wenzetu wakenya wanatuacha hao.

KUNANI PALE TGA

Senior Member
Feb 6, 2009
138
7
Hizo ni baadhi ya za flyovers and road expansion to 8 and 12 lanes taking shape.leave everything aside,frankly speaking these people are moving,without minerals,without oil,without gas,they deserve a pet on the shoulder.
 

Attachments

  • 4218883359_56420cfb8a_b.jpg
    4218883359_56420cfb8a_b.jpg
    78.1 KB · Views: 188
  • 4890671137_d15094c291_b.jpg
    4890671137_d15094c291_b.jpg
    75.2 KB · Views: 168
  • 4918762585_b940008e75_b.jpg
    4918762585_b940008e75_b.jpg
    44.2 KB · Views: 156
  • 4274177594_cb1f097408_b.jpg
    4274177594_cb1f097408_b.jpg
    74.3 KB · Views: 157
Hatariii!!! Hivi ndani ya CCM huwa hakuna hata mtu mmoja tu mwenye wivu wa maendeleo??? Laaaannnnaaa tupu!!!!!
 
Wivu wa maendeleo toka CCM? Duuu! labda wivu wa kuchakachua akili za watz
 
Watuache mara ngapi? Wako serious hususani viongozi, sisi kiongozi gani yuko serious kuanzia na JK?
 
aise lakini inauma sana,sisi maisha yetu haya na thamani kabisa,yani tumekuja duniani kama kuteseka vile.yaani kweli mtu hupendi kupendezesha nyumba yako?yaani serikali kama vile haipendi nchi yake.
 
hata wao walitoboana macho sana miaka ya mwisho ya utawala wa KANU. Walipoweza kuibomoa KANU ndipo wakaanza kufanya haya tunayoyaona. CCM ndiyo tatizo kuu hapa nchini.
 
na hii construction ilianza 2009,yaani hakuna kucheza na kazi.by end of 2011 kazi itaisha na wana nairobi wata weza kufaidi pesa zao za kodi.sisi tuliambiwa sijui happa dar zitaanza kujengwa mwaka huu,ni kweli?au ilikuwa changamsha baraza,na zile train za mjini?we are simply stupid and we dont love ourselves and our country,period.
 
Mbona daraja la kigamboni lishajengwa kwenye documents na inawezekana kabisa tushalipia
 
wAKUU MIMI NAFIKIRI SISI TUNA LAHANA NDIYO MAANA HAKUNA KINACHOENDELEA!!
 
Hivi kumbe mema ya Wananchi kujiandikia KATIBA MPYA katika nchi ndio mambo hubadilika mara moja na inakua hivi kama ambavyo tunavyoona nchi jirani ya Kenya??

Jamani ni kama baba masikini (Kenya) kununulia watoto wake wote barabara za angani, viwanja vya ndege kama vya Ulaya, chanzo cha umeme wa uhakika na bei nafuu kama ya Urusi.

Halafu wewe mwenye baba tajiri wa kila kitu (Tanzania) ndio kwanza mnalala chini ya mti, ufisadi kila kona na watu kuwaza tu dili maofisini hakuna kufanya kazi, Uranium yako kuendeleza Iran, Vijana nguvu kazi kupelekwa kwenye ugaidi kwa ajili ya dini tu, basi tuuuu, taabu tuuuu!!!

Mungu tusaidie, CCM mnaodoka lini na sisi tuweke viongozi waadilifu tukapate na sisi maendeleo kutokana na rasilmali tele tulizojaliwa?

Yaani hadi wakati mwingine unaobora kuzamisha kizazi kizima cha viongozi wa CCM.
 
Hatariii!!! Hivi ndani ya CCM huwa hakuna hata mtu mmoja tu mwenye wivu wa maendeleo??? Laaaannnnaaa tupu!!!!!

Wana wivu sana huoni jinsi wanavojilimbikizia mali wao wenyewe kwa wenyewe! Mijengo yao maasaki, msasani na sasa wanamiliki estates maeneo ya kibaha, mlandizi, bagamoyo mbezi juu, makongo juu ukiacha wa mikoani...................!
 
aisee.:dizzy::whoo: kweli tanzania tuko nyuma sana kimaendeleo,yes we need changes: :nod:YES WE CAN IF WE WILL HAVE ONE VOICE: :sad::clap2:

CHANGES
 
Hatariii!!! Hivi ndani ya CCM huwa hakuna hata mtu mmoja tu mwenye wivu wa maendeleo??? Laaaannnnaaa tupu!!!!!

Wivu wanao, waangalie akina Rostam na Lowasa waliona akina Mramba na Yona wamekula mashavu nao wakajitengenezea kadili kao ka kunyonya kwa kupitia kampuni hewa ya Richmond........
 
raha nyingine ya Nairobi.Planners wa mji walifikiri mbele tangu miaka hiyo sio dar yaani ni nyumba baada ya nyumba.hakuna sehemu hata ya kutengenezea park ,michezo ya watoto bandika nyumba bandua nyumba,hakuna room ya future expansion kuondoa barabara mbili tu.Kenya wakitengeza kitongoji wanapima viwanja,wanaweka miundo mbinu halafu ndo wanagawa viwanja.anayebisha aende Thika,Kasarani,Kikuyu ataona jamaa walivyo vizuri ..kwetu ni uzuzu tu
 
Inauma sana kuona wenzetu wakipiga hatua kubwa wakati sisi bado tumelala,lakini haya yote ni kutokana na kuwa na serikali yenye mawazo mgando kwa muda mrefu,serikali isiyosikia wala kujali maendeleo ya wananchi wake.
Nasi wananchi tunapaswa kupewa lawama kwa kukubali kuiweka madarakani serikali hii kwa muda mrefu kwani hakuna kinachofanyika,kofia,khanga na mat shirt vinatugharimu.
 
Jamaa wana move tatizo wa TZ tupo blind sana!nadhani haya ni maeneo ya Mombasa Road!
 
Kwa Tanzania, inabidi kwanza kujenga RINGS kuzunguka Dar. Kama ilivyo Mandela Roads ukiunganisha na Sam Nujoma, basi inabidi zijengwe barabara nyingine kupita karibu na uwanja wa ndege na ianzie baharini hadi baharini ikiwa na maana Mbezi beach hadi Kigamboni. Nyingine ipite mitaa ya Mbezi ila nayo pia ianzie baharini hadi baharini.

Mkimaliza hizi, ndiyo mje kwenye Fly-over.

Mzizi wa fitina kwa Dar unaanzia na mifano kama "Mtu yuko Tegeta, anakuja hadi Mwenge ili baadaye aende uwanja wa ndege."
 
Back
Top Bottom