Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Werema kumpinga Pinda ni utovu wa nidhamu Tuesday, 28 December 2010 20:32
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
Mpasuko uliomo katika Serikali ya Rais Kikwete juzi ulidhihirika wazi wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema aliposema kuwa hakuna uwezekano wa kuwa na katiba mpya, isipokuwa katiba iliyopo itafanyiwa marekebisho katika baadhi ya vipengele. Kauli hiyo aliitoa Ikulu, Dar es Salaam juzi, mara baada ya Rais Kikwete kumwapisha Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa suala la kubadilisha ibara zinazoonekana kutokidhi haja na kuingiza mambo mapya kwenye katiba linakubalika, lakini suala la kuandika katiba mpya hapana. Alisema kinachohitajika sasa hivi ni kupata michango mingi ya mawazo ya wananchi kuliko kupoteza muda kwa kile alichokiita kuzungumza kama bata kila kukicha.
Jaji Werema alitaka kujua upya wa katiba unaotakiwa ni upi, na kuongeza kuwa sio sahihi kusema Watanzania wanataka katiba mpya wakati kauli za madai hayo zinatoka Dar es Salaam tu. Alisema sio lazima kila mtu anachokisema kifuatwe na akatoa mfano kuwa kule anakotoka, wafugaji watataka mambo ya ngombe yaingizwe kwenye katiba na Wahaya nao wanaweza kusema ndizi nazo ziingizwe kwenye katiba.
Huo ndio msimamo na mtazamo wa mtu mwenye dhima na wajibu wa kuishauri Serikali kuhusu masuala ya sheria na katiba ambaye haoni umuhimu wa kuwapo katiba mpya katika wakati na mazingira tuliomo hivi sasa. Ni msimamo wa mtu aliyelewa madaraka na asiyejua mipaka ya madaraka yake wala uzito wa kauli yake pale anaposema waziwazi kwamba suala la katiba mpya hapana, lakini kuiweka viraka ile iliyopo ni ruksa. Ni kauli nzito, ya kitemi na kidikteta ambayo hata Rais Kikwete ambaye ni kiongozi wa nchi hawezi kuitoa katika mazingira yaliyopo hivi sasa hata kama naye angekuwa na msimamo kama wa mteule wake huyo.
Ni msimamo hasi unaotolewa baada ya bosi wake, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa msimamo tofauti Desemba 7, 2010 alipowaambia wahariri wa vyombo vya habari kuwa alikuwa haoni tatizo lolote katika kukaa na kuliangalia suala la kuwapo katiba mpya katika nchi yetu na akaongeza kuwa angemshauri Rais ili uwekwe utaratibu wa kuliangalia suala hilo. Alisema kuwa anadhani njia bora ni kuhusisha watu wengi kadri inavyowezekana, na ikibidi suala hilo lipelekwe kwa wananchi.
Kauli ya Waziri Mkuu Pinda imejaa busara na unyenyekevu anaposema atamshauri Rais. Somo analowapa viongozi wa Serikali, akiwamo Jaji Werema, ni kuwa yeye hana kauli ya mwisho na anatambua kuwa juu yake iko mamlaka kubwa zaidi ambayo ni Rais Kikwete. Hivyo, Jaji Werema anapokurupuka na kutangaza kuwa katiba mpya hapana anakuwa ni mtovu wa nidhamu, kwa sababu ameitoa wakati bosi wake tayari ametoa msimamo tofauti na bahati mbaya Rais Kikwete hajatoa msimamo wowote kuhusu suala hilo.
Ni utovu wa nidhamu uliopindukia, hasa tukitilia maanani kwamba tayari viongozi kadhaa wa nchi, wakiwamo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani nao wameshauri iandaliwe katiba mpya. Kwa vigezo vyovyote vile, Jaji Werema kwa elimu na uzoefu wake wa uongozi ni mithili ya kichuguu mbele ya viongozi hao ambao wako juu kama Mlima Kilimanjaro.
Inatia simanzi kuona pia kuwa hata baada ya viongozi wa kidini, vyama vya siasa, wanaharakati, vyama vya wafanyakazi , Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na wananchi kwa ujumla kutaka katiba mpya, bado anajitokeza mtu na kutoa kauli zenye kuchochea hasira za wananchi ambao wanadai katiba mpya ambayo italinda umoja na mshikamano wetu na kutuepusha na uwezekano wa kutokea machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika siku za usoni. Sisi tunasema Jaji Werema ni mtovu wa nidhamu, awajibishwe.