Wenye malori waridhia kodi ya mafuta ya taa kupanda

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Monday, 14 June 2010 21:00

mabasi.jpg

UMOJA wa Wamiliki wa Maroli na Waagizaji wa Mafuta (Tatoa), umesema kuwa serikali inapoteza zaidi ya Sh25 bilioni kila mwezi kutokana na tatizo la uchanganyaji wa mafuta, ambao wiki iliyopita ulisababisha magari ya Ikulu yashindwe kufanya kazi.

Wamiliki hao, ambao magari yao yanaathirika zaidi na vitendo hivyo kutokana na kutumia dizeli, wamesema ushauri wa wabunge wa kutaka kuongezwa kodi kwenye mafuta ya taa ni faraja kubwa kwao kwa sababu bei ndogo ya mafuta ya taa ndiyo inayowapa vishawishi wafanyabiashara wenye tamaa kuchanganya mafuta hayo na dizeli ili wajipatie fedha nyingi.

Mwenyekiti wa Tatoa, Seif Ally Seif alisema katika kila lita ya mafuta ya taa inayochukua nafasi ya dizeli serikali inapoteza Sh462 wakati kwa kila lita ya petrol serikali inapoteza Sh487 na kwamba kodi ya lita milioni 36 za mafuta ya taa ambazo zinachanganywa kila mwezi ni Sh17 bilioni.

Alisema tayari magari 150 yamekamatwa nchini Rwanda na Burundi yakiwa yamebeba mafuta yaliyochanganywa na kwamba serikali ya Rwanda imeamua kuzuia shehena za mafuta yake kupitia Tanzania.

Alisema tatizo hilo lilianza kidogo kwa wastani wa lita 200 hadi 300 za mafuta ya taa kwa gari moja la petrol ama la dizeli, lakini hivi sasa limekua na kufikia lita 16,200.

Mwenyekiti huyo alisema kutokana na uchanganyaji huo kwa kila safari moja madereva wamekuwa wakijipatia Sh4.3 milioni wakati kiwango cha juu ni Sh14.5 milioni.

Alisema uchanganyaji wa mafuta una athari kubwa kama vile kupoteza biashara ya kusafirisha mafuta, uharibifu wa magari, majenereta, injini za treni, mitambo inayotumika kwenye kilimo, viwandani, uchimbaji madini, utengenezaji wa barabara, ujenzi, kusukuma maji na kufua umeme.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope alisema tatizo la uchanganyaji wa mafuta lilianza tangu wakati wa utawala wa Ally Hassan Mwinyi kwa kuwa aliwahi kukumbwa na mkasa huo wakati huo Rais Jakaya Kikwete akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

“Rais Mwinyi alipokumbwa na tatizo hili siku ile ile jioni, kodi ya mafuta ya taa ilipandishwa na alipokuja Kikwete ilishushwa kwa nia njema ya kumsaidia mwananchi lakini inatumika kifisadi,” alisema Hanspope.

Alisema tatizo hilo linakua kwa kasi kwa sababu uagizaji wa mafuta ya taa kwa sasa unalingana na ule wa mafuta ya dizeli na petrol.

Mkurugenzi huyo alizitaja sehemu zinazotumika kuchanganya mafuta hayo kuwa ni Chalinze, Gairo na Kibaigwa na kwamba walijitahidi kuweka ulinzi wao wenyewe, lakini hawakufanikiwa kutokana na waliowekwa kulinda kukubali kupokea hongo.


Wenye malori waridhia kodi ya mafuta ya taa kupanda
 
Back
Top Bottom