Elections 2010 Wenje + Mbowe VS Masha: Hii itakuwa ni kumaliza kabisa

kasyabone tall

JF-Expert Member
Sep 13, 2009
254
59
Mimi napendekeza kwa CHADEMA kuwa kuna haja kubwa ya mbowe kumsaidia kampeni WEnje hata kwa siku moja tu.Nawaangalia hawa watu kwa mtazamo kwamba Masha anajifanya mtoto wa mjini, Sasa akipelekewa mtoto mjanja wa mjini zaidi hali itakuwa safi sana kwa CHADEMA. Wenje sina mashaka kuwa anamuweza Masha lakini Mbowe atammaliza kabisa. Masha hawezi furukuta kwa Mbowe hata kidogo. Napendekeza kwa viongozi wa chadema kama itawezekana Mbowe aende kumsaisia Wenje hata kwa siku moja tu.
 
Wakuu wa Chadema wote wako kamili mwanangu!...Marando ndo Mwanaizaya zaidi, utadhani wa mama mmoja wote!..Usipate shida Nyamagana ni yetu!
 
Nakumbuka enzi zile kama kuna sehemu mambo yanakuwa yamebana CCM walikuwa wanampeleka Mzee Malecela aka Tingatinga kusawazisha. Kwa Chadema nao wanao Troubleshooters kama mpiganaji Marando aka Che Guevara na wengineo wengi (Zito, Mbowe, Lissu) wanaweza tumwa na chama kwenda sawazisha mambo inapobidi!!! Tanzania bwana, mambo Tambarare!!!
 
Nakumbuka enzi zile kama kuna sehemu mambo yanakuwa yamebana CCM walikuwa wanampeleka Mzee Malecela aka Tingatinga kusawazisha. Kwa Chadema nao wanao Troubleshooters kama mpiganaji Marando aka Che Guevara anakwenda sawazisha mambo!!!
kwa sasa ccm wana Riz 1 na mama hatoki mtu hapo!
 
Masha kashikwa pabaya. Historia inamhukumu na watu wamechoka kuburuzwa. wenje anasubiri kuapishwa... Sijui yu hali gani hasa baba wa mshkaji wake anaponing'inizwa pia. Maana anajua uwaziri alipewa kwa sababu ya dogo. Baba anatemwa, yeye anatemwa sa sijui nani atambeba mwenzie

Amakweli siku za kufa nyani....................
 
Watu wa Mwanza Nyamagana ni yetu.

Masha aliaanza kuweweseka hata kabla ya uteuzi wa Wenje akidai siyo raia. Tume wakampiga na chini. Nasikia mkakati wake kwa sasa ni kutumia wadhifa wa Waziri wa Mambo ya ndani na Jeshi la Polisi kuchakachua matokeo.

Na kama NEC watamtangaza Masha kuwa Mshindi LAZIMA TUENDE MAHAKAMANI LAZIMA WATAKUWA WAMEIBA KURA.
 
Kwa hali nilivyoona Nyamagana Jana TBC1 saa nne usiku, Masha aandike maumivu hata kama Mbowe hatakwenda kule.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom