What is the meaning of PMTC1?

Mkuu @PakaJimmy, unamaanisha hiyo 1 waliyoongeza hapo ina maana ya positive? nimejribu kukusom between the lines nikahisi kama ndiyo unavyomaanisha! Au nimekusma vibaya?
Mkuu,
Umeboa!
Hii kitu haina raha yoyote kuongelea hapa majukwaani, especially kama unayemwongelea ni mwandani wako!
Una raha gani aisee?
Kakaeni kama familia na mkeo muongelee jinsi ya kukabiliana na challenge ya maisha haya na yajayo, na jinsi ya kumlea mtoto wenu mtarajiwa, na zaidi kumwepusha na tatizo!
Andamana na mkeo muwaone medical practitioners mara moja!
 
Hi GT!
my wife is pregnancy (5months) her clinic card shows she has blood group 0 and rh +ve
and PMCT1

PMTCT1 ni negative. PMTCT2 ni positive, PMTCT3 matokeo hayana uhakika na kwamba ukiona PMTCT ujue amesahau kurekodi au hana ujuzi wa kutofautisha maana ya namba hizo na hivyo anajiepusha na utata utakaotokea
 
Miongozo ya serikali inaagiza na kusisitiza kuwa mjamzito aambatane na mwenza /mume kwenda kliniki ili wote kwa pamoja wapate ushauri nasaha, wapimwe na wapokee majibu wakiwa pamoja. Vipimo wanavyopimwa kwa pamoja ni HIV status, na Syphilis (kaswende) na magonjwa mengine yatokanayo na ngono. Privatepurpose usiogope kivuli chako andamana na mkeo mpate ushauri, mpimwe na mchukue majibu ya vipimo na mpate huduma sitahiki. Mjenga nchi ni mwananchi.
 
PMTCT1 ni negative. PMTCT2 ni positive, PMTCT3 matokeo hayana uhakika na kwamba ukiona PMTCT ujue amesahau kurekodi au hana ujuzi wa kutofautisha maana ya namba hizo na hivyo anajiepusha na utata utakaotokea


Hakuna PMTCT 3....
Ipo 0,1 na 2 ( kipindi cha nyuma zilikua zinatumika rangi tatu ili kutofautisha)
0 - iwapo mama mjamzito ameshauriwa ila hajachukuliwa vipimo
1 na 2 sitopenda kuzingumzia
 
Hakuna PMTCT 3....
Ipo 0,1 na 2 ( kipindi cha nyuma zilikua zinatumika rangi tatu ili kutofautisha)
0 - iwapo mama mjamzito ameshauriwa ila hajachukuliwa vipimo
1 na 2 sitopenda kuzingumzia

thread imenisikitisha............. aksante kwa ufafanuzi mzuri.
 
PMTCT 1 ni HIV positive na PMTCT 2 ni HIV negative
Haya mambo yanachanganya sana maana wengine wanasema PMTCT 1 ni negative na PMTCT 2 ni Positive sasa nani wa kumwamini?.....Ila kuna sehemu niliona kwenye kadi ya clinic wameandika PMTCT 1N (mtoto apewe dawa) sasa sikujua wana maana gani! Haya mambo yanachanganya sana wajameni!
 
nadhani wengi sasa mshaanza kupata picha ya haya mambo lakini ni vema kwenda hosspitali na mwenza wako ili kupta ushauri wa kitaalam kuliko kukalia humu ambako wengi tunaishia kurushana roho tu!
 
Hii ndio maana ya hizo code
 

Attachments

  • 1409644819310.jpg
    1409644819310.jpg
    92.3 KB · Views: 748
Kikawaida mwanaume unatakiwa uwe wa kwanza kwenda kupima kabla wife hajaenda, ukikuta ndivyo sivyo unafanya kumwandaa mapema.

Ila kiukweli ukimwi unatisha, inabidi upate counseling ya kueleweka si mchezo.

All in all, Ukimwi wa siku hizi hauui kama zamani, ukijikubali ziko njia za kueleweka za kuishi nao.
 
Back
Top Bottom