Wenyeviti wa vitongoji Bunda kuiburuza Halmashauri yao Mahakamani

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Kuandamana kupinga kuondolewa uenyeviti wa vitongoji


na Ahmed Makongo, Bunda


amka2.gif
JUMLA ya wenyeviti 14 wa mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, mkoani Mara, wamesema kuwa wataingia mahakamani kupinga hatua ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, Cyprian Oyier, kuwaandikia barua kwamba kuanzia sasa sio wenyeviti wa vitongoji.
Wenyeviti hao wakiwemo waanzilishi wa mji mdogo wa Bunda, wakati huo ukiwa na vitongoji 14 tu, hivi karibuni wameandikiwa barua na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, Oyier, kwamba kuanzia sasa sio wenyeviti wa vitongoji hivyo.
Wenyeviti hao ambao 12 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mmoja Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), wamedhamiria kwenda mahakamani kupinga uamuzi huo, kutokana na kuchaguliwa kwa mujibu wa sheria hivyo ni viongozi halali.
Akizungumza na Tanzania Daima Erenest Nkonoki mwenyekiti wa kitongoji cha Mbumatare, ambacho awali kilikuwa Nyamakokoto, alisema hakuna kikao chochote kilichopitisha maazimio ya kuwaondoa madarakani hali ambayo imewafanya waamue kufanya maandamano ya amani ya kupinga maamuzi hayo.
‘Sisi lazima twende mahakamani kupinga uamuzi huu maana sisi tumechaguliwa kihalali kabisa na wananchi wanatuamini sasa leo hii tuchakachuliwe kiasi hiki….. hatukubali, wananchi wameamua kufanya maandamano ya amani katika kupingana na hilo,” alisema.
Kwa upande wake Oyier amekiri kuwaandikia barua ya kutowatambua wenyeviti hao 14 na kwamba amefanya hivyo kwa mujibu wa sheria na kuongeza kuwa ufafanuzi kamili juu ya suala hilo atatoa kesho Desemba 13.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kupata nakala ya barua iliyoandikwa na mkurugenzi huyo ambayo ina kichwa cha habari kisemacho ‘Marekebisho ya vitongoji katika kata, mamlaka ya mji mdogo wa Bunda’ iliyoandikwa Desemba 3, mwaka huu.
Barua hiyo inasema: “Mnafahamishwa kuwa kutokana na marekebisho yaliyofanywa katika sheria ya serikali za mitaa (mamlaka ya wilaya) sura ya 287, tangazo la serikali Na. 173/2010, (Amri ya kugawa maeneo mapya katika kata) ya mwaka 2010, tangazo hilo limefanyiwa marekebisho tangazo la serikali namba 205/2009.”
Aidha, barua hiyo inawataka wenyeviti wa vitongoji hivyo kukabidhi vifaa vyote vya ofisi zao, zikiwemo mihuri kwa watendaji wa kata zao husika ambapo taarifa ya makabidhiano hayo inatakiwa ifanyikie ofisini kwa mkurugenzi huyo, siku 7 kuanzia tangu kutoka kwa taarifa hiyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom