vipi???ofkoz katika nyanja nyingi tu yani ni sifuri...

eeh Jehova ebu tuonyeshe tufanyeje?
 
Team za afrika zitafanikiwa pale tuu zitakapojifunza mpira wa kiafrika na kuzingatia nidhamu na kujitumaa zaidii katika mchezoooo....

inaumaa..ila ndivyo tulivyoooo katika tasnia mbali mbali.
 
Jamani tusilaumiane kabisa Black People...........................................Alipokuja Maximo Tanzania kwaajili ya kuinoa Taifa Stars tulimlaumu sana kuwa ameshindwa kutengeneza safu nzuri ya washambuliaji walio na uchu na magoli.Lakini kinachoonekana South kwa sasa kumbe huu ni ugonjwa wa nchi zote za Afrika kwasasa.Ghana ambayo ndio kidogo wanachechemea magoli yao yote yamefungwa kwa deadball=Penati katika game mbili,wengine wote hakuna hata matumaini.

God Bless Tanzania,God Bless Africa
Nabaki Africa one day yes
 
waafrika hatuko makini kwa kila kitu sijui ni nani katuloga na sio kwenye mpira peke yake , ili tuanze kufanya vizuri kwenye mashindano ya kombe la dunia intupasa kuanza kuwa makini katika mambo yote ya msingi mfano
elimu
utawala bora
uchumi
demokrasia na mengine mengi.
tukifanya hivyo issue ya kombe la dunia itakuwa ndogo sana. kwani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya maendeleo ya kiuchumi na mafanikio ya michezo. angalia nchi zote zinazo tamba katika medani ya michezo ni imara kiuchumi pamoja na utawala bora. brazil iliyo mfunga jana ivory cost sio tu wanajua mpira lakini uchumi wao ni imara sana , basi nasisi waafrika tuanze kuhimiza masuala ya elimu sayansi na tekinolojia tutafanikiwa kwenye michezo yote si kombe la dunia tu
 
Saikolojia inatuathiri sana........................inferiority complex.............

Na hata ukiangalia zile nchi zenye majina makubwa kwenye soka nao wanakuwa na superiority complex inawasaidia sana...................kwa mfano ukiangalia mechi ya jana CMR na Dens........CMR hawakuwa na sababu ya kutoshinda ile gemu.....................na jamaa wa Dens alivyo-score lile goli la pili.............yaani nikama alijua tu kuwa hawa waafrika hawawezi kuzuia lile shuti dogo........na ikawa goli kweli................yaani inaudhi sana..................

Tuna lack confidence...mazingira tuliokulia,malezi...huoni hata Hashim Thabit,anacheza vizuri kikapu nje ya NBA...alipoingia kule..kindendemesi kikaanza.
Nadhani ndio mana wadhungu wanapenda tuka sign mikataba huko kwao ili waongeze kiwango cha kutojiamini kwa viongozi wetu.
 
Halafu wachwzaji wa afrika wanaonekana kabisa kuwa hawajitumi, yaani mpira wanacheza kama hobi tuu.Angalia Wanigeria walivyovuruga wakati walikuwa wakishinda!

lakini cha ajabu hawa wakicheza timu za ulaya wanacheza vizuri kwelikweli, ndio maana mtu wakati mwingine unajiuliza, je wanapewa hongo na hawa wazungu?

What is wrong with us?
 
World cup iko mdomoni kwetu, tumebaki wasindikizaji, nafasi hii sijui Africa itaipata lini, nasikitika sitaweza kushuhudia kombe la dunia likibaki Africa nikiwa Hai, maana mpaka tupate tena nafasi pengine 50 years to come.
Lazima tukubali ukweli ingawa unauma sana, sisi Waafrica bado adui Ujinga hajaondoka kwetu. Nenda sehemu mbalimbali Duniani, mambo tuyafanyayo ni tofauti kabisa na Wazungu, tuendelee kujiuliza, WHAT IS WRONG WITH US?
 
Kufanyika kwa michuano hii barani kwetu nilichukulia hyo kama nafasi ya sisi walau kuingia katika hatua ya nane bora kwa timu zetu at least mbili, tatu, very unfortunate sioni timu ya kiafrika itakayo fika raundi ya pili, siioni. Poor us, poor Africans!, nahamia Brazil!
 
kama kuna mtu ambae kashaumizwa na timu za kiafrika basi na mimi nimo,yani ukishangilia ni ugonjwa wa moyo ni sawa ukipenda sana halafu siku mwenzi wako anakufanya ukose raha na itakufanya usahau tena mambo ya kupenda,na si ajabu kuona kati ya timu 6 za afrika hakuna hata moja kuingia raundi ya 2 mana hata ghana nao naanza kuwa na wasiwasi nao kutokana na mechi yao vs watu 10 australia,na kesho wanacheza na ujerumani ambae kocha wao alikuwepo uwanjani kuwasoma ktk mechi ya ghana vs australia,mwaka 2002 kweli simba wa teranga walinifurahisha sana yani walijituma na kuweka utaifa mbele wakatolewa kwa bao la kifo robo fainali,ila sasa hivi basi tushangilie ila ukisema ndio unaziwekea dhamana hazidhaminiki utapata ugonjwa wa moyo,mfano mzuri wasauzi kocha sio tatizo,ila anapangiwa na viongozi wa tff yao yani safa,hata kuachwa benny mccarthy sio yeye bali viongozi na mashabiki,ukianzia listi anapangiwa inaenda kitimu eg kaizer chiefs wacheze kadhaa na orlando pirates,halafu siasa nyingi kuliko mpira yani hiyo black economic empowerment inaingizwa sana na kiasi hata kwanza booth hachezi,huyo sibaya nae hachezi kisa timu fulani kubwa ya sauzi lazima ktk 1eleven awepo mchezaji hata kama kiwango kidogo,cameroon etoo tu ndie anajituma anakosa msaidizi,nigeria mabrazameni sitaki hata kuwasikia,ivoria nao wanalewaga sifa sana hasa walipodroo na portugal wakaona soka wanajua na wasipoangalia wanaweza hata kufungwa na north korea mechi ya mwisho japo walikula 7-0 hao north korea jana,algeria hawatabiriki wakicheza na timu kubwa ila unaweza kushangaa wakicheza na hata bongo wanafungwa,ghana nao sio wabaya sana ila nao naona wanaambukizwa ubishoo wa kuridhika na waliidharau sijui australia baada ya kuona wamefungwa 4-0 na ujerumani?
 
Guys, I think Africa was not ready for this 2010 world CUP, itakuwa aibu kama hatutafikisha hata timu moja kwenye last 16. Wazungu watatudharau zaidi.

Bad Preparations results into:-

a) Poor tactics
b) Poor defending
c) Poor discipline
d) No winning morale
d) Players are not creative when on the pitch.
e) ????
f) ????


Wafrica sisi tuna matatizo gain? What can we do to show the whole world that we’re capable of?

A) Mpira hatuwezi
B) ???? hatuwezi
C) ???? hatuwezi
D) ???? hatuwezi

Tunaweza nini?

 
Mimi sina la kusema naona tuendelee tu kuitwa shamba la bibi maana hakuna tunaloliweza kila fani ni ziro. Tuendelee tu kupokea vitu feki, adhabu hakun wenzetu wa ulaya ukikamatwa unahujumu uchumi kunyongwa Mfano wale wachina na maziwa yao lakini bongo unaundiwa tume, tume baadaye kimya hujui mwisho wake kweli unafikiri tutaweza hata hayo ya soka naona Afrika yote tuko sawa tofauti ni jinsi tunavyoanza kupanga na kumalizia.
 
mkuu sidhani kama hatukuwa tayari kwani tulijua mashindano yanafanyika wapi na lini mda mrefu sana.tulikuwa tayari lakini hivyo ndivyo tulivyo na sijui lini tutabadilika.no team work kila mtu yupo yupo kivyake vyake na ndio maana tumeshindwa kutumia advantage ya mashindnao kufanyika Africa.

Labda mda umefika kukaa mbali na makocha w akigeni pia hili tuwapate wazalendo wenye uchungu na nchi zao.hii itasaidia kupata marekebesho on time kwenye ufundi unapohitajika.
 
Africa watafuna walichopanda kutoka kwa makocha wa kithungu! Afrika kuna matatizo mengi sana kuanzia kwenye uongozi, vilabu na wachezaji wenyewe...Maandalizi yamefanyika sana ndo maana Bondeni kumependeza na kumejaa watu ..kwa upande wa timu zetu naona sijui hata niseme vp mana kama kucheza wanaweza kucheza vyema ila wanakosa vitu vichache sana wanapokuwa kwenye eneo la goli..sidhani kama ni kazi ya kocha kukufundisha jinsi ya kulenga Goli, wachezaji hawana mpango mbadala pindi mpango mmoja unaposhindwa..hawako creative na kubwa zaidi ni kujituma..kuna mengi yakuzungumzia kuhusu timu zetu.Timu zilionekana kuzima moto mwisho kama CIV walipata kocha mwezi hvi kabla kuanza mashindano hata ghana pia...
Am sick and tired of AFRICA YETU..Ngoja tusubirie kuona maajabu ya SAUZI kama mende ataweza kuangusha kabati!!
 
Back
Top Bottom