Wewe unakerwa na Gubu?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Aisee! Mimi hii kitu inanikera sana. Hivi ni kwa nini watu wanakuwa na GUBU. Ni jambo la kuzaliwa nalo au wanajiendekeza tu? Mtu ukimfanyia kosa ataseeema jambo hilo hilo usiku na mchana mpaka kichefuchefu kikupate. Sasa akufanyie yeye wema atataka kila mtu ajue na wewe kila ukikutana naye umshukuru kwa wema aliokutendea.

Hivi na wewe unakerwa na GUBU kama ninavyokereka mimi?
 
Nadhani hiyo ni tabia ya mtu na mara nyingi huwa inarithiwa. Mfano mama yangu ni mtu ambaye anasema sana pale unapomkosea na hasa akiwa amekasirika. Yaani akikasirika atasema na kuzunguka nyumba nzima mpaka hasira zake ziishe. Kukweli hiyo tabia inanikera sana na ndio maana mara nyingi nikiona mama anaanza kusema sema sana, namwambia yaishe pale pale iliasiendelee kuongea.
 
linanikera hata mie, mbaya zaidi kosa haliishi hata ipite miaka ipo siku litakumbushiwa.......
 
nilidhani dubu, kumbe gubu!!
Hilo silijui
.

Ndiyo hilo hilo Kongosho!! Mtu unamuuliza "leo tutakwenda Movie?" yeye anakujibu "sijui", kisa jana uliangalia taarifa ya habari wakati yeye alikuwa anataka kuangalia tamthiliya!!
 
Honestly kigarama wanaume wana gubu mbaya mno! anarudia rudia hivyo na wakati mwingine atanyamaza ukidhani yameisha kumbe anavuta pumzi huh!
Precious hao ni wachache ni kama hawapo, sema bahati mbaya katika hao wachache waliopo mmoja wao ndiyo akuangukie awe mumeo!!
 
Precious hao ni wachache ni kama hawapo, sema bahati mbaya katika hao wachache waliopo mmoja wao ndiyo akuangukie awe mumeo!!

si wachache kama unavyodhani na kimsingi hatuwezi kujua statistic yao ila kama ilivyo kwa wanawake hiyo personality iko kwa wanaume pia.Thank God my hubby hayuko na hii kitu!
 
Back
Top Bottom