Wewe ni nani? Swali gumu sana

Ukiweza kulijibu hilo swali maisha yako yatabadilika sana utajifaham ww ni nani, unatakiwa uweje, uvae nn, uishi vipi , hutoiga iga vitu wala kuona mtu mwingine amepewa na ww huna nk
 
kati ya maswali ninayoyachukia ni hili...
utakuta uko mahali umetulia na majamaa wenzako mara anatokea mtu ambaye anafahamiana na jamaa zako lakini wewe hakufahamu..., sasa badala ya kutumia busara tu kuuliza kwa namna ya kistaarabu yeye anawauliza wale wenzako "eti huyu ni nani..?"
 
Mimi ni mtanzania jinga nayeshabikia ccm halafu maisha yamenibana balaa na masikini.
 
Wewe ni nani?

Ni swali ambalo ukiulizwa unaweza kuliona rahisi sana na kulijibu haraka haraka kwa kutoa jibu linalotaja jina lako. Mimi ni James, ama nimi ni Janeth. Lakini ni ukweli ulio wazi kua wewe si jina lako. Wewe ni zaidi ya jina lako.

Ama unaweza kujibu kwa kutaja kazi yako, wewe ni nani? Ukajibu, mimi ni Mkurugenzi wa Masoko wa CRDB, mwingine atasema mimi ni Mbunge au mimi ni Waziri, ama mimi ni Mwalimu. Lakini ukweli ni kwamba wewe si kazi yako, wewe si cheo chako. Wewe ni zaidi ya kazi yako. Na kazi yako sio wewe.

MIMI NI NANI?
Naweza kujibu hivi.
Mimi ni mimi duniani kote, nipo mimi mwenye mawazo ya aina yangu, hakuna mwingine kama mimi, Nikifa. Akizaliwa mwingine akapewa jina langu, atakua mwingine mwenye jina langu. Mimi hana mbadala ila kuna mwingine atakayefanya niliyofanya. Mimi hawezi kua ndani ya mwingine popote, kabla yangu na baada yangu.

Je! Wewe ni Nani?
Mimi ni mimi duniani kote, mimi mwenye mawazo ya aina yangu, hakuna mwingine kama mimi, mimi ni mimi nilievaa mwili na siku mwili wangu ukichoka nitatoka na kwenda zangu, na siku nikipenda nitarudi mimi ni mimi wa ndani yangu.
 
Back
Top Bottom