What does this picture say about Us the People?

Unajua hiyo picha ya mtoto hapo nyuma huo mlango unaniacha na maswali ya kifalsafa:

a. Ukiingia unatokea wapi?
b. Huko unakotokea na kule unakoingia kuna tofauti gani?
c. Ni bora kuwa upande gani wa mlango?
 
Kwa jinsi akili za watawala wetu zilivyo usishangae ukisikia ikiundwa tume ili kuchunguza sababu zinazofanya uchafu kurundikana katika jiji la DAR
 
Waone SUMTRA NA POLICE walianza kukomalia reckless daladala bila kujua ya kwamba ni za watawala. Akatokea mjinga mmoja anaitwa Lukuvi Rais waw DAR akawapiga stop. Initialy wakambana akayield but only for a week, lakini Baadae akaenda kaa na kamati ya siasa wakaambiana huu ni mwaka wa uchaguzi so kill the Majembe Contract for a while mpaka tupate kura and you see Majembe wakingia mtini na fujo za vipanya na bajaji ziko pale pale .



huu ni usanii mwingine, kaazi kwelikweli.
 

So take it as a lesson hawa majambazi wako tayari kutoa kafara maisha ya watu ili mradi tu washinde therefore uchafu is here to stay unless tutumie mbinu ya fatmas otherwise imekula kwetu na tutachonga sana!!!!

Mkereme, hawa watu ni wauaji. Hawana tofauti mafia mob; kwa ufupi ni genge ja majambazi waliolewa na mazoea. Sikati tamaa, najua ukombozi wa kweli umefika.:mad:

Amandla...
 
Tuko mbioni kumpata msaada kutoka kwa wahisani wa kutusafishia jiji letu.Lol
 
Imagine kiongozi mkuu wa mkoa anajisikiaje na matatizo haya ambayo jibu lake haliko mbali na kuta nne za ofisi yake.Inawezekana waafrika ndivyo tulivyo, lakini kuna mambo mengine mimi sifanani kabisa na hawa watawala. Niko some steps ahead.Duuh, shabash!
 
Tumeshazoea kufanyiwaa tuuu..Kwa madhari ya hayo mazingira natumai kuna jamii inayoishi eneo husika na bado hatuoni ni tatizo au suluhisho la kero hiyoo..lazima lawama za mwanzo tuwapelekee viongozi kwani wenyewe hatuwezi kujiongozaa..lol..

Lile somo la usafi wa mazingira katika shule za msingi halikuishia kunawa mikono tuu kabla na baada ya kula!!!
 
Je tuanzishe kampeni ya usafi bila kuhusisha wafadhili?
Mzee gone are the good old golden days ambapo wananchi kwa taarifa kutoka kwa Mjumbe wa Nyumba Kumi na bila mikwala yoyote tulikuwa tukitoka na fagio za chelewa tukiimba nyimbo za "AAAH! TANU YAJENGA NCHI" na kufanya usafi mitaani kwetu!
 
mfumwa inawezekana huo uchafu hautoi harufu au wenyewe wameuzoea kiasi kwamba hawasikii harafu?

wao wenyewe watakuwa wananuka...kama sio uchafu basi wananuka rushwa.
ukiishi jalalani na wewe unakuwa uchafu kwa sababu utanuka, kama hutanuka basi ukizoea harufu maana yake utakuwa unanuka ubogo.....ubongo umekubali kunuka kwa niaba ya mwili.
 
Na bila kuhusisha Mayor na serikali ya CCM?

Nasikia Rais Kagame wa Rwanda ana utaratibu wa yeye na familia yake (wote wanaoishi nyumbani kwake) mara moja kwa wiki kutoka na kujumuika na wananchi kufanya usafi mitaani. I can't imagine that happening here. Acha JK. je, Kimbisa na maafisa walio ofisini kwake wanaweza kuonyesha mfano kwa kubeba zana za kufanyia usafi na magari ya kunyonya maji machafu na kwenda kushughulikia uchafu na hayo maji yaliyotuama anayoyaruka kijana huyo? It can be done it is only a matter of playing our parts effectively!
 
Inaonyesha "si jukumu la yangu"
It tells "it is not my responsibility"
Il dit "que ce n'est pas ma responsabilité"
Esto dice "que esto no es mi responsabilidad"

Sijui niseme kwa lugha gani! In a plain and simple language that pic tells no one is there for service of this country! sasa kama hapo ni Kariakoo! You dont tell me nobody hasnt that! Wahusika wanalifahamu, why should I bother!!! An irrational behaviour and selfish of its own.
Hivi ni lini tutaona sheria zetu zinafanya kazi! Maana mambo yote haya ni sheria kutofanya kazi, Huu ni uzembe na kutotimiza wajibu na kama mtu hatimizi wajibu Get rid of Him! Lakini kwa sababu pesa imeliwa na bosi mwenyewe Bosi atapata wapi nguvu ya kusimamia sheria!
 
Tatizo si uongozi ingawa nao una play part kubwa tu tuanze na sisi wenyewe mtu una kula ndizi maganda unatupa barabarani hapo utasema ni uongozi fikiria watu mia wakifanya hivyo tayari unakuwa mlundikano wa taka chukulia picha hii familia za polisi pale msimbazi nyingi hutupa uchafu wao tokea madirishani kwa hiyo tunapotupia lawama sheria zetu na wanaotakiwa kuzisimamia tujiulize je sisi tunawajibika vipi
 
Tumezoea uchafu katika miji yetu hasa Dar, sasa inakuaje mkuu wa kaya anasema kuwa anataka barabara za juu wakati hata uchafu tu ni matatizo kama haya
 
Tatizo si uongozi ingawa nao una play part kubwa tu tuanze na sisi wenyewe mtu una kula ndizi maganda unatupa barabarani hapo utasema ni uongozi fikiria watu mia wakifanya hivyo tayari unakuwa mlundikano wa taka chukulia picha hii familia za polisi pale msimbazi nyingi hutupa uchafu wao tokea madirishani kwa hiyo tunapotupia lawama sheria zetu na wanaotakiwa kuzisimamia tujiulize je sisi tunawajibika vipi

Could it be that people are frustrated and they do not care any more?
 
Kumbe jamaa unamjua ukimbana zaidi anasema mimi ni lecturer hapo chuoni au mimi nachukua kozi hiyo huku marekani kazi zote ni zake sijui huwa anazifanya vipi kwa wakati mmoja ana tabia ya kujiboss sana

ha h aha,

hiyo ya u-lecturer nilikuwa sijaisikia ila sitashangaa. Waberoya kwake kila kitu kilichoharibika hapo Tanzania kimesababishwa na wapinzani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom