Single D
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 457
- 14
Nakubaliana na baadhi ya wachangiaji kwamba hawa watu washitakiwe kwa mujibu wa sheria na pia walipe riba maradufu.
Wasiwasi wangu ni kwamba,Tutathibitishaje kuwa hizo hela zimerudishwa??Inaweza tokea press conference wakaitwa waandishi wa habari,kwamba watuhumiwa wamerudisha pesa,waadishi wakapewa hilo tamko la katibu mkuu kiongozi,wakaandika basi ikaishia hapo?Kumbe ni maneno matupu tu ya kufunika kombe mwana haramu apite.
Ninaonyesha wasiwasi huo kwa sababu wananchi wamekuwa wanadanganywa na ahadi kemkem nyingi kuwa matatizo yao yatashughulikiwa na serikali lakini kumbe ni hewa kama Richmond.
Ninavyofahamu utawala huu ulianza kwa mbwembwe nyingi sana za kuleta maisha bora,lakini leo petrol TZ SH 1540 KWA LITA jijini Dar.Hayo mamilion 600??? ya ki america kama ni kweli,hizo si pesa chache inabidi yarudipo ionyeshwe kwa dhahiri yatatenda kitu gani.
Na serikali ya SISIEM wanavyoona tena 2010 inakaribia,watatumia hata mashushu kuzusha mitaani kuwa mambo yanaenda sawa kumbe wanaficha kitu.
Hizo hela warudishishapo mafisadi nasi tuzihisi huku mtaani kwamba kuna unafuu,au wale wazee wasitaafu wa iliyokuwa jumuia ya Afrika mashariki wasionekane tena mitaa ya hazina kuranda randa wakipigwa jua,walipwe mafao yao.
Walimu walipwe malimbikizo yao au wazielekeze hizo pesa ktk shughuli ambayo wananchi wataiona,La sivyo tutapewa maneno matamu ya MABILION YA JK KILA MKOA.KUMBE Kulikuwa na visenti,na wananchi wakadhalilika kutwa nzima NMB,CRDB N.K
SERIKALI IWE WAZI KWA WANANCHI WAKE KATIKA KILA HATUA INAYOCHUKUA KATIKA HILI