Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,510
Aisee, Nyani:
Yaani unataka nasi tukaanzie huko? Unajua iliwachukua miaka mingapi kufikia hapo walipo?
Sisi tuna faida ya ku-'leapfrog,' pamoja na kwamba nasi pia hatuwezi kukwepa 'process' itakayotupeleka katika maendeleo hayo (kwa muda mfupi kuliko waingereza); kwani hatuna haja tena ya kwenda kuvumbua gurudumu.
Pamoja na kwamba njia yetu itakuwa ni fupi, lakini hatuwezi kuyakwepa maandalizi mhimu yanayotakiwa kutupeleka kwenye hayo maendeleo. Ni haya maandalizi ndiyo yanayotusumbua sasa hivi.
Yaani kuwa na shule za kutosha na nzuri ili wataalam wawepo.
Pawe na miundombinu, barabara nzuri kupitisha pembejeo kwa mkulima.
Afya - watoto wasiishie kufa hata kabla ya kufikisha miaka mitano.
Viwanda mhimu - kuyaongezea mazao yetu thamani kabla ya kuyauza nje kwa bei nzuri.
Mifano ya wenzetu tumeiona: Korea ya Kusini, Malaysia, Indonesia, Turkey, Morocco, Tunisia - nchi zote hizi hawakuwa mbali sana na sisi kimaendeleo miaka michache iliyopita?
Mimi ninasema: Tunaweza, tuendelee vizuri na kuchapa kazi; mradi tu mafisadi wasiturudishe nyuma zaidi.
Nadhani umei-miss point yangu.....