WEWE MWANA JF ANGALIA JINA LAKO HAPA. Je Limo?

JINA LAKO LIPO HUMU?
Haya ndo baadhi ya majina ya wafanyakazi wenye mishahara ya kima cha chini Waliouziwa viwanja TMK na kuwaacha walala hoi wakilia na kuishia kutozwa Tsh 30,000 /= Bure

1. Wilson Mukama
2. Job Ndugai
3. Prof. Makame Mnyaa
4. Pereira Ame Silima
5. Dr. Florence Turuka
6. RAmadhani Kijjah
7. Omari Chambo
8. Dr. Idrisa Rashid
9. Dr. Didas Masaburi
10. Jerry Slaa
11. Paul Chagonja
12. Suleiman Kova
13. Haruna Masebu
14. Ludovick Uttoh
15. Marina Njelekela
16. Augustino Mrema.
17. Deo Filikunjombe
18. Sylivester Koka
19. Idd Azan
20. Cyril Chami
21. Mohamed Misanga
22. David Kafulila
23. Dr. Peter Kafumu
24. Selemani Zedi
25. Maulid Komu
26. Suzan Lyimo.
27. Dr. Marry Mwenjelwa
28. Zakhia Megji
30. Miraji Kikwete
31. Khalifani Kikwete
32. Junita Mramba
33. Suzan Mkapa
34. Zainab Mkomwa
35. George Rupia
36. Maimuna Mfutakamba
37. Mary Membe
38. Pharles Njelela
39. Judith Kahama
40. Wilfredy Mwanry

Mbona simo
 
naona miraji katia saini badala ya Riz-1... big up , wazee wa misitu ya pande
 
kama wameomba na kupewa kihalali bila kupendelewa sioni shida kwa hili
ila kama wametumia vyeo vyao kulazimisha kupewa ndio itakuwa shida.

pia shida ipo kwa kuwaita walala hoi na wenye kipato cha chini, je kipato chao ndicho MTz wa hali ya chini? Kweli Tz ni zaidi ya tuijuavyo
 
Hata sehemu moja ilinikuliwa kwamba Mwenye nacho ataongezewa, asiye nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho.
Yesu alikuja ili tuwe na uzima, kisha tuwe nao tele.
 
Waiter: ze kiki ya baridiiii tafadhari .... Uwiiiii kigumu cha cha mapinduzi hahaha
 
Kwa hali hiyo, rushwa ni mwiko kuisha!! tutaendelea kutoa na kupokea rushwa kwa vitu kama hivi ambavyo ni haki ya kila mmoja lakinikwa style hii ni upuuzi.
 
JINA LAKO LIPO HUMU?
Haya ndo baadhi ya majina ya wafanyakazi wenye mishahara ya kima cha chini Waliouziwa viwanja TMK na kuwaacha walala hoi wakilia na kuishia kutozwa Tsh 30,000 /= Bure

1. Wilson Mukama
2. Job Ndugai
3. Prof. Makame Mnyaa
4. Pereira Ame Silima
5. Dr. Florence Turuka
6. RAmadhani Kijjah
7. Omari Chambo
8. Dr. Idrisa Rashid
9. Dr. Didas Masaburi
10. Jerry Slaa
11. Paul Chagonja
12. Suleiman Kova
13. Haruna Masebu
14. Ludovick Uttoh
15. Marina Njelekela
16. Augustino Mrema.
17. Deo Filikunjombe
18. Sylivester Koka
19. Idd Azan
20. Cyril Chami
21. Mohamed Misanga
22. David Kafulila
23. Dr. Peter Kafumu
24. Selemani Zedi
25. Maulid Komu
26. Suzan Lyimo.
27. Dr. Marry Mwenjelwa
28. Zakhia Megji
30. Miraji Kikwete
31. Khalifani Kikwete
32. Junita Mramba
33. Suzan Mkapa
34. Zainab Mkomwa
35. George Rupia
36. Maimuna Mfutakamba
37. Mary Membe
38. Pharles Njelela
39. Judith Kahama
40. Wilfredy Mwanry

Walalahoi kumbuka sie ni "proffessional squarters" cha msingi hawa wateule wasituingilie huku kitaaa?
 
Nasema kuna siku nitafanya maandamano peke yangu mtanikuta huko nikiwa naelekea popote potelea mbali, I am tired of what is done in this nation. They always say that we are poor but they grabbing every thing. I will do whatever i can you will find me there. God bless You.
 
tukafyeke mapori tupate viwanja,mwenye macho haambiwi tazama!Mbona tulishafundishwa na baba kuwa AKILI ZA KUAMBIWA UCHANGANYE NA ZAKO,twendeni msituni,kule kuna viwanja tele!
 
CCM OYEEEEEEEEEEEEEEE! KIDUMU CHAMAAAAAAAAAA:fear:
 

Attachments

  • CCM & Chadema.jpg
    CCM & Chadema.jpg
    51.1 KB · Views: 67
JINA LAKO LIPO HUMU?
Haya ndo baadhi ya majina ya wafanyakazi wenye mishahara ya kima cha chini Waliouziwa viwanja TMK na kuwaacha walala hoi wakilia na kuishia kutozwa Tsh 30,000 /= Bure

1. Wilson Mukama
2. Job Ndugai
3. Prof. Makame Mnyaa
4. Pereira Ame Silima
5. Dr. Florence Turuka
6. RAmadhani Kijjah
7. Omari Chambo
8. Dr. Idrisa Rashid
9. Dr. Didas Masaburi
10. Jerry Slaa
11. Paul Chagonja
12. Suleiman Kova
13. Haruna Masebu
14. Ludovick Uttoh
15. Marina Njelekela
16. Augustino Mrema.
17. Deo Filikunjombe
18. Sylivester Koka
19. Idd Azan
20. Cyril Chami
21. Mohamed Misanga
22. David Kafulila
23. Dr. Peter Kafumu
24. Selemani Zedi
25. Maulid Komu
26. Suzan Lyimo.
27. Dr. Marry Mwenjelwa
28. Zakhia Megji
30. Miraji Kikwete
31. Khalifani Kikwete
32. Junita Mramba
33. Suzan Mkapa
34. Zainab Mkomwa
35. George Rupia
36. Maimuna Mfutakamba
37. Mary Membe
38. Pharles Njelela
39. Judith Kahama
40. Wilfredy Mwanry
Aisee hawa wakubwa mbona imeshakuwa hatari.
Vigogo wagawiwa viwanja Dar Send to a friend
Wednesday, 25 July 2012 21:03
0digg

mukama-top2.jpg
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama

WALALA HOI WALALAMIKA, WALITOA SH30,000 ZA MAOMBI ‘ZIMEENDA NA MAJI’
Patricia Kimelemeta
MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.

Majina hayo ambayo gazeti hili iliyaona jana, yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo wa manispaa hiyo, ili wananchi walioomba viwanja hivyo waweze kuangalia kama wamo katika orodha ya waliopatiwa viwanja hivyo.

Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.

Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

Mkurugenzi apatwa kigugumizi
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.

“Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo,” alisema Nyalile.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.

Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wananchi walalama

Baadhi ya wananchi walikuwa wakiangalia majina hayo katika ubao huo walidai kuwa, baadhi ya maofisa wa halmashauri hiyo wamedaiwa kupewa rushwa wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo.

“Walitangaza kama kiini macho, lakini tayari walikuwa na majina yao ili waweze kuwapatia na jambo ambalo limejionyesha wazi kwenye majina ya watu waliopewa viwanja hivyo,” alisema mwananchi mmoja (jina tunalihifadhi) na kuongeza:

“Kutokana na hali hii, hatuna imani na viongozi wowote wa Serikali kwa sababu inaonyesha wazi kuwa, kila mmoja anaangalia masilahi yake na si wananchi wasio na kipato”.

Aliongeza kuwa, wananchi hawana imani na viongozi wao, hivyo Serikali inapaswa kuingilia kati kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha matatizo.

Mwananchi mwingine aliyekuwa akifuatilia jina lake alisema: “Wewe unachokiona ni nini hapo kama siyo yaleyale ya ubinafsi! Wewe unaamini kabisa kwamba kweli hawa viongozi wetu hawana nyumba au hawana viwanja hapa Dar es Salaam.

Aliongeza: ”Kama manispaa walitangaza viwanja ili wajiuzie wangesema tu badala ya kuchukua fedha zetu Sh30,000 halafu viwanja wakajigawia wenyewe.”

Mgawo wa Viwanja

Mapema mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza kwamba imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji Viwanja.

Fomu za maombi ya kununua viwanja hivyo zilianza kutolewa Juni 11 na kila mwombaji alipaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha Sh30,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

“Fedha hizo hazitarejeshwa na mwombaji atajaza nakala mbili za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana,” linasomeka tangazo rasmi la manispaa hiyo.

Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la mradi ambao walikuwa wametambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, pia walitakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule.
 
JINA LAKO LIPO HUMU?
Haya ndo baadhi ya majina ya wafanyakazi wenye mishahara ya kima cha chini Waliouziwa viwanja TMK na kuwaacha walala hoi wakilia na kuishia kutozwa Tsh 30,000 /= Bure

1. Wilson Mukama
2. Job Ndugai
3. Prof. Makame Mnyaa
4. Pereira Ame Silima
5. Dr. Florence Turuka
6. RAmadhani Kijjah
7. Omari Chambo
8. Dr. Idrisa Rashid
9. Dr. Didas Masaburi
10. Jerry Slaa
11. Paul Chagonja
12. Suleiman Kova
13. Haruna Masebu
14. Ludovick Uttoh
15. Marina Njelekela
16. Augustino Mrema.
17. Deo Filikunjombe
18. Sylivester Koka
19. Idd Azan
20. Cyril Chami
21. Mohamed Misanga
22. David Kafulila
23. Dr. Peter Kafumu
24. Selemani Zedi
25. Maulid Komu
26. Suzan Lyimo.
27. Dr. Marry Mwenjelwa
28. Zakhia Megji
30. Miraji Kikwete
31. Khalifani Kikwete
32. Junita Mramba
33. Suzan Mkapa
34. Zainab Mkomwa
35. George Rupia
36. Maimuna Mfutakamba
37. Mary Membe
38. Pharles Njelela
39. Judith Kahama
40. Wilfredy Mwanry

Nimeliona jina langu!!
 
nimeisikia hii kwenye uchambizi wa magazeti... amakweli mtaji wa maskini nguvu za mafisadi kha!

BornTown, unasemaje eti?? ngoja nivae miwani ni kama vile macho hayaoni vizuri....

BACK TO THE TOPIC
Hii ndio Tz... ni zaidi ya uijuavyo. Hili linanikumbusha historia ya sinza na chanzo cha kuitwa sinza kwa wajanja...pengine wanataka kutengeneza tena kwa wajanja huko au wenyenazo street...
 
unajua nimegundua watanzania tunapenda kudandia treni kwa mbele. viwanja vipo 1, 800 vigogo wamepewa 40. kwa hesabu za haraka hiyo ni 3%, viwa nja 1760, 97% vimeenda kwa hao makabwela. halafu kafulila nae kigogo, kapata ubunge 2010, kabla ya hapo nae alikuwa mlalahoi. toa ubunge wake nae ni mtanzania anahitaji kiwanja ajenge, ubunge nao ni kazi lazima ajiendeleze. hili gazeti la mwananchi nilikuwa naliamini kwa habari za ukweli lakini mwaka huu nina wasiwasi nao kuna tatizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom