Sote tunajua kuwa hiyo ni janja ya CCM kwani wanavyuo wengi wanasupport upinzani. Lakini cha kujiuliza ni kwamba mbona miaka yote wakati wa uchaguzi vyuo vinakuwa vimefunguliwa? kwa nini sasa vifungwe?mimi nahisi hiyo yote njama ya CCM wanajua tukirudi chuo kabla ya uchaguzi majimbo yatachukuliwa na chadema.
leo kwenye gazeti la tanzania daima ukurasa wa 3 kulikuwa na picha ya viongozi wa tahiliso na kichwa cha habari tunadai haki yetu.
Iliandikwa kwa kifupi kuwa viongozi hao wa tahiliso walikuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari (maelezo) kuhusu madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kunyimwa haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Hata hivyo hakukuwa na maelezo zaidi.
Naomba wanajamvi wenye habari zaidi watujulishe hapa.
This can happen Only in Tanzania! Watu karibuni 60,000 wajiandikishe kisha wanyimwe haki yao ya msingi ya kupiga kura wakiwa ndani ya nchi yao wenyewe! 60,000???
Akina Marando, Ananilea Nkya na watetezi wengine wa haki za Binadamu Mko wapi Jamani????