wenye dini na wasio na dini nikaribisheni

lovulovu

Member
Jul 22, 2009
20
5
naitwa lovulovu, mkazi wa jijini, mpagani kwa dini au kwa lugha rahisi kafiri. nimefurahia sana mtandao huu nami naomba mnikaribishe tuungane tuweze kubadilishana mawazo hasa hili la kutaka eti kutumia kodi yangu kuwalipa mahakimu wa waungwana wasiokula visivyochinjwa waitwao makadhi na mengine mengi kama ya uchumi, siasa, elimu na kadhalika na kadhalika.
lovulovu
 
mpagani? huna upagani wowote, intro yako inajionyesha wewe ni wa upande upi, hapa umefika maana ndio kwenu, hujakosea njia,
 
Nenda sayari ya mars ukaishi peke yako huko. kama huna dini, utakuwa hauna akili, kwasababu hata ndege wa angani wanajua kuwa kuna Mungu. ndege wa angani wanataka kukuzidi akili mzee..hahaha.
 
naitwa lovulovu, mkazi wa jijini, mpagani kwa dini au kwa lugha rahisi kafiri. nimefurahia sana mtandao huu nami naomba mnikaribishe tuungane tuweze kubadilishana mawazo hasa hili la kutaka eti kutumia kodi yangu kuwalipa mahakimu wa waungwana wasiokula visivyochinjwa waitwao makadhi na mengine mengi kama ya uchumi, siasa, elimu na kadhalika na kadhalika.
lovulovu

Tumeingiliwa,

Lovulovu,

Wewe si Mpagani.

Wewe ni kristo!

Mgalatia, mfuasi wa Paulo.

Usitudanganye hapa!
 
MAMBO YA WENYE DINI HAYA

Mchungaji atiwa mbaroni kwa kukutwa na viungo vya albino

Habari Nyingine
• Mchungaji kortini kwa madai ya kukutwa na viungo vya binadamu 21.02.2009 [Habari Zaidi]
• Mwanahabari ‘anasa' muuza viungo vya albino 21.07.2008 [Habari Zaidi]
• Wawili mbaroni wakisaka albino 17.12.2008 [Habari Zaidi]

NA PETER KATULANDA, MWANZA

WATU wanane wakiwemo waganga wa kienyeji wawili na Mchungaji wa Kanisa la Baptisti la wilayani Magu, wametiwa mbaroni wakiwa na viungo vya albino, Aron Mongo, aliyeuawa Mkolani wilayani Nyamagana jijini Mwanza.

Watuhumiwa hao walikamatwa juzi kwa nyakati tofauti, baadhi yao akiwemo mchungaji wakiwa katika harakati za kutafuta soko la kuuza kiungo hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Jamal Rwambow, akitoa taarifa za kukamatwa kwa wauaji hao jana, alisema polisi limewakamata watuhumiwa wakiwa na mfupa wa mguu ambao walikiri ni wa mlemavu huyo aliyekuwa mkazi wa Ibanda Relini Mkolani.

Alisema mbali na mfupa huo, walikamatwa wakiwa na nyama za marehemu ambazo walizitupa sehemu tofauti, ambazo zimekutwa zimeharibika na polisi wamezihifadhi kwa ajili ya vielelezo na uchunguzi wa kitaalamu.

Rwambow alisema kukamatwa kwao kumetokana na taarifa za raia wema wawili ambao jeshi hilo limewazawadia sh. Nilioni moja kama lilivyotoa ahadi kwa wananchi kuwa atakayefanikisha kupatikana kwa watuhumiwa wa mauaji ya Mongo, watazawadiwa kiasi hicho.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Mchungaji Alfred Komanya (35) wa Kanisa la Baptist Irungu wilayani Magu, Chacha Jeremiah (30) na Mathew Mlimi (21) wakazi wa Mahina wilayani Nyamagana jijini hapa.

Waganga waliokamatwa ni Gervas Lutufu (58) mkazi wa Nyanguge wilayani Magu na Kishosha Lutambi au Komanya (60) mkazi wa Mahina wilayani Nyamagana ambao pamoja na viungo hivyo, wamekutwa wakiwa na nyara za serikali na tunguli za uganga.

Nyara walizokutwa nazo ni ngozi mbili za wanyama ambao hawakufahamika mara moja, ndege mmoja aliyekaushwa (hakufahamika jina) na mkia unaodhaniwa kuwa wa nyumbu.

Wengine ni Paschal Lugoye au Mashiku (28) mkazi wa kijiji cha Semba Katani Buhongwa, Paul Lumalija (36), mkazi wa kijiji cha Kishili Kanindo Katani Igoma na Alex Joseph au Bugwema Silola (24) mkazi wa Mahina.

Rwambow alisema baada ya kuhojiwa watumiwa walikiri kuhusika na mauaji ya Aron Mongo yaliyotokea Juni 26, mwaka huu Ibanda Relini.

Alifafanua kuwa wamebaini mganga wa jadi Kishosha, aliwahi kumtibu marehemu na mahali anapoishi si mbali sana na yalipokuwa makazi ya albino huyo na kuwa mganga na mchungaji huyo ni ndugu.

Kamanda huyo alisema polisi bado inaendelea na uchunguzi wa kina dhidi ya watuhumiwa hao na mtandao mzima wa wauaji wa walemavu hao na kuwaomba wananchi wazidi kulipa ushirikiano ili litokomeze mauaji hayo ya kikatili.
 
Nenda sayari ya mars ukaishi peke yako huko. kama huna dini, utakuwa hauna akili, kwasababu hata ndege wa angani wanajua kuwa kuna Mungu. ndege wa angani wanataka kukuzidi akili mzee..hahaha.

kuamini kuwa kuna mungu na kuwa na dini ni vitu tofauti. AU?
 
naitwa lovulovu, mkazi wa jijini, mpagani kwa dini au kwa lugha rahisi kafiri. nimefurahia sana mtandao huu nami naomba mnikaribishe tuungane tuweze kubadilishana mawazo hasa hili la kutaka eti kutumia kodi yangu kuwalipa mahakimu wa waungwana wasiokula visivyochinjwa waitwao makadhi na mengine mengi kama ya uchumi, siasa, elimu na kadhalika na kadhalika.
lovulovu

kwa kuandika tu hayo maneno nilioweka red color tayari tumeelewa kuwa wewe si mpagani,tena inaonekana wewe ni mdini chronic ndo maana umeingia hapa ni mkwara ati ni mpagani,ndani ya forum hii kuna watu makini na wanajua kuchambua neno baada ya neno na kukupata vilivyo,tumeshaelewa wewe ni mfuasi wa dini ipi kwa hiyo usifikiri unatudanganya sisi bali elewa kuwa unajidanganya mwenyewe

Tunakuomba usituletee mamabo ya udini huku ndani.
 
Lovulovu, umeingia kwa kishindo mno kana kwamba si mgeni bali ni mwenyeji. Ndo mana watu hawakukaribishi kwa "karibu" ya kawaida bali wanaanza kukujadili mara moja kwani umejitambulisha huku ukiwa na "limada". Mi nasema "Karibu mkuu".
 
nilitarajia kukaribishwa kwa maneno ya upendo na upole. bahati mbaya hilo halikutokea bali nimekaribishwa kwa maneno ya kunituhumu na mengine ya kunibeza eti mimi na katoliki mgalatia mkubwa. hata hivyo miye nimefurahishwa sana na mawazo ya watz wenzangu. na wengine tayari wameanza kunijadili kana kwamba mimi ni mkongwe wa mtandao huu, inafurahisha sana.
well, nimekaribia sasa. tatizo langu ni namna ya kujua hot topic of the day. tatizo langu ni ugeni wa mtandao maana kuna heading nyingi nami napata taabu kufungua zote ili kujua siku hiyo yametolewa mawazo yapi mapya na mtu gani? hata hivyo nitajitahidi kufuatilia huku na kule kujua kinachoendelea.
lovulovu
 
naitwa lovulovu, mkazi wa jijini, mpagani kwa dini au kwa lugha rahisi kafiri.
lovulovu

Kwa kutaja Kafiri, sisi wana saikolojia tayari tumejua kuwa wewe uko kwenye Dini ile ila unatakakijificha chini ya meza ya ukafiri.
Mimi sikukaribishi kabisa.
Labda uje kwa uwazi.
 
kwa kuandika tu hayo maneno nilioweka red color tayari tumeelewa kuwa wewe si mpagani,tena inaonekana wewe ni mdini chronic ndo maana umeingia hapa ni mkwara ati ni mpagani,ndani ya forum hii kuna watu makini na wanajua kuchambua neno baada ya neno na kukupata vilivyo,tumeshaelewa wewe ni mfuasi wa dini ipi kwa hiyo usifikiri unatudanganya sisi bali elewa kuwa unajidanganya mwenyewe

Tunakuomba usituletee mamabo ya udini huku ndani.

Tume mgundua mkuu.
Msindima, huyu mwanadini anadhani MSINDIMA HANA KAZI?
 
Karibu jukwaani, udini ulianzia ndani ya Ilani ya uchaguzi CCM, 2005 kifungu cha 108, ambapo ilani hiyo ilivalishwa kibaraghashia!
 
Masuala ya kuzungumzia dini za watu hayatupeleki popote na sana yanaweza kubadilisha mtazamo mzuri wa jamii forums. Wewe kama mpagani au kafiri kama unavyojiita heshimu imani za watu wengine. Kumbukeni kuwa migongano ya kidini yameleta machafuko katika nchi nyingi, sidhani kama kuna mtanzania anapenda kuona machafuko!!
 
Back
Top Bottom