Wema sepetu aharibika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125


Ilikuwa ‘lokesheni' katika moja ya nyumba maarufu za ‘shuuting' huko Mbezi-Beach, jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo Wema alibambwa na Kamera ya Ijumaa akiwa na donda katika goti la mguu wake wa kulia.

Baada ya kuona jereha hilo, king'ora cha ubongo wa Paparazi Wetu kilianza kugonga kutaka kujua kulikoni.

Mbali na kidonda, upekuzi wa ‘bodi' la mnyange huyo anayeongoza kwa kufanya vichwa vya habari za mastaa ‘town', ulionesha baadhi ya maeneo ya mwili wake yakiwa ‘full' mistari miekundu na hivyo kupoteza mvuto uleee!

Ilibidi kuanza kuhoji kilichosababisha mrembo huyo kuharibika ngozi yake nyororo, ambapo katika nusanusa ya hapa na pale, mmoja wa mastaa wenzake ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, alilinong'oneza Ijumaa kwamba, mabadiliko ya ngozi ni jambo la kawaida linaloweza kuwatokea baadhi ya wanawake lakini hustawi zaidi baada ya matumizi ‘tuumachi' ya vipodozi.




"Mabadiliko ya ngozi hasa kuwa na michirizi na wakati mwingine mistari, siyo ishu kubwa kwa baadhi ya wanawake, lakini inaweza kuwa ishu endapo vipodozi hivyo vitakuwa too much," alisema staa huyo aliyekiri kuwa, hata yeye alishangaa alipomwona Wema akiwa na michirizi kibao mwilini.

Ilibidi Ijumaa liongee na mtaalamu wake wa masuala ya afya ya ngozi ambaye alibainisha kwamba, kupasuka kwa ngozi na kuwa na mistari miekundu (scrabs) kwa wanawake kunaweza kusababishwa na mambo makuu mawili.

Mtaalamu huyo aliyataja mambo hayo kuwa ni unene na matumizi ya vipodozi kama vile ‘carolight' yenye kemikali za ‘hydroquine' zinazosababisha madhara makubwa kwa ngozi ya binadamu.

Alisema kwa mwanamke ambaye si mnene lakini akatoka michirizi hiyo, mara nyingi ni matumizi ya vipodozi vyenye kemikali.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumsaka Wema kupitia kilongalonga chake ili aeleze kidonda hicho kilisababishwa na nini, hakuweza kupatikana.

http://www.globalpublisherstz.com/2009/09/18/wema_sepetu_aharibika.html
 
St. John Chrysostom alisema kwamba uzuri wa mwanamke siyo kwamba atumie vipodozi. Mwanamke kama huyu Wema,atapendwa zaidi na wanaume kama akiwa na afya,kama akicheza netball. Kwa sababu kama unataka kutumia pincer,unachohitaji ni iwe inaweza kubana vitu vizuri,na siyo iwe imerembwa.
 
Aisee, inatisha hali hiyo ingawa naskia naye alitumia sana vipodozi vya kichina vya kunenepeshea mambo fulani.
 
Madhara ya mizigo toka China ndo hii sasa.
Ila mrembo katumika mno nahisi itakuwa imechangia vipodozi kugonga mwamba
 
hilo donda litakuwa ni la tukutuku tu

yes ila mbona karibia miguu yote ina mikwaruzo si bora angevaa hata suluari jamani kuliko kuweka pozi wakati kaharibika?

Au ni kidonda bandia kwa kuwa alikuwa anaigiza?ila kweli ameharibika Madhara ya mbwia unga Jumbe
 

mbonea mie nashangaa sana sijui huyo mtoto katumia mkorogo au hayo madawa ya kichina wanayosema hapo juu ,mungu anawaumba kwa uzuri kama tausi ila wanamkosoa
au kaligombana haka kadada kakadundwa maana nako mmh
 
Mhh athari za vipodozi miguuni na sio usoni? mbona kama athari za madawa ya kulevya?
 
Why didn't she wear pants to cover up whatever that is...
 
Bado sasa maana watu wengine wataka mpka uso waou uwe kama wa nyani vile na nyuma kuwa kukubwa ndio faida ya kazi toka China, Pole Wema Sepetu
 
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumsaka Wema kupitia kilongalonga chake ili aeleze kidonda hicho kilisababishwa na nini, hakuweza kupatikana.


hawa wadaku bwana,wameweza kumpiga mpaka picha,alafu wanasema juhudi za kumtafuta zimeshindikana....wangemuuliza aliyewapa picha...
 
uzuri mwengine una gharama nzito

sasa kuna uwezekano wowote wakumsaidia ili ngozi yake irudi ktk hali ya kawaida
 
Wema ni mweupe wa asili, anaongeza nini tena jamani?? Huo weupe wake wa asili aliokuwa nao hautoshi?? Kwa nini wadada twapenda kutumia mikorogo na madawa makali ya kubadilisha rangi ya ngozi?? Labda niulize swali moja kwani ukiwa mweusi unakuwa mbaya?
 
Back
Top Bottom