DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,212
- 4,515
Salaam kwa wote,
Mimi ninamiliki biashara ya car wash maeneo ya Mabibo kwenye barabara ya kuelekea Loyola opposite na Jambo Garden.
Nilikamilisha taratobu za kuomba huduma za Za umeme na kufanikiwa kulipa kiasi cha 1,175, 500/= kama gharama za kuunganishiwa umeme 06/02/2012. Mpaka leo, sijaletewa umeme zaidi ya nguzo waliouleta karibia miezi miwili iliyopita.
Leo mida ya saa tano na nusu nilipigiwa simu na kijana wangu akinitaarifu kwamba kuna watu kutoka Tanesco wamekuja kung'oa nguzo ikabidi niongee nao kwenye simu, jamaa wakaniambia kwamba wanalazimika kung'oa nguzo kwasababu watu wanalalamika eti serikali haikuwalipa fidia nilipomuuliza maswali mawili matatu nikaona anashindwa kunipa majibu yakuridhisha ikabidi niende kuongeanao ana kwa ana.
Nilishangaa kukuta gari aina ya Canter yenye namba T845 ASH inayomilikiwa na kampuni ya Sengerema Engeneering Group Ltd.
Tulibishana matokeo yake walishindwa kung'oa nguzo baada ya kuishiwa hoja ikabidi niende Tanesco Magomeni kufuatilia.
Nilichoambiwa ni kwamba hawa ni independent contractors wa Tanesco ila kuna wakati wanaiba vifaa kama hivyo kwa matumizi yao ya kampuni. Mapokeo ya Tanesco kwa kiasi yamenionyesha picha kwamba watumishi wa Tanesco wanalielewa hili ila ninashangaa hawachukui hatua stahiki kuondokana na watu kama hawa katka uchumi wetu.
Tunakokwenda mbali kweli. Ngoja tuone!