What about R&D?..The Case of Foreign Aid Influx & 'A Japanese Expert' Invite

Nyani hapo pa "sweat, blood, and tears" panawezekana Ulaya huko Tanzania mtu ahenyeke kisa nini? nadhani "Waafrika ndivyo tulivyo" tunapenda vya kunyonga, vya kuchinja hatuviwezi.

Mkuu MMKJJ,

Hivi unafikiri Prof.Dr. James Watson alikuwa na makosa aliposema kile alichosema in 2007?Mi nafikiri na napenda kuungana na Watson kuwa something is wrong with us in our biological/DNA make-up!!licha ya watu (na baadhi ya wazungu) kumponda Watson kuwa ni mbaguzi,alichosema kinahold water,ebu tazama tu jinsi watu pale Tabata Dampo sasa wanalala nje kwa vile makazi yao yamebomolewa kwa "kuvamia ardhi ya mtu"!!BoT mapesa yanachotwa tu ambayo yangeweza kabisa kuziba nyufa hizi za umasikini wa kujitakia,tuna maprofessor kibao kwenye serikali na vyuo ambao wameishia kuvizia na kudandia semina na warsha tu basi...damn it James Watson is right 100%,tena kwa wasomi wa (wanaojiita maprofesa na madokta) kiafrika nadhani Wtason angejaribu pia kupima bongo zao maana hao ndio ovyo kabisa
 
Umesoma historia lakini? Hao wa Enron nao ni waafrika? Lord Black anayeanza kifungo naye ni muafrika? Kila jamii ina watu ovyo si waafrika peke yao.
 
Umesoma historia lakini? Hao wa Enron nao ni waafrika? Lord Black anayeanza kifungo naye ni muafrika? Kila jamii ina watu ovyo si waafrika peke yao.

Fundi, I did read history well,lakini hata nisingesoma bado ukweli ujko wazi,hebu jaribu kulinganisha cases (chache sana) kama hizo za Conrad Black,Enron,yule Rogue Trader wa Soociete Generale etc, na ulinganishe na BoT yetu,Kiwira,Tanesco,Richmond,the so called mashirika ya umma,TRL,TISCAN...damn the list is interminally endless!!!Pia kwa maelezo yako hapo juu kuhusu Enron na Lord Black unaungana na Watson kuhusu waafrika,wazungu are very swift in action,Black kafanya madudu sasa yuko jela hivyo hivyo kwa maboss wa Enron,sisi je?Jeethu patel yuko wapi?Ballali,Chenge,Msabaha,Mkapa, Karamagi,Rostam,ect?...Fundi need I say more?
 
Kama umesoma historia kweli utajua kuwa nao walifanya udhalimu kama huu walipokuwa katika hatua ya maendeleo tuliyokuwa nayo sisi. Imewachukua muda mrefu kujenga institutions hizo tunazozisifia. Najua mtu ukiangalia madudu yanayofanywa si tu na waafrika bali ndugu zetu wenye rangi kama yetu unatamanishwa kukubaliana na Dr. Watson. Hiki mimi ndicho ninachokipinga. Nakataa kuwa defined na hao walio nitawala pamoja na watu kama hao uliowataja. Watu weusi tunahukumiwa kutokana na vitendo vya wakina Mugabe lakini wakina Stalin, Hitler, Ceausescu, Slobodan Milosevic, na wale walio wa'lynch' watu weusi marekani hawaonekani kuwa ni mfano wa watu weupe! Tuwashughulikia hao waovu walio kati yetu kwa vile hao si mfano wetu! Tukikubali ya wakina Dr. Watson basi hatuna budi tuache kuwakemea maana ndivyo tulivyo. Huko sitakubali kwenda.
 
Ibambasi, you are damn right!

Wazungu na waasia wakifanya uhuni na ujinga hupata kibano bila kujali nafasi zao. Sisi kwetu wezi wenye tai na kutumia mashangingi, yakiwa na nembo ya taifa hushangiliwa, huabudiwa, hutetewa na kusafishwa na vyombo vya dola, mpaka na maaskofu.

Hiyo ndiyo tofauti yetu sisi nyani(sorry if offended) na rangi nyingine.

Waafrika ndivyo tulivyo.
 
Umesoma historia lakini? Hao wa Enron nao ni waafrika? Lord Black anayeanza kifungo naye ni muafrika? Kila jamii ina watu ovyo si waafrika peke yao.

Ni kweli, lakini si unaona hawa umesema mwenye kwamba wameenda jela, sisi je? Kote kuna watu wabaya na wazuri, tofauti ni kwamba sisi wenzetu wakimpata mbaya humshughulikia wakati sisi huwa tunawakumbatia!
 
Tunalinganisha apple na chungwa. Hawa tunaowasujudu sisi manyani (kama invisible alivyotuita) walipokuwa katika hatua yetu ya kimaendeleo walifanya ufisadi na uovu kama huo tunaoufanya sisi. Hizo taasisi zinazowapeleka jeshi zimetokana na umwagaji wa damu na mapambano makubwa kati ya wale waliokuwa mafisadi na watu wa kawaida. Hayo maendeleo yanayowafanya wananchi wao wasifanye wizi wa kijinga tunaoufanya sisi umetokana na kukamua na kugadamiza sehemu kubwa ya jamii iliyo na rangi tofauti na wao! Hatuwezi kujilinganisha hata siku moja na huko waliko. Hii haina maana kuwa siyaoni hayo maovu ambayo mtu mweusi anayoyafanya dhidio ya mtu mweusi mwingine. La hasha, nayaona na pengine yananiumiza kuliko wengi mliomo humu. Huo mtazamo wenu wa kudai kuwa sisi wetu weusi tumelaaniwa tangu tuzaliwe ni njia ya mkato ya kufurahisha genge. Naam, tu waovu, naam tu wezi, naam tuna uwezo wa kufanya ukatili usioeleweka, naam tunatabia ya kukumbatia vi petty tyrants miongoni mwetu na mengineyo. Lakini hatuzaliwa hivyo. Tumefikishwa hapo na mfumo ambao ulimfanya mtu mweusi afikie kuamini kuwa yeye aliye kizazi cha Ham amelaaniwa na hana jinsi ya kujitoa katika hali hiyo! Kujiita nyani, nigga si dalili ya ushupavu bali ni maendelezo yale yale ya kutojithamini tuliopachikwa na waliotutawala! Ni katika uhai wa wengine wetu hapa ambapo ilikuwa halali kumuua mtu mweusi kwa vile amemwangalia mwanamke wa kizungu vibaya! Ni hivi karibuni tuu ambapo mtu mweusi alikuwa haruhusiwi kuishi pamoja na mtu mweupe huko Afrika ya Kusini. Hao mnaowaabudu walipotuacha, walituacha na mawakili wawili, wahandisi wanne na madaktari 12 nchi nzima. Hizo institutions ambazo zingeweza kuwashughulikia hao waovu zingejengwa vipi kwa mtaji huu? Mimi bado naamini kuwa iko siku watu wangu watajikwamua katika hili janga la umasikini, ufisadi na uonevu uliokithiri. Nikiacha kuamini hivyo itakuwa heri nife.
 
Kwa wakina Nyani Ngabu,

Tusisahau tulikotoka. miaka karibu 30 baada ya muingereza kuchukua nchi, tulikuwa na shule moja yenye kutoa mafunzo ya sekondari nchi nzima na ilchukuwa wanafunzi sita tu. Miaka 41 ya utawala wa muingereza tulikuwa na graduates 70. Katika hao madaktari hawakuzidi kumi. Sijui kama wahandisi walifika watano! Miaka 41 ya kujitawala wenyewe, tunaexport madaktari Botswana,wahandisi wako kwenye mamia (kama sio maelfu), wasomi wetu wa nyanja mbalimbali wameenea dunia nzima. Leo hii maelfu ya watoto wetu wako kwenye vyuo vyetu vikuu wakitafuta elimu.

Frantz Fanon alisema ( si kwa maneno haya haswa) kuwa dhambi kubwa aliyofanya mkoloni ni kuwafanya waliowatawala kuamini kuwa wao wameumbwa duni kuliko huyo anayewatawala. Mtawaliwa hataweza kujikomboa hadi hapo atakapoikabili na kuiondoa imani hiyo ndani yake mwenyewe. Itachukua vizazi vingi mpaka sisi wenye ngozi nyeusi kuweza kuondoa sumu hii tuliyowekewa kwa takhriban miaka mia tano. Hii si sababu ya kukata tamaa.

Katika miaka ya sabini kuna mwandishi wa habari mmoja alimhoji mwanamapinduzi wa ANC kuhusu mapambano yao yasio na tumaini dhidi ya utawala wa makaburu. mwanaharakati huyo akamjibu " tulipoanzisha Umkhonto we Sizwe mwaka 1961 tuli'estimate' tutamng'oa kaburu katika miaka miwili which I think was a pretty good estimate! Yule mwandishi akasema hapo ndipo alipotambua kuwa hawa jamaa wata'prevail'.

pengine si kesho wala kesho kutwa lakini najua iko siku sis watu weusi tusimama bega kwa bega na wale waliotufananisha na tumbili!

Aluta Continua.

Fundi Mwenzagu:

Unaleta siasa sasa. Na siasa ndio iliyotuingiza mav!n!. Digrii kwa miaka ya nyuma kilikuwa kitu nadra. Hata nchi zilizoendelea digrii zilikuwa sio za kupewa kila mtu.

Watu wanaosema NDIVYO TULIVYO wana point za maana sana. Na ku-play victim card hazitusaidii. Ni lazima tueleze matatizo ya kuanguka kwetu kwa kutumia vigezo ambavyo vinakosoa mapungufu yetu kuliko kuendeleza vigezo kuwa sisi hatukuwa na wasomi au tulinyanyaswa. Hata makabila ya kijerumani, celtic yalikuwa chini ya utumwa wakati fulani.

Katika vitabu vyote vya siasa na historia tulivyosoma suala na wenye digrii kuwa ni wachache lilikuwa halitajwi. Inakuwaje leo zaidi ya miaka 40 toka tumepata uhuru tunajitetea kwa kusema kuwa idadi ya wasomi ilikuwa ndogo.

Suala la Tanganyika kupata uhuru mapema bila kuwa na wasomi wa kutosha lilikuwepo mezani. Na tulikuwa na uwezo wa kujadiliana na umoja wa mataifa katika masuala haya.

Sehemu kubwa tuliyoboronga baada ya uhuru ni elimu. Ndio nchi iliweza kufuta ujinga lakini gharama za kufuta ujinga ziliambatana na kupungua kwa kiwango kikubwa cha elimu. Na suala hili lilikuwepo mezani vilevile. Wataalamu wa elimu walisema mipango ya kufuta elimu ichukue miaka 20 lakini wanasiasa wakasema miaka saba inatosha.

Mashamba makubwa ya chai au mkonge yaliendesha na wageni wasio na digrii. Yalitaifishwa na kuongozwa na watu wazawa wenye digrii. Na haikuchukua zaidi ya miaka saba kwa mashamba hayo kufa. Wanaosema NDIVYO TULIVYO wana-point katika vitu ambavyo vimefanyika baada ya uhuru.

Tanzania ilisaidia na Sweden karatasi za bure kuchapisha vitabu vya elimu ya watu wazima. Vitabu vingi vilivyochapishwa vilijaa siasa na viliwekwa kwenye makabati tu, watu wamefungia vitumbua na hakuna mabadiliko ya maana mtu anaweza kuonyesha mipango hiyo ilikuwa na mafanikio gani.

Makao makuu Dodoma ilianza kujengwa kabla ya watu wengi hapa JF kuzaliwa na bado inaendelea kujengwa na mapesa kibao yamepotea. Na haya yamefanyika katika Tanzania huru na yenye wasomi.

Mzani wa maendeleo haupimwi na wasomi wangapi mkoloni aliacha na wasomi wangapi tunao sasa. Na kama tunakubali kutumia wasomi basi ni lazima tutumie kigezo cha ufanisi (PERFORMANCE). Performance wakati wa mkoloni ilikuwa kubwa kuliko wakati wasasa.

Na vilevile kusema kuna watanzania wanaofanya kazi Botswana inaonyesha ni jinsi gani nchi isivyovutia wasomi wake. Na vilevile hilo sio suala la kujifunia kwani Ethiopia ambayo haikutawaliwa ina wasomi wengi sana tena katika nchi zilizoendelea kuliko Tanzania. WaEthiopia waliosoma mjini Washington DC ni kubwa kuliko ya watanzania waliopo Botswana.

Mambo yatakayotusaidia ni kujikosoa na sio ku-play victim card au ku-point vi-mafanikio fulani vya hapa na pale.
 
With all due respect, nyinyi ndiyo mnaoleta siasa. Kwa kusema NDIVYO TULIVYO mna'cop' out kwenye kuchukua responsibility maana kama mmelaaniwa kwa nini mjitahidi kujinasua! Mimi nakiri matatizo yote hayo yanoyowakera nyinyi lakini nakataa kumtupia lawama muumba kwa mambo yaliyonikuta. Nawalaumu binadamu wenzangu ( weupe na weusi) kwa matatizo haya. Ninaamini kuwa nikijitahidi nitajikwamua pamoja na juhudi zote za downpressas hawa. Kwa kusema kuwa weupe wamechangia kwa kiasi kikubwa kunifikisha hapa hakuna maana kuwa nangojea Marshall kwa ajili ya Afrika. Haitatokea pamoja na kwamba 'they owe us'. Tukubali tuliyotendewa, tujifunze kutokana nayo na tuwakemee wale wote wanaotaka kutubakiza katika hiyo hali kwa vile HIVYO NDIVYO TULIVYO!
 
Fundi Mwenzagu:

Unaleta siasa sasa. Na siasa ndio iliyotuingiza mav!n!. Digrii kwa miaka ya nyuma kilikuwa kitu nadra. Hata nchi zilizoendelea digrii zilikuwa sio za kupewa kila mtu.

Watu wanaosema NDIVYO TULIVYO wana point za maana sana. Na ku-play victim card hazitusaidii. Ni lazima tueleze matatizo ya kuanguka kwetu kwa kutumia vigezo ambavyo vinakosoa mapungufu yetu kuliko kuendeleza vigezo kuwa sisi hatukuwa na wasomi au tulinyanyaswa. Hata makabila ya kijerumani, celtic yalikuwa chini ya utumwa wakati fulani.

Katika vitabu vyote vya siasa na historia tulivyosoma suala na wenye digrii kuwa ni wachache lilikuwa halitajwi. Inakuwaje leo zaidi ya miaka 40 toka tumepata uhuru tunajitetea kwa kusema kuwa idadi ya wasomi ilikuwa ndogo.

Suala la Tanganyika kupata uhuru mapema bila kuwa na wasomi wa kutosha lilikuwepo mezani. Na tulikuwa na uwezo wa kujadiliana na umoja wa mataifa katika masuala haya.

Sehemu kubwa tuliyoboronga baada ya uhuru ni elimu. Ndio nchi iliweza kufuta ujinga lakini gharama za kufuta ujinga ziliambatana na kupungua kwa kiwango kikubwa cha elimu. Na suala hili lilikuwepo mezani vilevile. Wataalamu wa elimu walisema mipango ya kufuta elimu ichukue miaka 20 lakini wanasiasa wakasema miaka saba inatosha.

Mashamba makubwa ya chai au mkonge yaliendesha na wageni wasio na digrii. Yalitaifishwa na kuongozwa na watu wazawa wenye digrii. Na haikuchukua zaidi ya miaka saba kwa mashamba hayo kufa. Wanaosema NDIVYO TULIVYO wana-point katika vitu ambavyo vimefanyika baada ya uhuru.

Tanzania ilisaidia na Sweden karatasi za bure kuchapisha vitabu vya elimu ya watu wazima. Vitabu vingi vilivyochapishwa vilijaa siasa na viliwekwa kwenye makabati tu, watu wamefungia vitumbua na hakuna mabadiliko ya maana mtu anaweza kuonyesha mipango hiyo ilikuwa na mafanikio gani.

Makao makuu Dodoma ilianza kujengwa kabla ya watu wengi hapa JF kuzaliwa na bado inaendelea kujengwa na mapesa kibao yamepotea. Na haya yamefanyika katika Tanzania huru na yenye wasomi.

Mzani wa maendeleo haupimwi na wasomi wangapi mkoloni aliacha na wasomi wangapi tunao sasa. Na kama tunakubali kutumia wasomi basi ni lazima tutumie kigezo cha ufanisi (PERFORMANCE). Performance wakati wa mkoloni ilikuwa kubwa kuliko wakati wasasa.

Na vilevile kusema kuna watanzania wanaofanya kazi Botswana inaonyesha ni jinsi gani nchi isivyovutia wasomi wake. Na vilevile hilo sio suala la kujifunia kwani Ethiopia ambayo haikutawaliwa ina wasomi wengi sana tena katika nchi zilizoendelea kuliko Tanzania. WaEthiopia waliosoma mjini Washington DC ni kubwa kuliko ya watanzania waliopo Botswana.

Mambo yatakayotusaidia ni kujikosoa na sio ku-play victim card au ku-point vi-mafanikio fulani vya hapa na pale.

1. Tunazungumzia mwaka 1961 sio mwaka 1661! Nchi zilizoendelea zilikuwa tayari zina vyuo na institutions zilizokomaa wakati walipotuacha sisi na wahandisi wanne.

2. Hawa walikaa miaka 41 bila kufanya lolote bado unaamini kuwa wangekaa zaidi ndiyo wangetujengea vyuo?

3. Hao hao waliomuona mwalimu mpuuzi kusisitizia kuwekeza kwenye elimu na social issues leo wamegeuka na kukubali kuwa bila kuwekeza katika sehemu hizo hakuna maendeleo. makosa yalifanyika ndiyo, lakini si katika kufanya asilimia karibu 80 ya watanzania wajue kusoma na kuandika.

4. Mashamba hayakuendeshwa na wazawa walio na digrii. Hao walikuwa wachache sana wakati wa Azimio la Arusha. Pamoja na hayo sipingi kuwa tulifanya makosa kutaifisha mashamba lakini hii haina maana kuwa tumelaaniwa. Mashamba hayakufa katika muda huo unaoutaja. mashamba haya yalikufa kama yalivyokufa mashamba mengi yaliyoendeshwa kijamaa hata huko kwa wazungu. Mfano mzuri ni USSR na Uchina.

5. Uzembe mwingi ulifanyika katika sekta ya elimu. Si hiyo tuu ya kutokuchapisha vitabu vinavyohitajika. wakati mimi nasoma ilikuwa hauwezi kwenda A-level kama haujafaulu masomo ya siasa na kiswahili. Ilikuwa ni lazima mjumbe wa nyumba kumi akupitishe ili uweze kwenda ng'ambo kwenye masomo ya ziada. Lakini haya ni matatizo ya sera na si ya ethnicity.

6. Mradi wa makao makuu umefanyika kisiasa ni makosa. Kama vile warusi walivyokausha ziwa lao kubwa kwa ajili ya mradi wa kilimo . Au wachina na zoezi la vita za utamaduni za Chairman Mao. Wote walifanya makosa ya kiitikadi na si rangi.

7. utakuwa unajidanganya kama utakana kuwa idadi ya wasomi na uwezo wa kujiendesha tulioachiwa na watawala wetu haukuwa na impact katika hali yetu ya sasa. hiyo performance unayoizungumzia wakati wa wakoloni ni ipi? Hali ya Native ilikuwaje. Ni kama kusema afrika kusini ilikuwa na hali nzuri wakati wa Apartheid kuliko sasa. kwa watawala labda lakini si kwa jamii yote.

8. Siwezi kukubishia kuhusu ethiopia. lakini hawa nao si waafrika kama sisi? au wahabeshi si nyani?

9. Tutaweza kujikosoa pale tu tutakapokubali hali yetu halisi, historia yetu na bila kutafuta hivi visingizio vyenu kuwa ndivyo tulivyoumbwa. Tutakapokataa kujiona tumelaaniwa na kudai kuwa tupimwe kama binadamu mwingine ndipo safari itakapoanza. Na safari hii ni ndefu na ina suluba nyingi lakini tukipania tutafika.
 
Ibambasi, you are damn right!

Hiyo ndiyo tofauti yetu sisi nyani(sorry if offended) na rangi nyingine.

Waafrika ndivyo tulivyo.
Halafu eti unajiita msoni na mchumi.. na haya ndio maneno yanayotoka kinywani mwa mchumi.. mimi ninachoweza kusema ni kwamba mimi sio nyani ila kama wewe na familia yako ni manyani basi sikukutalii kwa maana maana wewe mwenyewe ndio umeamua kujiita hivyo....tatizo lako wewe na wengi wenu humu hamna akili na hilo linajidhihirisha humu kutokana na maneno yenu, kwani binadamu yeyote yule mwenye akili hawezi kujishusha kiasi hicho na kujiita nyani kwa sababu tuu ya matatizo yanayomkabili.... kama kweli ungekuwa una akili ungeweza kuelewa na kufikiria kwamba nchi yetu ni masikini na ina matatizo ambayo yanaweza kutatulika, kama sisi ambao tupo nje ya serikali tunaweza kupambana na kuweza kuyatatua kwani kwani kutokana na mnavyokosoa humu mnaonekana matatizo mnayaona sasa ni kwanini hamuendi kupambana kuyatatua...
ngoja nitesti ubongo wako kidogo kama wewe ni mchumi kweli

f(x,y) = (2x(kipeo cha pili)y )+ cos yx
nitafutie
df/dxdy
 
habari Leo

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Masoko, Mary Nagu, amesema Tanzania itamtumia mtaalamu kutoka Japan kuhakikisha inaondokana na kutegemea jembe la mkono badala yake inakuwa nchi ya maendeleo ya viwanda.

Nagu aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuwa mtaalamu huyo kazi yake kubwa ni kuishauri serikali namna ya kuweza kuondokana na jembe la mkono badala yake nchi kuwa ya viwanda kama ilivyo kwa Japan.

Mtaalamu huyo, Yoshiyasu Mizuno ametokana na ziara aliyofanya Rais Jakaya Kikwete mwaka jana nchini Japan ambako pamoja na mambo mengine, aliiomba nchi hiyo iisaidie Tanzania ili nayo iweze kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya viwanda.

Japan imetoa mtaalamu wa mambo ya viwanda ambaye atafanya kazi na Serikali ya Tanzania asaidie katika kutoa ushauri wa namna ambavyo taifa hili masikini linaweza kupiga hatua ya maendeleo kwenye sekta ya viwanda. Nagu alisema kwa kuanzia, mtaalamu huyo atajikita zaidi katika kushughulika na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo kuinua sekta hiyo.

Alisema iwapo mazao yanayozalishwa nchini yakiuzwa nje yakiwa yamesindikwa na kuongezewa thamani, yataweza kuiletea nchi fedha nyingi za kigeni. “Lengo letu ni kuondokana na jembe la mkono tunataka kuwa nchi ya viwanda,” alisema Nagu wakati akizungumza baada ya mtaalamu huyo kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu.

Japan ni moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa katika maendeleo ya viwanda hali inayoelezwa na Nagu ni jukumu la mtaalamu huyo kutoa ushauri kwa serikali ili maendeleo ya namna hiyo yafikiwe nchini.

Alisema kama nchi ina jukumu la kufanya, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu pamoja na kuiunga mkono sekta ya kilimo ili viwanda vitakavyoanzishwa viweze kuwa na malighafi ya kutosha.

Naye Mizuno alisema Tanzania inaweza kubadilika kiuchumi iwapo itajikita katika kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda kwa kualika wawekezaji wa sekta binafsi kufanya kazi hiyo.

Alisema serikali pia ina jukumu la kuwekeza katika elimu kwa ajili ya manufaa ya baadaye ya watoto ambao watakuwa na akili za kuendeleza viwanda. Alisema jukumu lake akiwa nchini ni kutoa ushauri wa namna ya kupiga hatua ya kimaendeleo katika viwanda.

“Kazi hiyo nishaianza na nitaifanya kila siku kwa kipindi chote nitachokuwa hapa,” alisema Mizuno ambaye atafanya kazi na serikali akiwa kama Mshauri wa Mambo ya Maendeleo ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.

My Take:
Jamani kuna mtu anaweza kumuambia mama Nagu kuwa tuna CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE? Yaani kilichoshindwa kufanywa na LICHUO LIKUU LA NCHI, kitafanywa na MTAALAM MMOJA!!!?

MoD naomba uiunganishe na ile mada jingine, I couldn't resist the temptation to scream!
 
Hili ni jambo zuri sana tena sana. JK hongera kwa kuona mbali, waJapan wanajulikana dunia nzima kwa viwanda vyao ambavyo viko mbele sana kiteknologia, nakumbuka Mahathir Muhammad alifanya hivyo hivyo na leo tunaiona Malaysia kwa viwanda.

Ilimradi tuwasikilize maoni ya hao wataalam na tuyafatishe tusijidai kujuwa zaidi yao.

Anaetaka ushauri, akapewa na akaufatisha = Mtu kamili
Anaetaka ushauri, akapewa na asiufatishe = Mtu nusu
Asiyetaka ushauri, = hakuna mtu kabisaaaa.
 
Mtaalamu mmoja kwa nchi ya watu karibu million 40?
 
Back
Top Bottom