what is it?

Mkandara ulivyosema Oman ni nchi masikini sijakuelewa. Navyojua GDP per capita ya Oman ni kubwa kuliko TZ.
Mkandara wrote "Nchi kama Oman ambazo Sultan wake alifikia kututawala sisi mbona nazo maskini"
Mkuu wangu nchi maskini sio lazima ziwe chini ya Tanzania. Oman maskini na hata ukizungumzia GDP wanazidiwa na nchi kibao maskini pia, tena basi wanalingana na Sudan tazama data zote za IMF, World bank na hata CIA upate uhakika. Kwa hiyo sii GDP inayo ashiria Utajiri wa nchi ila GDP ni kiungo kikubwa kinachowezesha kwa wenye kufahamu maana.
 
WATANZANIA UPINZANI SI KUPINGA NI KUTOA MAWAZO MBADALA
Inapofikia wakati watu wanapotoshwa kijinga jinga tu kuna hatari
taifa likaangamia au kutoweka kabisa. Kwa jinsi vyama vya upinzani
vilivyo Tanzania nachelea kusema kuwa maana ya upinzani haijaeleweka
hata kidogo na kwenye makala hii nitaweka wazi ili nieleweke vizuri
siwezi kuendelea kukaa kimya ilihali uwezo wa kuielimisha jamii ninao
kwa maana hata mwanaharakati Martin Luther King Jr anasema kuwa wale
wenye uwezo wa kuongoza wanapokaa kimya kwenye jamii sio tu kuna
hatari ya kuongozwa na wajinga ,King anasema hata mawe yatatawala ,
binafsi sioni sababu kwanini nifumbie macho propaganda zinazoendeshwa
na vyama vya upinzani ambazo kimsingi hazina tija kwa Tanzania ya leo
wala ya kesho, sasa naomba nizame kwenye mada yenyewe nayotaka
kuidadavua na kimsingi nitangulie kusema kuwa katika uchambuzi wangu
huu nitajitahidi kutoa ufafanuzi wangu kwa misingi ya hoja ili
nikibidi kujibiwa nijibiwe pia kwa misingi ya hoja na sio hoja bali
hoja zenye mantiki na mashiko pia.
Upinzani hauna maana nyingine ila kuharakisha maendeleo ya wananchi,
hata leo hii ukienda kwenye za magharibi vyama vya upinzani vimekuwa
mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo iwe kwa
kuihimiza serikali au kushiriki moja kwa moja katika kusaidia wananchi
kujiletea maendeleo sasa hii ni tofauti na kwetu ambapo vyama vya
upinzani vimekuwa mstari wa mbele kuongelea umaskini wa watu pasipo
kusaidia watu hao kujiletea maendeleo, hapa kidogo inashangaza kuona
kuwa kiu ya watu ni maendeleo sio kuambiwa wao ni maskini kwa kiwango
gani lakini cha ajabu vyama vya upinzani hawalijui ili wao wanadhani
kazi yao ni kuwaminisha watanzania kuwa ni maskini sana kuliko watu
wote Duniani na wakitaka kuwa na maendeleo kama Marekani basi ni
kuing’oa madarakani CCM huku wakishindwa kujadili kisayansi juu ya
tofauti kubwa iliyopo baina ya Tanzania na Marekani kwa maana Tanzania
ina miaka 49 ya uhuru marekani ina miaka 250 ya uhuru, usawa uko wapi
hapa?
Upinzani ni lazima kuisaidia seikali kutimiza vipaumbele vya taifa,
nakumbuka falsafa ya rais wa awamu ya tatu wa Tanzani mzee Benjamin
Mkapa aliyepata kusema kuwa, katika maisha ni muhimu kuwa na
vipaumbele lakini ukikosa kutambua kipaumbele cha vipaumbele hakika
wewe ni mjinga , hapa Mzee Mkapa anatufundisha kuwa katika maisha ni
lazima kuwa na vipaumbele kwa mantiki hiyo kwenye uwanja wa siasa za
Tanzania ni lazima kama taifa tuwe na vipaumbele ambavyo vitaungwa
mkono na watanzania wote licha ya tofauti zao za kisiasa . Mfano mzuri
ni swala la elimu , hili si jambo la kuendeshwa kisiasa hata kidogo,
si jambo la kufanywa mtaji wa kisiasa kabisa, haiingii akilini kuona
kuwa wakati serikali ya CCM imejenga shule za kata vyama vya upinzani
vinapinga tu bila kutoa hoja za msingi sababu inayoimbwa kila uchao
ni moja tu nayo ni hazina maana shule hizo hazifai kabisa. Sasa hapa
kuna mambo ya kujiuliza, unawezaje kuitwa mume bila kuoa? Au unawezaje
kuwa na shule bora bila kuwa na shule kwanza? Au tuseme unawezaje
kuwa na nyumba bila msingi kwanza?, hapa kuna hatari kuwa vyama vya
upinzani Tanzania havijui vipaumbele vya kitaifa ndio maana wanataka
kutatua matatizo ya kielimu kwa mbinu za kisiasa(they seem to solve
academic problems on the basis of political techniques) kwamba sasa
badala ya kujadili jinsi gani ya kuboresha shule za kata ili ziwe na
ubora sasa shule za kata zinataka kufanywa ndio sababu hasa ya
kuiondoa CCM madarakani, hata rais Kikwete alipata kunena kuwa
tusherehekee tofauti zetu lakini tubaki wamoja(let’s celebrate our
differences but keep our unity) hapa nacholenga kukisema hapa ni kuwa
lazima tuwe wamoja kwanza tofauti baadae(unity in diversity) na sio
tofauti kwanza umoja baadae(diversity in unity), hivyo kwa mantiki ya
kawaida nilitegemea hoja za wapinzani kuhusu shule za kata zilenge
namna ya kuboresha shule hizo na sio wimbo wa hazina maana ambao
tumeanza kuuchoka.
Ni lazima kuunga mkono mambo ya muhimu , upinzani wenye tija ni ule
unaounga mkono serikali kwenye mambo ya muhimu ambayo hayahitaji
mijadala ya kisiasa ila yanahitaji utekelezaji wa wananchi wote licha
ya tofauti zao kisiasa mfano swala la kilimo kwanza halihitaji
mijadala ya kisiasa ila utekelezaji, hapa nategemea upinzani wenye
tija kuwahimiza watanzania kuunga mkono kauli mbiu hiyo kwa vitendo na
sio kupinga pinga tu bila hoja , kimsingi vyama vya upinzani vinapaswa
kujua kuwa sio kila linaloasisiwa na chama tawala ni lazima lipingwe
huu ni ujinga mambo mengine yanafaa kuungwa mkono bila kuangalia
chama gani kimeliasisi jambo hilo, cha msingi kinachopaswa kuangalia
je jambo hilo lina tija kwa taifa?
Popularism inajengwa kwa hoja sio propaganda, hili ni jambo lingine
ambalo ni muhimu vyama vya upinzani vikalifanyia kazi kwamba
popularism(umaarufu kwa wananchi) hauletwi kwa propaganda bali hoja
ambazo zinawagusa wananchi, hapa kuna la kujifunza kutoka kwa Obama wa
Marekani ambaye umaarufu wake haukuletwa kwa propaganda bali hoja kwa
maana hatari ya propaganda huwa zinaimbwa redioni na majukwaani na
zinakinaisha lakini hoja huwa zinaishi mioyoni mwa watu na kukaa
vichwani mwao. Mara nyingin upinzani wa Tanzania umejikita katika
propaganda na sio hoja, nitoe angalizo kuwa Intelligent people discuss
ideas(wenye akili zaidi hujadili hoja), Normal people discuss
events(wenye akili za kawaida wanajadili matukio) and stupid people
discuss people(na wajinga hujadili kuhusu watu), sasa kwa kawaida
propaganga hujikita kwenye kuwajadili watu kila uchao huu kwa maana
nyingine ni ujinga, upinzani wa Tanzania unapaswa kulijua hili.
Upinzani sio upingaji, bila shaka hili ndicho ambacho kinanifanya
niamini kuwa somo la upinzani halijaeleweka Tanzania kwa maana vyama
vya upinzani vimejigeuza majukwaa ya kupinga serikali yachama tawala,
huku ni kukosa maono kwa maana mpinzani sio lazima kupinga kila mda
wakati mwingine ni busara Zaidi kuunga mkono , kutokana na hulka hii
ya kupinga vyama vya upinzani vimekuwa havipo tayari kukubali hata
matokeo ya uchaguzi , kila baada ya uchaguzi maneno CCM wameiba kura
limekuwa ni kiitikio cha wimbo maarufu wa hakuna uwanja sawa wa
kisiasa nchini. Vyama vya upinzani vinapaswa kuwa vyama mbadala na
kutoa changamoto sasa ni wakati wa kuamka na kuwa vyama vya upinzani
hai na sio kuendelea kuwa vyama vya upingaji.
Naomba nimalizie makala yangu kwa shairi langu fupi nililotunga
mwenyewe ili vyama vya upinzani waweze kukumbuka na kuzingatia haya
niliyojadili kwa maana hata wanasaikolojia mabingwa duniani wanaamini
mashairi ni moja ya njia kuu za kufanya mtu akumbuke kitu fulani,
shairi langu ni kama ifuatavyo;
UPINZANI SI UPINGAJI
1. Inafaa kutambua , maana ya upinzani
Yafaa kuzingatia, kuyaweka akilini
Haifai kukandia, walio madarakani
Kiu ya watu maendeleo, malumbano hawataki.

2. Uzalendo si kelele, ni kupenda nchi yako
Changamoto ziko tele, onyesha mchango wako
Taifa lisonge mbele, kutoka hapa tuliko
Upinzani sio kupinga, inafaa kutambua.

Makala hii imeandikwa na Novatus Kambota wa Vijana Zaidi na Kuhaririwa
na Gama , mwandishi wa makala hii anapatikana kwa anwani ya barua
pepe; novakambota@gmail.com au mtembelee kwenye blog (wavuti) yake ya;
www.novadream.blog.com


Usivyunjike moyo, hoja na changamoto unazo lakini kwa ushauri, jaribu kuwavuta wachangiaji ukiomesha pia mafanikio ya oppposition na sio kasoro zao tu. Binafsi nimechoka kusoma mambo ya ushabiki, kama ni spamm basi ni wale washabiki wa vyama vyao, wasiotaka kusikia makosa kuhusu chama chao. Hao ndio spamm hapa JF, na wengine ni bendera fuata upepo... Hawana hoja bali vitimbi, by now you know that hapa JF majority ni Chadema....SEMA USIOGOPE
 
mail
Naona hoja imehama bwana imekuwa sio maana ya upinzani tena ni kuhusu mimi kutafuta girl................aah...........binafsi sidhani kama hilo lililoibuliwa litatusaidia kuelewa maana ya upinzani hebu tujadili mambo ya msingi..............nimechambua kwa hoja inabidi nijibiwe kwa hoja sio mzahamzaha .........tuchambue mambo yenye tija kwa taifa ......tujadili kwa mantiki mzaha sio mda wake huu.............kama umeshindwa mada haijaeleweka ni heri kaa pembeni kwa maana kujiuzulu sio udhaifu tu wakati mwingine ni ujasiri kuyaacha yapite(resigning does not only mean you are weak , sometimes it means you are strong enough to let it go)

Kichwa cha Panzi kinafikiria kula majani
 
"WATANZANIA UPINZANI SI KUPINGA NI KUTOA MAWAZO MBADALA
Inapofikia wakati watu wanapotoshwa kijinga jinga tu kuna hatari
taifa likaangamia au kutoweka kabisa.
Kwa jinsi vyama vya upinzani
vilivyo Tanzania nachelea kusema kuwa maana ya upinzani haijaeleweka
hata kidogo na kwenye makala hii nitaweka wazi ili nieleweke vizuri
siwezi kuendelea kukaa kimya ilihali uwezo wa kuielimisha jamii ninao
kwa maana hata mwanaharakati Martin Luther King Jr anasema kuwa wale
wenye uwezo wa kuongoza wanapokaa kimya kwenye jamii sio tu kuna
hatari ya kuongozwa na wajinga ,King anasema hata mawe yatatawala ,
binafsi sioni sababu kwanini nifumbie macho propaganda zinazoendeshwa
na vyama vya upinzani ambazo kimsingi hazina tija kwa Tanzania ya leo
wala ya kesho,
"
:confused2:
1. How can you differentiate hoja mbadala from the obsolete ones without criticism?
2. I think Martin Luther King Jr. has been quoted in the wrong article with the motives contrary to what he stood for.
3. Kwa mtu mwenye akili timamu haitaji kuambiwa ni nani anayepotosha watu kijinga kati ya CCM na upinzani
4. Propaganda???? What about the "preachings" of Mzalendo, Uhuru, Habari Leo, Daily News & Co..."bright future" for Tanzanians huh?
We have the watch and we have the time as well, too late for brain wash
 
Mtoto anaandika mambo mengi!!!! We don't have the luxury of reading all that cheap staff young man. Try to be brief and focused. Kafanye hiyo exercise and when you are done please come back again, ok?
 
mail
Kwa kawaida hatujibu hoja kwa jazba wala kwa kuzifupisha wala vitisho wala kwa maswali.............huku ni kukosa maoni kwa maana mimi nimetoa hoja inabidi zijibiwe kwa hoja sio vinginevyo.
 
Back
Top Bottom