Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Kwa kifupi, we have other priorities! Sisi bado tunaganga njaa na hivyo hilo unalolizungumzia halina nafasi kwetu. Badala ya kuwapeleka vijana wetu MIT ambako wale walio wakali watabaki huko ( MIT sio wajinga)na wale ambao watarudi tutashindwa kuwapa nyenzo, mishahara na mazingira ya kuwawezesha kufanya hizo R & D tuangalie kwanza basic needs zetu.
Turudi kwenye elimu ya msingi na sekondari, tuiboreshe ili watoto wetu wajifunze udadisi na sio kunukuu. Tupanue wigo la elimu hii nchi nzima ili kila mwenye nia ya kusoma apate nafasi hiyo. hawa ndio watakao'feed' vyuo vyetu vikuu na kuvifanya vitoe watu wenye calibre inayoendana na mahitaji ya dunia ya sasa. Hawa wakiwepo, mashirika binafsi yatawekeza kwenye R&D bila hata ya msaada wa serikali. India wamefanikiwa kutokana kuwa na idadi kubwa ya wasomi waliozalishwa na vyuo vyao vya IIT. Mashirika ya kigeni na yale ya kihindi yenye intenational presence ndiyo sasa yanavuna matunda hayo. Serikali ya kihindi ilishajaribu kubuni gari la gharama ndogo( mradi uliongozwa na mtoto mdogo wa marehemu Indira Gandhi, marehemu Sanjay Gandhi) waliloliita maruti na hawakufanikiwa mpaka waliponunua teknoloji kutoka Suzuki. Leo hii kampuni binafsi ya kihindi, Tata imefanikiwa kubuni gari la gharama ndogo duniani. Tusipoteze wakati kujaribu kuvumbua gurudumu kama tulivyofanya kwa miradi kama ya nyumbu bali tuwekeze kwenye kizazi cha kesho na bila shaka hizi R&D zitakuja. tatizo letu tunapenda sana njia za mkato. Hatuna subira.
Fundi Mchundo:
Naona mambo mengi hapa tulijadili katika mada ya Nuklia. Kwa mijadala ya siasa vitu vyote vinawezekana. Lakini miradi mingi ya kiserikali ni TEMBO MWEUPE (White Elephant).