What about R&D?..The Case of Foreign Aid Influx & 'A Japanese Expert' Invite

inachekesha (absurd) sana...................pale siku manabii watapokubalik pale mahala watokako ndio tutapiga hatua kama Japan na Malaysia

Hazina tunazo.....TUMEKOSA UTASHI wa kila aina wa uwajibikaji na utekelezaji

......mfano mdogo....JF tukisema tunaitwa MAGAIDI.................akina Lowassa wakituletea mvua za Thailand na Richmond wanaitwa HEROs na kupokelewa na zulia jekundu na Askofu kumsindikiza.......what a shame!!
 
Na wale wataalamu wa kilimo toka Ukiriguru, Ilonga na Uyole watakuwa na kazi gani sasa kama tutaita Wajapani kutufundisha kulima kwa maksai ama matrekta? Ina maana hatuna wataalamu nakwa hili pia?
Amazing!
 
inachekesha (absurd) sana...................pale siku manabii watapokubalik pale mahala watokako ndio tutapiga hatua kama Japan na Malaysia

Hazina tunazo.....TUMEKOSA UTASHI wa kila aina wa uwajibikaji na utekelezaji

......mfano mdogo....JF tukisema tunaitwa MAGAIDI.................akina Lowassa wakituletea mvua za Thailand na Richmond wanaitwa HEROs na kupokelewa na zulia jekundu na Askofu kumsindikiza.......what a shame!!

Kumbuka tulitaifisha viwanda vingi sana vikawa vya umma tulianzisha pia viwanda vya umma licha ya tulivyotaifisha, viko wapi? vilivyobaki ambavyo hatujaviua kabisa tunaona leo vimebinafsishwa na vinatoa faida ambayo vilipokuwa vya umma vilishindwa kabisa. Wakati ule wa viwanda vya umma tulikimbilia china na wakaleta wataalamu wao na kutuwekea viwanda kwa kuwa siasa yetu ya wakati ule ilishabihiana na ya wachina.

Leo mambo yamebadilika, si kwetu tuu, hadi huko china. Tupo kwenye mfumo wa u-capitalist na waJapan kwa hilo ndio usiseme. Sasa kuna ubaya gani tukiwaita wataalamu wao waje kutowa ushauri? Mbona hapa kwetu tunabingwa ambao wanaitwa mpaka nje ya Tanzania kutowa ushauri? hata huko china amabako kuna-maendeleo makubwa lakini tunafahamu kuwa kuna wataalamu wa viwanda kutoka Japan na waJapan wanaviwanda walivyowajengea wa China huko huko China.

Kwwa hili msitake ubishi wa ili-mradi kubishana, mbona mpaka sasa tuna wataalamu wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani ambao wako hapa Tanzania, inakuwa nongwa tu pale ambapo inasemwa kuwa hii inatokana na JK alipotembelea Japan? Kunani jamani? mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Kama hatuna wataalamu wa mikataba nadhani kuna uwezekano kuwa pale SUA hakuna mtu ambaye amewahi kusikia "agro-mechanics".. hivyo nadhani ni bora tulete wakufunzi wa mambo hayo...
 
Kama hatuna wataalamu wa mikataba nadhani kuna uwezekano kuwa pale SUA hakuna mtu ambaye amewahi kusikia "agro-mechanics".. hivyo nadhani ni bora tulete wakufunzi wa mambo hayo...

Kusikia, kutenda ni vitu tofauti hata kama si mtaalam unaweza ukasikia, kutenda jee? mbona yalitushinda maviwanda, mashamba, mabenki, mpaka tukaamuwa kuyarudisha kwa "wawekezaji" sasa tunacholalamika nini? ingekuwa hatujawa na fursa au kwa kuja huyo mjapani ndio kunazuwia fursa za wataam wetu?
 
ndio hivyo wanakuja hao wa Japan kutazama wapi tunapokosea watushauri, tukifata haya tusifate haya. They have got nothing to lose.

Hakuna lolote kwani sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo...hata waje wataalamu mamilioni hakuna lolote la maana litakalotokea.
 
Kama hatuna wataalamu wa mikataba nadhani kuna uwezekano kuwa pale SUA hakuna mtu ambaye amewahi kusikia "agro-mechanics".. hivyo nadhani ni bora tulete wakufunzi wa mambo hayo...

Ni kweli kabisa, kuchukua wataalamu toka nje ni matumizi mabaya ya rasilimali watu (katika kilimo) tuliyo nayo!
 
Miafrika bana tunashangaza sana...eti hadi namna ya kuzalisha msosi lazima tufundishwe....
 
Miafrika bana tunashangaza sana...eti hadi namna ya kuzalisha msosi lazima tufundishwe....

Na wale waTaalam wetu waliopo nje ya Afrika wakitowa ushauri? Kumbuka hakuna ajuwae kila kitu ndio maana kuna kushauriana kuna kubadilishana mawazo, haya ni mambo ya kawaida kabisa duniani mimi nawashangaa nyinyi mnayoyaona kuwa ni mageni, hata sijuwi mnaishi dunia gani, ya kusadikika?
 
Sasa kwa nini hayo mataalamu yasirudi Afrika kusaidia kuleta maendeleo?

Ni kweli hakuna ajuaye kila kitu lakini usiniambie katika mijitu millioni 40 hatuna watu wanaojua mambo ya kilimo.
 
Sasa kwa nini hayo mataalamu yasirudi Afrika kusaidia kuleta maendeleo?

Ni kweli hakuna ajuaye kila kitu lakini usiniambie katika mijitu millioni 40 hatuna watu wanaojua mambo ya kilimo.

Duhhh, umeshindwa kunifahamu kabisa, kwanza wataalamu ninaoongelea mimi ni wale ambao wanaishi Tanzania na kutakiwa kutowa ushauri wao nje ya hapa, si tu kuwa huko wanakokwenda hakuna wataalam, no, wapo lakini kupeana ushauri ni wajibu wa ubinadam.

Siwezi kukwambia kuwa "katika mijitu millioni 40 hatuna watu wanaojuwa mambo ya kilimo" bali ntakukumbusha:

1) mashamba ya mbarali, yalipoanzishwa na wachina yalikuwa yalizalisha vizuri sana mpunga, walipoondoka yamekufa kuzalisha na wataalamu wetu wa kilimo walikuwa wapi?

2) Mashamba ya ngano ya katesh, hali hiyo hiyo, haya yalianzishwa na wa-canada.

3) Mashamba ya mkonge, haya tuliyataifisha kutoka kwa watu mbali mbali wengi wao wakiwa wagiriki na yapo zaidi Morogoro na Tanga, yalikufa kabisa, baada ya kupewa wawekezaji, tunaona yanafufuka. Kulikoni na waTaalam wetu?

Kwa hayo inabidi tupate ushauri, kwa nini tushindwe? labda there is something very wrong with us? what is it? tungoje washauri wanasemaje, tukifata tusifate ni shauri letu. Kwa hili la kutaka ushauri unaweza kunipa ubaya wake? wakati wenyewe tunafanya madudu?
 
Back
Top Bottom