Wenzangu mnafanya nini mpaka nakubaliana kufunga ndoa na wapenzi wenu?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
anahitajiushauri
"Ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32, ninafanya kazi hapa Dar es Salaam. sasa tatizo lililonileta hapa leo ni kwamba ningependa sana kuolewa na ninaomba Mungu anipe Mume mwema. Nimekuwa na mahusiano mazuri tu na wanaume lakini inapofikia wakati ukigusia masuala ya ndoa inakuwa sumu.Yaani tunakorofishana mpaka kufikia hatua ya kutishia kuwachana.

Kwa sasa nina mwanaume na tumekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka mmoja sasa, lakini nikimueleza masuala ya ndoa ndio inakuwa ugomvi na anaona kama vile namghasi nainafikia hatua tunakorofishana kabisa.

Zake ni kunipiga danadana tu nakuniambia nimpe muda, mimi umri unaenda si unajua tena mwanamke? Yaani hanishirikishi kwenye mipango yake hivyo nashindwa kuelewa. Nikiuliza Muda upi unahitaji? na kwanini tusishirikiane kimawazo?

Nafikiria kuachana nae lakini najiuliza nitaachana na wangapi? Yaani ninapata wakati mgumu sana na ninashindwa kuelewa, je inakuaje mwanamke anaweza kukubaliana na mwenzie vizuri hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa?

Au labda mimi napata wanaume ambao hawako tayari kuwa ndani ya ndoa? Naomba mnishauri nifanye nini ili niweze kujua kama ana nia ya kweli au ndio nimechemsha tena!"

USHAURI
 
dada kama wewe ni mkristu nenda kwenye maombi, utaombewa na njia itafunguliwa utapata mume mwema.
 
Unaingia bila kuchunguza kuwa na subira usiingie kichwa kichwa wala usikubali kuingia kwenye mahusiano haraka haraka. Vijana wengi wa kiume na hata wa kike hawapendi kuoa au kuolewa wanapenda kula good time tu. chunguza ninaimani utampata wa ubavu wako.
 
anahitajiushauri
"Ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32, ninafanya kazi hapa Dar es Salaam. sasa tatizo lililonileta hapa leo ni kwamba ningependa sana kuolewa na ninaomba Mungu anipe Mume mwema. Nimekuwa na mahusiano mazuri tu na wanaume lakini inapofikia wakati ukigusia masuala ya ndoa inakuwa sumu.Yaani tunakorofishana mpaka kufikia hatua ya kutishia kuwachana.

Kwa sasa nina mwanaume na tumekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka mmoja sasa, lakini nikimueleza masuala ya ndoa ndio inakuwa ugomvi na anaona kama vile namghasi nainafikia hatua tunakorofishana kabisa.

Zake ni kunipiga danadana tu nakuniambia nimpe muda, mimi umri unaenda si unajua tena mwanamke? Yaani hanishirikishi kwenye mipango yake hivyo nashindwa kuelewa. Nikiuliza Muda upi unahitaji? na kwanini tusishirikiane kimawazo?

Nafikiria kuachana nae lakini najiuliza nitaachana na wangapi? Yaani ninapata wakati mgumu sana na ninashindwa kuelewa, je inakuaje mwanamke anaweza kukubaliana na mwenzie vizuri hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa?

Au labda mimi napata wanaume ambao hawako tayari kuwa ndani ya ndoa? Naomba mnishauri nifanye nini ili niweze kujua kama ana nia ya kweli au ndio nimechemsha tena!"

USHAURI

Upo tayari Kuwa Mke Mwema au wewe unataka tu Mume Mwema?
Labda huyo BF hajaona kama unastahili kuwa mama wa wanae, kwa mda ulokae naye anaona wewe hutakuwa mke Mwema.

Ndoa ni maisha, kufanya maamzi ya kuingia kwenye Ndoa yanahitaji multiple analysis, Best,more likely na Worse Scenarios, na mumeo mtalajiwa anatakiwa kuyaangalia hayo yote kama ataweza kuya accommodate yakitokea, hasa pale matalajiyo yatakuwa si kama yale aliyotarajia. Anakusoma kwanza Usije kuwa umeficha makucha, chapo hata baadaye binadamu anaweza kubadilika tabia.

Anafikilia huko nyuma files zako zikoje maana the past predicts the future (Trend analysis) japo inaweza kuwa na variations. Kama mulishasimuliana files zenu zako zikamshituwa.

Omba sana, maana Mungu anampa mtu kile kinachomstahili, Huwezi kuomba mume mwema wakati wewe si mke mwema.

Endelea kuomba, Nichunguze ni kipi kilikuwa tatizo kwenye relations za mwanzo na ulikirekrbisha vipi, ni muhimu dada.

Mke/Mume Mwema anatoka kwa Bwana, na wale wamchao Bwana ndo anawapa kile kinachowafanana. Endelea kuomba Utapewa dada.

U
 
Ndoa itakuja tu..vuta subira.
Ukichunguza kwa makini sana utaona kuwa kuna rika kwa mwanamke ambapo kuombwa ndoa na mwanaume kunakuja kirahisi zaidi - hii ni miaka kuanzia 20-25 ( nimesema na narudia tena mara nyingi siyo mara zote) - umri huu msichana hupata wachumba/waume kwa urahisi sana. Ukishavuka 30 chances hupungua lakini haina maana kuwa hawapati wachumba.
 
Vuta subira kama Mungu amekupangia huyo mwanaume kuwa mume wako wa ndoa basi itakuwa hivyo kama hajakupangia basi atatokea mwingine pia i guess sababu unaona miaka inazidi kusogea ndio maana unazidi kuwa so desperate just be patient na uzidi kumuomba mungu akuonyeshe njia ya kukupa mume bora na sio baora mume. Ila unabidi na wewe ujiulize swali je uko tayari? Hicho ndio kitu cha msingi linapokuja suala la ndoa ni vyema wote kukubaliana kabla ya kusonga mbele ningeshauri umuulize huyo BF wako tatizo ni nini je hayuko tayari? Sio awe anakupiga tu danadana bila kuwa na sababu ya msingi.
 
Ndoa itakuja tu..vuta subira.
Ukichunguza kwa makini sana utaona kuwa kuna rika kwa mwanamke ambapo kuombwa ndoa na mwanaume kunakuja kirahisi zaidi - hii ni miaka kuanzia 20-25 ( nimesema na narudia tena mara nyingi siyo mara zote) - umri huu msichana hupata wachumba/waume kwa urahisi sana. Ukishavuka 30 chances hupungua lakini haina maana kuwa hawapati wachumba.

Age hiyo wakiishapata mwanaume huwa wanakuwa so desperate kuolewa I guess ni kwasababu huwa sijui wanaona kama vile umri umeenda
 
Pole sana mpendwa, Hakika umepata ufumbuzi pindi tu ulipotoa siri yako rohoni na kuiweka hapa.Naomba sana jaribu kunitumia private message kisha nitakupa namba yangu ya simu uweze kupata msaada wa uhakika kabisa.Hilo nakuhakikishia asilimia mia moja umepata jibu lililo kamili.
 
Tatizo lako unaendekeza uasherati. Mwanamme akikuijia huwa hakwambii anataka kukuoa. Mnapoanza kushiriki tendo la ndoa wewe unadhani anampango wa kukuoa??!!!!!!! Anakutamani tu ndo maana umefika hapo ulipo. Nakushauri uachane kabisa na uasherati (dont tell me haiwezekani!!!). Ukitulia Mungu atakuletea mme kwa wakati wake. Na huyu mme haakuja kwa nia ya kufanya uasherati.
 
Wadada wengi hawafanikiwa kupata ndoa kwasababu wanaweka vigezo vingi vikubwa kwa mwanamume wa kumuoa.Wasichana wengi wakifikisha umri wa miaka 18 mpaka 26 wanakuwa na mvuto wa ajabu kipindi hicho chance za kuolewa zinakwa nje nje badala ya kutumia nafasi hizo bila ajizi wanaanza kuweka vigezo vya ajabu ajabu mara utasikia nataka mume mwenye gari na nyumba nzuri,wengine nataka mume mrefu,wengine nataka mume kabila na dini yangu,wengine nataka mume kama wa fulani !,wengine nataka mume mwenye &%** kubwa,wengine nataka mume kutoka familia nzuri na nk.

Kipindi cha wanawake wengi kuvutia ni kifupi sana wakati wakiendelea kusubiri chaguzi zao ziwadondokee muda nao unakimbia wakija kushtuka wameshagonga miaka 30 au zaidi chance zinabaki finyo sana labda wanaume waliofiwa na wake au wakubali kuwa nyumba ndogo.Wito kwa wasichana siku hizi midume mingi haipendi kuoa sana sana wanatamani kwa muda tu wakishapata hawana habari.Kuna binti mmoja aliwahi kuniomba ushauri kuhusu kuolewa na jamaa ambaye hakuwa msomi wa level yake [yeye chuo kikuu mwanaume mwalimu wa primary],nilijaribu kumshawishi amkubali kwasababu umri wake ulishakimbia sana na nilimwambia pengine ni nafasi yake ya mwisho kusikia kauli ya namna hiyo.walioana miaka minne iliyopita wamefanikiwa kupata mtoto mmoja zuri zaidi mwanaume anamalizia shahada ya kwanza chuo kikuu huria.Wanawake vigezo vingine vinaweza kupatikana ndani ya ndoa mfano elimu,nyumba,gari na nk
 
Huyo dada anatakiwa ajue ndoa sio ya kila mtu, kama mungu amepanga aolewe basi atakuja kuolewa other than that asilazimishe ndio mambo ya kuja kuishia kuwa miserable.
 
Ndoa itakuja tu..vuta subira.
Ukichunguza kwa makini sana utaona kuwa kuna rika kwa mwanamke ambapo kuombwa ndoa na mwanaume kunakuja kirahisi zaidi - hii ni miaka kuanzia 20-25 ( nimesema na narudia tena mara nyingi siyo mara zote) - umri huu msichana hupata wachumba/waume kwa urahisi sana. Ukishavuka 30 chances hupungua lakini haina maana kuwa hawapati wachumba.

..........WoS hapo umenena katika umri huu 20-25 unapata wanaume wengi wanaotangaza nia ya kuoa mie nilijionea unafanya kuchagua tu.Ila sema cha msingi uwe makini kuchagua huyo mume sio ilimradi uolewe.
 
Miye nakumbuka nikiwa na miaka 21 nilikataa wachumba 7!
Ila nilipofika miaka 23 nikakubali kuolewa na mchumba niliyeona anafaa kwa wakati ule.
Hadi leo tuko pamoja. Wasichana jamani msichezee bahati inapokuja. Usitafute sana vigezo vua kupita kama pesa na mali. Angalia tabia njema na kumcha Mungu.Ikiwezekana muwe wa imani moja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom