Wema Sepetu adai kuwa "hana mpango wa kuolewa na mtanzania"

fabinyo

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,991
2,109
[h=3][/h]



MSANII wa tasnia ya filamu bongo, Wema Sepetu, amefunguka kuwa hawezi kuolewa Tanzania kwani hata akiamua kuchukua maamuzi hayo bado kuna watu wanaweza kumuharibia ndoa yake kwa sababu zao binafsi.

Msanii huyo alidai kuwa hawezi kuacha kuzungumza ukweli kwani watu hawapendi maisha yake na ndiyo maana kila siku hawaishiwi cha kusema juu yake na hata mahusiano yake ya kimapenzi.

Alidai kuwa kutokana na kuandamwa na skendo kadhaa wanaume wengi wanamini yeye ni mwanamke muhuni, na ndiyo maana hakuna anayetaka kumchumbia, hivyo anaamini hawezi kuvishwa pete na mwanaume wa kitanzania kwani tayari wameshalishwa maneno machafu juu yake.

“Unajua wapo watu ambao kazi yao ni kunichafua na hawapendi maendeleo yangu, na kwangu mimi naamini hata kama nikisema nataka kuolewa kuna watu watafanya juu na chini ili tu ndoa yangu isifungwe, hivyo naweza kufunga ndoa na mwanaume wa nchi za nje kwani hata mi mwenyewe sitaki wabongo,” alidai.

Mwandishi wetu alipotaka kujua mahusiano yake na Diamond mwisho wake utakuwa vipi, alijibu “Suala la mimi na Diamond halihusiani na ishu yangu ya kufunga ndoa na mwanaume wa nje kwani najua Diamond hawezi kuishi na mimi kwa sababu tayari naye anaanza kulishwa maneno kuwa anatembea na mwanamke mkubwa wakati miaka yangu ni midogo sana,” alidai.

Hata hivyo mtandao huo ulipotaka kujua kauli ya Diamond juu ya Wema anaposema kuwa hawezi kuolewa na mwanaume wa kibongo, simu yake haikuweza kupokelewa baada ya kuita kwa muda mrefu.


UNA MTAZAMO GANI JUU YA HABARI HII? TUPE MAONI YAKO,MLIOPO NJE MCHUMBA HUYO JAMAN
 
Hana jipya rafiki yake(snura) kamchana kamwambia kuna mambo anayofanya wema akiamua kuyaadithia hakuna mtu atakayemtamani,amesisitiza kwamba watu wanamuona wema kama mungu wakati yeye anasema wema ni wa kawaida sanaaaaaaa!
 
Ni kweli je ni kwanini hapa tunamuongelea vibaya msichama wa Kitanzania ambaye anatafuta maisha mema kwa yeye na familia yake. Ni lazima tuelewe watu wanakuwa wakubwa na kubadilika hivyo hatuwezi kuongelea historia tu za watu kila siku wakati tunajua watu wanabadilika na umri.Tuna utamaduni wakuweka viwango tofauti kwa wanawake wakati wanaume wanafanya uhuni wa hali ya juu na hatusemi chochote!. Kama ni uhuni wanaume ni wahuni mara 10 ya wanawake wa Tanzania hivyo tusianze kuongelea dada zetu wakati wanaume wenyewe ni washabiki wa uhuni!!!
 
Hiki kichangu nacho kimezidi. Nani kamwambia kuwa kuna mtu mwenye kutaka kumuoa? Nani aoe mtu ambaye ameishachakachuliwa kulhali na kila mtu? Je hii ni sizitaki mbichi hizi? Angalau angejitahidi kuuguza moyo wake baada ya kugundulika kuwa Diamond ameanza kukohoa sana kama dalili za kitu kibaya. Wema atulie aache papara na kupapatikia usupastaa uchwara. Who wants to marry a ***** binti yangu?
 
Hiki kichangu nacho kimezidi. Nani kamwambia kuwa kuna mtu mwenye kutaka kumuoa? Nani aoe mtu ambaye ameishachakachuliwa kulhali na kila mtu? Je hii ni sizitaki mbichi hizi? Angalau angejitahidi kuuguza moyo wake baada ya kugundulika kuwa Diamond ameanza kukohoa sana kama dalili za kitu kibaya. Wema atulie aache papara na kupapatikia usupastaa uchwara. Who wants to marry a ***** binti yangu?

duh,taratibu,punguza jazba hahhaa!lol,lakini kweli
 
So called ''Bongo celebrities'' lacking PR skills or PR strategeies to sell themselves as a result they think negative publicity helps in upgrading their so called 'called celebrity status'!. Yagghhh! Disgusting!
 
Ninachompendea Wema ana akili sana huyu mtoto, anajijua hakuna Mtanzania anayeweza kweli kumuoa, wanafanya ni kummega na kumuacha maana hana hadhi ya kuolewa kwa uchafu alionao. Wa nje hawajui hilo ndio maana nae anawataka wa nje wasiomjua
 
kwani hao mabwana anaotembea nao tunawajuaje?si ni yeye mwenyewe anajitangazia,akiwa na bwana anataka kila mtu ajue,kwa hiyo watu hawamuharibii,anajiharibia mwenyewe!zile picha anazopiga nao na kuzitangaza mitandaoni?halafu ajue utandawazi sasa dunia ni kama kijiji,asidhani huko kwingine hawasomi taarifa zake,wanamjua.ye aamue kubadilika,waume wapo hata bongo!
 
Back
Top Bottom