Netanyahu
Senior Member
- Oct 2, 2008
- 147
- 22
Ukitaka kutuma pesa nchi nyingine kupitia western union Tanzania imekuwa vigumu mno.Wanataka uwe na passport sijui na viza za huyo unayemtumia na vikolokolo vingine kutegemea wanavyojua wenyewe na unapeleka wapi.Hawajali hata unatuma kiasi gani.Hata kama ni dola 10 au 20 utadaiwa vikolokolo kibao.Hivi dola 10 ,20 au 100 hivi nayo inaangukia kwenye kundi la Money laundering au Capital flight? Na hiyo ni kwa Tanzania tu?
Matokeo yake kwa taarifa za mitaani nilizonazo watu wanasafiri na mabasi kwenda Kenya,Zambia au Uganda na kuzituma pesa kupitia Ofisi za Western Union za nchi hizo ambako hakuna ujinga kama huo wa ofisi za western union za Tanzania.Matokeo yake ofisi za western union za nchi hizo zinaneemeka kwa commission nzuri na kuziacha za Tanzania ziko hoi.Je Western Union offices za Tanzania zinahujumiwa au ni kitu gani?