Wengi Wafa Kwa Kunywa Kikombe Cha Babu Loliondo.

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
IDADI kubwa ya wagonjwa
waliokwenda kutafuta tiba
kwa Mchungaji mstaafu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Ambilikile
Mwaisapile, Loliondo wamepoteza maisha. Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii ambayo sasa itatangaza
matokeo ya utafiti wa tiba hiyo
ya ‘Kikombe cha Babu’
imesema wengi ni wale wenye
Ukimwi walioacha matumizi ya dawa za kurefusha maisha
(ARVs). Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Regina Kikuli, aliiambia
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC) jana
Dar es Salaam, kwamba hadi sasa Serikali inafanyia utafiti
watu 206 ambao walipata
kikombe hicho. Utafiti unaofanywa na Wizara
hiyo inataka kubaini kama
kweli dawa hiyo ina uwezo wa
kuponya Ukimwi, kisukari,
saratani na magonjwa
mengine sugu. Wanaofanyiwa utafiti huo walipata ‘kikombe’
hicho baada ya kuugua
kisukari na Ukimwi. “Kwa sasa ni vigumu kusema
dawa hiyo inaponya au
haiponyi, tusubiri utafiti wa
kitaalamu. “Baada ya miezi
miwili tutatangaza matokeo
kwa umma,” alisema Kikuli na kuongeza kuwa utafiti huo
unafanywa katika hospitali
mbalimbali nchini chini ya
usimamizi wa Taasisi ya Utafiti
wa Magonjwa ya Binadamu
(NIMR). Utafiti huo unafanywa katika
hospitali za Bugando, Mwanza;
Mbeya; Mount Meru, Arusha;
Hydom, Manyara na KCMC,
Kilimanjaro. Hospitali hizo ziko
maeneo ambayo wananchi wengi walijitokeza kupata
‘kikombe’ Loliondo. Kikuli pia
alisema kwa sasa idadi ya
Watanzania wanaokwenda
Loliondo kupata tiba hiyo
imepungua; lakini bado wananchi wa kutoka Kenya na
nchi zingine wanaendelea
kwenda kupata ‘kikombe’
hicho. Hata hivyo, Kaimu Mganga
Mkuu wa Serikali, Donan
Mmbando, alikiri kuwa
wagonjwa wengi wa Ukimwi
waliokwenda kupata tiba hiyo
na kuachana na ARVs wamepoteza maisha. Mbunge
wa Nkasi, Ali Kessy Mohamed
(CCM), aliishauri Wizara hiyo
kuacha siasa badala yake
iwaambie wananchi kwamba
dawa ya Babu wa Loliondo haina madhara kwa binadamu,
lakini pia haina uwezo wa
kuponya magonjwa. “Msiogope kusema kama
wanasiasa, ninyi ni wataalamu,
ni kweli kuwa ile dawa haina
madhara kama yalivyo maji,
lakini tusidanganyane, haitibu,
kwa nini mnaendelea kudanganya wananchi?” Alihoji
Mbunge huyo. Makamu
Mwenyekiti wa PAC, Zainab
Vullu, ndiye aliyetaka Wizara
itoe taarifa ya utafiti wa tiba
ya ‘kikombe cha Babu’. Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
John Cheyo, alitaka kujua kama
bado kuna idadi kubwa ya
Watanzania wanaokwenda
kupata tiba hiyo Loliondo.
Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola, alitaka kujua
kama Wizara hiyo
imewasiliana na nchi zingine
za Ulaya ambazo raia wake
walikwenda kupata tiba ya
‘kikombe’ kama walipona magonjwa waliyokuwanayo. “Wenzetu wale Wazungu ni
wepesi katika masuala haya ya
utafiti, nataka kujua kama
mmefanya juhudi za
kuwasiliana nao?” Alihoji
mbunge huyo na kujibiwa na Kaimu Mganga Mkuu kuwa kila
nchi ina utaratibu wake wa
utafiti
 
Mmeanza!
Wa kufa ni wa kufa tu, hata asingepata kikombe!!
Dawa ya Babu imeponya watu wengi mno, na kwa taarifa yenu ni kwamba hadi leo hii kuna watu wanaenda kumpelekea Babu zawadi baada ya kusalimika na kifo!
 
Mmeanza!
Wa kufa ni wa kufa tu, hata asingepata kikombe!!
Dawa ya Babu imeponya watu wengi mno, na kwa taarifa yenu ni kwamba hadi leo hii kuna watu wanaenda kumpelekea Babu zawadi baada ya kusalimika na kifo!


Mi ninawashuhudia wengi waliokwenda na kupata kikombe mtaani kwangu na leo wako gado balaa!

Pj!
Nakuunga mkono ya kwmb wa kufa ni wa kufa tu!
 
Mmeanza!
Wa kufa ni wa kufa tu, hata asingepata kikombe!!
Dawa ya Babu imeponya watu wengi mno, na kwa taarifa yenu ni kwamba hadi leo hii kuna watu wanaenda kumpelekea Babu zawadi baada ya kusalimika na kifo!

mmmh, ngumu kumesa..!
 
Kikombe cha babu kikombe cha shetani!!!!!!!!! Janja ya ccm imekufa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom