"Wengi Wape"...Uamuzi Mzito

umuhimu wa kwanza ni...

  • Total voters
    40
Swali gumu hili, ila kwangu naona kizazi cha Leo tumependa sana Kipato ama mali kuliko Familia, nasema hivi kwa sababu, unapata mtu katokomea hukooo nchi za mbali. Mtu akaa miaka ya kuhesabu, kipato anachopata wastan, pia nae ana mahitaji na maisha pia huko aliko si rahisi, huku nyumbani akituma, hela zenyewe hazitoshi....uzushi na wasi wasi unaanza.

Kumbuka wakati huo huo watoto wanakosa malezi na uzazi wa wawili. Mimi naona wakati mwengine, tukae chini kwanza na kujiuliza kama shughuli yenyewe itajipa kwa manufaa ya sasa na siku za baadae kwa familia. Familia jama....iwe kitu cha kwanza..isiwe Baba unasafiri mpaka ukirudi humkumbuki mwanao!!!!!Na pia ukiwa huko nje miaka Minne mitano..Kumbuka Hapo Mkeo au Mumeo umemwaachia majukumu yoote na huzuni!!!!
 
...dahhh, am speechless kaka...na kweli, katika miaka kumi na mbili nikijumuisha najikuta nimeishi na familia siku 365 tu!

Swahiba,

Unaona hizo zinatosha au ni nyingi sana???

Kama ingewezekana, basi ningependa nisikae mbali na familia yangu kwa zaidi ya miezi 3 mfululizo!!

Kuna kipindi nilisafiri, nikamwacha first born wetu ana miezi 4 na huko nikaa miezi 3. Niliporudi nikakuta mtoto ana miezi 7 na anaanza kufahamu watu na vitu....Yaani alinichunia na kuniangalia kama kinyago... I failed to resist, na kuanza kumwaga machozi!!

Labda naumwa ugonjwa wa kuwa na familia yangu ....ila niko tayari tule majani ili mradi tuko wote na tuko wazima!! Mbona Watanzania walikula majani wakanunua ndege ya Rasi??? Jambo la muhimu ni kuelewana na kukubali kuishi kadri ya kipato chenu!!!!

Babu DC!!
 
Swali gumu hili, ila kwangu naona kizazi cha Leo tumependa sana Kipato ama mali kuliko Familia, nasema hivi kwa sababu, unapata mtu katokomea hukooo nchi za mbali. Mtu akaa miaka ya kuhesabu, kipato anachopata wastan, pia nae ana mahitaji na maisha pia huko aliko si rahisi, huku nyumbani akituma, hela zenyewe hazitoshi....uzushi na wasi wasi unaanza.

Kumbuka wakati huo huo watoto wanakosa malezi na uzazi wa wawili. Mimi naona wakati mwengine, tukae chini kwanza na kujiuliza kama shughuli yenyewe itajipa kwa manufaa ya sasa na siku za baadae kwa familia. Familia jama....iwe kitu cha kwanza..isiwe Baba unasafiri mpaka ukirudi humkumbuki mwanao!!!!!Na pia ukiwa huko nje miaka Minne mitano..Kumbuka Hapo Mkeo au Mumeo umemwaachia majukumu yoote na huzuni!!!!

Chiko,

Nakubaliana na wewe kabisa,

Nadhani tunapata tatizo kuainisha, ni kipi bora kati ya means (kipato) and meaning (family) of life??

Na kipindi kinachoongelewa hapa ni karibia 1/10 ya karne (10yrs au zaidi)...

Kitu ambacho hatujiulizi ni kwamba, kipindi hicho uko mbali, familia yako unamwachia nani ili wewe ukahagaike na kipato??

Babu DC!
 
Swali gumu ila nimefurahishwa na maoni ya wasomaji wengi kwani wameeleza vema, mambo yote hayo ni muhimu sana kama inakulazimu kuwa mbali na familia yako kwa manufaa ya familia pia na kwa muda fulani huna jinsi ila yakupasa kuwa na mipango yakinifu uhakikisha kwamba kila mara itokeapo nafasi ya wewe kuwa na familia yako basi make sure unaitumia nafasi hiyo vizuri na familia yako. Kuna mifano mingi ya watu ambao waliacha kazi zenye fedha malipo makubwa kwa sababu ya familia ila wao tayari walikuwa na uwezo mkubwa sana na walikuwa na option nyingine na tamaduni pia zilichangia wao kuamua hivyo, ila pamoja na hayo yote bado nakushauri usiipoteze hiyo nafasi ila tumia vema likizo pamoja na familia with time mambo yatakaa sawa tu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...nashukuru sana kwa maoni yako, ubarikiwe.
 
Swahiba,

Unaona hizo zinatosha au ni nyingi sana???

Kama ingewezekana, basi ningependa nisikae mbali na familia yangu kwa zaidi ya miezi 3 mfululizo!!

Kuna kipindi nilisafiri, nikamwacha first born wetu ana miezi 4 na huko nikaa miezi 3. Niliporudi nikakuta mtoto ana miezi 7 na anaanza kufahamu watu na vitu....Yaani alinichunia na kuniangalia kama kinyago... I failed to resist, na kuanza kumwaga machozi!!

Labda naumwa ugonjwa wa kuwa na familia yangu ....ila niko tayari tule majani ili mradi tuko wote na tuko wazima!! Mbona Watanzania walikula majani wakanunua ndege ya Rasi??? Jambo la muhimu ni kuelewana na kukubali kuishi kadri ya kipato chenu!!!!

Babu DC!!

...mkuu we acha tu kiongozi, inauma sana...na kuna mengine yanayoumiza zaidi mfano kama huo ulotoa
mwanao wa kumzaa anapokuangalia kwa jicho la "...huyu nae nani!" au utaniambia nini wewe, kwani ulikuwa wapi
maisha yangu yote.

Hiki kisu kinakata kote kote,....mfano mzee wangu, yeye alikuwa anafanya zile kazi za wito...24hrs yupo on call ila alihakikisha kila jumapili ni family day. Bahati mbaya, elimu yangu ya sekondari yote nilisomea boarding school, mambo ya kurudi nyumbani twice a year...

...ipo siku tayari nishamaliza chuo, naye umri ushamuingia tumekaa tunapiga story na kucheka...ikamtoka
" ...nimepoteza a valuable time ya kukuona ukikua mpaka leo ushakuwa mtu mzima tunaongea haya!"...aisee, siwezi kusahau
huzuni yake alipoyatamka maneno hayo.

Mwenyezi mungu amrehemu huko alikolala.

Moskwito, I learned this from my old boss, wakati nataka kurukia kazi nyingine. Aliniambia money will never be enough, u think I am being paid a lot but iu still have money issues! I proved it for myself, japo I quited the new-better-paying job in 4months manake yalikuwa yananichachia. You are now dying to live, trust me. Kwani ukikaa na familia huwezi kupata the basics (if it is not too late), kama its too late already, u know what I mean with this; weeh jilipue tu babangu!

...huwa najiuliza ni lini inafikia kikomo cha kusema sasa kimetosha.
Naamini ni majukumu tu yanabadilika.
 
Moskwito, pole about your dad. Na ungeoa mzungu ndo angetia akili, manake angemuuliza 'what was mbu like when he was a boy?' Abaki anajiuma! You see, walau alikuwa anajitahidi jumapili kuwepo home... Sasa hii life yetu! Dah!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Moskwito, I learned this from my old boss, wakati nataka kurukia kazi nyingine. Aliniambia money will never be enough, u think I am being paid a lot but iu still have money issues! I proved it for myself, japo I quited the new-better-paying job in 4months manake yalikuwa yananichachia. You are now dying to live, trust me. Kwani ukikaa na familia huwezi kupata the basics (if it is not too late), kama its too late already, u know what I mean with this; weeh jilipue tu babangu!

Ahsante dada,

Hiki ndicho nimekuwa nikiongea wakati wote...Watu wanahangaika ila wanasahau kuwa safari moja huanzisha nyingine...Unapata pesa nyingi na hapo unaanza lust ya kutafuta nyingi zaidi.

Tunashindwa kujiuliiza, why mtu kama Bill Gates bado anafanyakazi??
 
...mkuu we acha tu kiongozi, inauma sana...na kuna mengine yanayoumiza zaidi mfano kama huo ulotoa
mwanao wa kumzaa anapokuangalia kwa jicho la "...huyu nae nani!" au utaniambia nini wewe, kwani ulikuwa wapi
maisha yangu yote.

Hiki kisu kinakata kote kote,....mfano mzee wangu, yeye alikuwa anafanya zile kazi za wito...24hrs yupo on call ila alihakikisha kila jumapili ni family day. Bahati mbaya, elimu yangu ya sekondari yote nilisomea boarding school, mambo ya kurudi nyumbani twice a year...

...ipo siku tayari nishamaliza chuo, naye umri ushamuingia tumekaa tunapiga story na kucheka...ikamtoka
" ...nimepoteza a valuable time ya kukuona ukikua mpaka leo ushakuwa mtu mzima tunaongea haya!"...aisee, siwezi kusahau
huzuni yake alipoyatamka maneno hayo.

Mwenyezi mungu amrehemu huko alikolala.

Pole sana mkuu,

Bahati mbaya haya mambo ya familia watu wengi huyakumbuka when it is too late!!

Binafsi sipendi kufanya kosa la namna hiyo...

Babu DC!!
 
Babu DC, unajua wengi wetu tunachukulia familia kuwa ni 'watoto', tunasahau mwenza nae ni sehemu ya kwanza ya familia zetu. Hili ni janga la kitaifa, siku hizi tunaoana kila mtu ana kazi yake seemingly nzuri mkoa mwingine. Ile tabia ya wanawake ku-sacrifice kazi zao tulishaiacha siku mingi kwa sababu ya kudanganywa (deceived sounds better). Mwisho wa siku by the time mnakaa pamoja mke ni mzururaji kajizoea ufugaji huria, mume ndo usiseme na magroup ya ulevi. You have different lifestyles, mnabaki mnashangaa tu! Angalau kipato kiruhusu kubadili mboga, na kuwa na quality family time, tutasonga tu. Kuna shosti aliacha kazi akafuata mume (wakati huo alinogewa na likizo ya maternity), baada ya kama miezi 8 hivi pamoja mume akafariki kwa ajali. She was happy kuwa walau wamekuwa na quality 8 months toka wamejuana!
Ahsante dada,

Hiki ndicho nimekuwa nikiongea wakati wote...Watu wanahangaika ila wanasahau kuwa safari moja huanzisha nyingine...Unapata pesa nyingi na hapo unaanza lust ya kutafuta nyingi zaidi.

Tunashindwa kujiuliiza, why mtu kama Bill Gates bado anafanyakazi??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom