Wezi wengine kwa watanzania-15556

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,401
7,307
Hii namba inaniibia fedha yangu katika acount ya simu ya Vodacom..sasa nimechoka voda wenyewe nahisi wanashiriki..nikiwapigia voda nawaeleza kuwa no.15556 inanitumia msg za Olimpiki wakati mi sijajiunga,kastama care wa voda wananiambia eti nimejiunga wakati misijajiunga,Voda huwa wananiambia niandike neno ONDOA kwenda no.15556..hii namba inanijibu 'SAMAHANI UJAJIUNGA NA HUDUMA HII'nikikaa siku mbili napata msg yao ya Olimpiki,na wanakata pesa yangu..sasa nimechoka naomba ushauri, kwanza nashangaa namba yangu nani kawapa wakati sijawahi jiunga na huduma za kilofa..
mimi ni memba wa JF chochote nachotaka kufahamu nakipata mfano michezo,siasa,mapenz,elimu,biashara nk.kwanini waniibie si bora nichangie JF
Angalizo
sijawahi jiunga na huduma 15556,ningejiunga ningesema na ningeomba kusaidiwa kujitoa
'Vox populi,Vox dei"
 
Kuna Jamaa alikuja na uzi m1 hv akasema anauza namba kwa mtu anayehitaji lengo ni kufanya biashara kwa mtindo huo!!
 
Jamani hii mitandao wanatajirika sana, ndio maana inabidi uwe unachagua, hata mm wameniambia nilipe 250/ mara 450/ nitapata huduma ya Internet kumbe ni uongo mtupu, ukishaliwa fedha wanakuambia ni kuanzia saa 6 usiku, ilipofika usiku nika- kaa hadi saa 7 usiku lakini wapi nikahamishia kwenye Modem lakini wapi.
Nashauri airtel (Zain ) ndio msemakweli utafanya kazi zako zote bila wasiwasi.
Ila kiboko ni BlackBerry ukushajaza utasurf na kuDownload bila tatizo sema haikubali mitandao mingine ya Kampuni za simu ukiweka Bundle zao
Nakushauri waombe no. ya kujifuta (Ondoa km ni 15050) au vinginevyo pole mkuu
 
Asante kaka
 
Tunaibiwa na makampuni ya simu hadi natamani kuacha kutumia simu. Pole mdau.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom