WENYE MALI HAWANA AKILI,WENYE AKILI HAWANA MALI-By,. Mh.Temba

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Nimekuwa nikibishana na rafiki yangu,nakumwambia kuwa Mh.Temba kwenye huu wimbo wake hii point ameongea pumba kwenye verse ya pili aliposema,WENYE AKILI HAWANA MALI,WENYE MALI HAWANA AKILI
Rafiki yangu anajidai kuwa CORRECT IS EQUAL TO CONSISTENCY.
CONSISTENCY (inavyojieleza,)In logic, a consistenttheoryis one that does not contain a contradiction.The lack of contradiction can be defined in either semantic or syntactic terms.
Conclusion yake anadai kwamba Temba yuko sahihi kuwa WENYE AKILI HAWANA MALI NA WENYE MALI HAWANA AKLI.
Tumekuwa tukibishana kwa mda mrefu sana.
Ina maana kina Billget wana mali na hawana akili?


http://www.youtube.com/watch?v=gtXtSuRCIt4



WENYE AKILI HAWANA MALI,WENYE MALI HAWANA AKILI.............ni kweli au pumba?
 
Its true kabisa, hasa kwa hii bongo yetu waliowengi wanamali lakini ukifuatilia backgrounds ya shule ni vilaza au wameiba mali za umma. Na ndio wanaotawala siasa kwa sasa. Huu ni ujumbe mzuri sana. Mtazamo wangu
 
Kama hana akili angepataje mali huko ndo kutofikiria wewe mwenye akili kwani akili zako unazipeleka wapi?.Jipeni matumaini ya kijinga
 
Its true kabisa, hasa kwa hii bongo yetu waliowengi wanamali lakini ukifuatilia backgrounds ya shule ni vilaza au wameiba mali za umma. Na ndio wanaotawala siasa kwa sasa. Huu ni ujumbe mzuri sana. Mtazamo wangu
Sasa kama hawana akili wamekuwaje na akili za kuiba mali?
 
Kama hana akili angepataje mali huko ndo kutofikiria wewe mwenye akili kwani akili zako unazipeleka wapi?.Jipeni matumaini ya kijinga
ndo nachojiuliza hata mimi,atapataje mali bila akili?
 
Tofautisheni akili za kuiba mali/fedha, akili za darasani, akili za maisha na 'common sense'. Mbona JK ni mwizi wa mali za umma, lakini darasani UDSM alikuwa kilaza? Mbona akili za kuongoza nchi hana? Lakini kwenye wizi ni namba 1. Mfano mwingine waziri chami, darasani alikuwa kipanga, lakini uongozi ulimshinda.
Tukija kwa watu kama kina Gates, Jobs, Zuckberk etc, hawa darasani walikuwa wa kawaida sana, ila wana akili au vipawa vya uvumbuzi, and they are thinking positively...
All watu wenye negative minds, hawawezi kufikilia positive, mfano wa negative minds ni kama hizo akili za wizi... Ndio maana KJ (Kubwa Jinga), akiachana na akili ya wizi, anabaki na akili ya kufungua zipu TU, lakini umeshasikia Gates ana akili za kufungua zipu?? Tafakari...
 
Kila kitu chenye thamani hupimwa kwa kizio chake. Kipimo cha akili ni IQ (Intellegent Quotient) Mtu aweza kumaliza madarasa mengi tu, lakini IQ yake ikawa ndogo sana. Hali kadhalika mtu aweza asiwe na darasa hata moja lakini akawa na IQ ya juu. Mafanikio kielimu yanategemea vitu vingi mfano nafasi (opportunity), wazazi wake wanauwezo wa kumpeleka shule, bidii (effort) mtu anauwezo wa kukariri au kusoma kwa muda mrefu hadi anakesha halafu anapata pass mark. Kuwa na PhD sio kiashiria pekee cha kuwa na akili.
Mafanikio ya kupata pesa pekee pia sio kigezo cha kuwa na akili. Yawezekana mtu akapata mtaji kidogo tu lakini akauendeleza kwa kujinyima. Uwizi sio kigezo cha kuwa na akili. Hata hivyo watu wengine ni wepesi wa kuona fursa na kuzitumia.
Akili katika maisha ni uwezo wa kuchanganya vyote darasani, maisha nk lakini inategemea unataka kumpima mtu katika nyanja gani. Upimaji wa elimu ya darasa au maisha au ukichanganya vyote weka uwiano (ratios) kutegemea uzito
 
MALI - inaweza kuwa ni fursa rasilimali zinazokuzunguka; hii ipo sana katika nchi yetu, kuna maeneo watu wamezungukwa na mali lakini hawana akili ya kuzifanya kuwa mali kwao.
 
1st huo msemo labda uufananishe na ile methali "penye mti mingi hapana wanyenzi" ,hapa ni kama unafananisha na nchi ina raslimali lakini hawatumii akili iendelee wageni wanakuja beba tu

2nd lakini sio kweli kwamba wenye mali hawana akili, na ni akili zipi haswaa anazomaanisha mh temba?
sababu kupata kwenyewe mali ( za kihalali ) ni akili imetumika !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom