Wenyeji wa Muleba Kusini, Muleba na Kagera kwa ujumla, niandaeni jamni nichukue jimbo!

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Hapa namaanisha. Namheshimu sana Prof. Ana ila mkinipa mawazo na weakness za prof, nmna ya kuingia na jinsi ya kuchukua ubunge baada ya prof. au kipindi kijacho ili niwatumikie wananchi.

Binafsi nahisi CCM hawezi kiingia mtu mzuri na ata akiingia basi ataharibika tu. Mfano mzuri ni Pinda.

NIPENI MAWAZO
 
Yaani unadhani tupo hapa kuwapa mawazo wahuni? yaani wewe unadhani ubunge ni kazi ya kuchukuwa tu basi, una kitu gani au plan gani unazotaka kuzifanya kwenye jimbo hilo?
Je mbunge wa sasa aliahidi nini na hii ni miezi 6 tu imepita una vigenzo gani vya kupima utendaji kazi wake?
Ushauri kama hauna kazi ya kufanya tafuta kazi kwa bidii utapata au jiunge na ujasiriamali utafanikiwa, usidhani ubunge ni kijiwe cha wahuni walioshindwa maisha kwenda kudumaza maendeleo ya umma.
 
Mkuu kijoka haujawa wazi hata kidogo hadi tutashindwa kueleza chochote. Ila usitafute udhaifu wa prof.jali unachoweza wewe. Nikuhakikishie kuwa prof 2015 hatoweza kurudi kwa uzee alionao na sababu nyingi. Ukumbuke pale muleba,ANNA hakushinda kwa kuwa masilingi alikuwa na udhaifu,hapana. Ukitaka kushindana na uyu mama muulize mzee Tibaigana au masilingi,alimwaga ela mpaka basi. Cha muhimu ni kutafuta kura kwa wananchi na si kushindana na wenye ela.
 
Yaani unadhani tupo hapa kuwapa mawazo wahuni? yaani wewe unadhani ubunge ni kazi ya kuchukuwa tu basi, una kitu gani au plan gani unazotaka kuzifanya kwenye jimbo hilo?
Je mbunge wa sasa aliahidi nini na hii ni miezi 6 tu imepita una vigenzo gani vya kupima utendaji kazi wake?
Ushauri kama hauna kazi ya kufanya tafuta kazi kwa bidii utapata au jiunge na ujasiriamali utafanikiwa, usidhani ubunge ni kijiwe cha wahuni walioshindwa maisha kwenda kudumaza maendeleo ya umma.

mkuu ktk siasa hasira na maneno yako ya kejeli hayafai. Uyu ndugu kaweka hoja asaidiwe we unabwatuka,haifai.
 
Ndugu,
Pamoja umeomba wenyeji wa Muleba Kusini,muleba na Kagera wakuandae Uchukue Jimbo!Mie Mkweche siyo wa Huko
Ila Nakutahadharisha kwamba Unatakiwa Ujiandae mwenyewe kabla Hujaandaliwa!Je wewe umejiandaaje na kwa Maandalizi hayo umejipimaje ukaona wewe ndie Candidate Unaefaa zaidi!
Angalia 'Jamaa wa Tangazo la Master Card' Alijiandaa lakini bado ikaoneka hajakamilisha mambo,Kazi ya Ubunge si ya Kwenda Mjengoni tu sehemu kubwa inatakiwa ni namna na Uwezo wa Kuwaongoza wapiga kura Kujipatia Maendeleo!
JIPANGE Ndugu ila Usicheze Rough
 
mkuu ktk siasa hasira na maneno yako ya kejeli hayafai. Uyu ndugu kaweka hoja asaidiwe we unabwatuka,haifai.
Mtu asiyejuwa hata kazi ya mbunge unataka kumshauri nini? au unadhani ubunge ni kijiwe cha kwenda kupunguza ukali wa maisha?, nyinyi watu wa CHADEMA ndio maana mnaingizwa mkenge kirahisi na wehu kama akina Shibuda.
 
kajenge mradi wa maji nawe, inasikitisha huyu mama kakubali kuwa wazri wa JK!
 
Back
Top Bottom