Wema, diamond... Hakuna ndoa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
WEMA MTUMWA WA MAPENZI?
“Nahisi nimekuwa mtumwa wa mapenzi, utadhani nililetwa duniani kuteswa na mapenzi.
“Hebu fikiria leo ni siku ya nne Diamond hapokei simu wala hajibu sms, najua sina la kufanya, nimeamua kumwachia Mungu kwa sababu mwenzangu anamsikiliza zaidi mama yake.

“Diamond anajua fika kuwa mama mkwe wangu ananichukia na kila siku ananichachamalia niachane na mwanaye, nimeamua kunyanyua mikono juu na kumshukuru muumba kwa hapa tulipofikia kwani sina jinsi.
“Najua jamii itaniona mkorofi na sistahili kuwa mke wa mtu, lakini ukweli mimi si mkorofi na nampenda Diamond kwa dhati,” alisema.

ETI PANDE ZOTE MBILI HAZITAKI NDOA
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa wakwe wa pande zote mbili hawataki kuona ndoa hiyo inafungwa, wanawachukulia wapenzi hao wanafanya mambo yao kujifurahisha tu na kwamba
 
IKIWA ni takribani wiki mbili tangu mwanamuziki Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond' alipomvisha pete ya uchumba ‘shugamami' wake Wema Isaac Sepetu, visa vimeanza ambapo habari zilizoenea kitaani zinadai kuwa ndoa ya wawili hao imebaki stori kwani kuna uwezekano isiwepo, Risasi Mchanganyiko lina maelezo kamili.

Akizungumza ‘exclusively' na vuvuzela wetu juzikati jijini Dar es Salaam akiomba ushauri afanye nini ili kunusuru uchumba wake huku akitoa sauti iliyoambata na kwikwi kama anayeomboleza msiba, Wema alifunguka kuwa kinachofanya achanganyikiwe na kuwa katika wakati mgumu ni kutokana na mama mzazi wa Diamond, Sandra Sammy ambaye anahisi anamchukia.

"Nilipoanza mapenzi na Diamond nilikuwa naelewana sana na mama yake, lakini sijui nini kimetokea kwani naona kama amebadilika.

UVUMILIVU WATAKA KUMSHINDA WEMA
"Binafsi naona kama uvumilivu unataka kunishinda. Yaani hadi hapa nimeshakata tamaa ya ndoa kutokana na maisha kutawaliwa na ‘timbwilitimbwili' za hapa na pale," alisema Wema.

Mnyange huyo alisema hivi karibuni waliitwa Zanzibar na baba yake mzazi kwa ajili ya utambulisho rasmi na kuweka mipango ya ndoa sawa lakini kwa jinsi anavyoona hakuna kitu kama hicho kwani kila akimpigia simu mchumba wake huyo haipokelewi na hata akituma ujumbe mfupi ‘sms' hazijibiwi
 
Hii ni kwa wale wanwake woteeeeeeeee wanaotarajia kuolewa

ukiwa kama mwanamke ukakubali kujiachia na wanaume kujaribu kupima urefu wa uume wao kwenye
uchi wako nakwambia ndoa itabaki simulizi..nasema hivi hata kama umeweza kumhadaa mwanaume
akaingia mkenge nakwambia ipo tyme ataruka manyanga ...na ndio maana nakumbushia wanawake msikubali
wanaume tuwafanye kama uwanja wa bibi kwenda kupima ukubwa wa uume zetu hizi ni kashfa ambazo mwishso wa
siku waliopita wengi watabki kukukaribisha kwenye ndoa zao......UNYWE ULE UENDE CHOONI WENZIO WANAANZISHA MAISHA MAPYA
 
Unalo hilo mama, rekebisha tabia yako, achana na skendo, unadahani mama mkwe wako hayaoni magazeti wala hajui kusoma? Mnaona raha kuandikwa kwenye magazeti na kujitangaza ovyo kwenye mitandao eeh? haya ndo matokeo yake sasa...
 
Haya ni maneno ya wanadamu tu ambayo hayana gerentii yoyote km ni mapngo wa mungu kwamba hawa watu watakuwa mme na mke basi hata km wataachana kbs na kila mtu kuoa au kuolwa na mtu mwingine wakati wao wa kuwa pamoja ukifika lzm watarudiana na kuoana na mpango wa mungu kutimia na kama sio mpango wa mungu hata km watafunga ndoa siku ikifika wataachana na kila mtu ataenda kukutana na wake aliyepangiwa na mungu kuwa naye maishani.
 
[FONT=Georgia,"Times New Roman",serif]Ikiwa ni takribani wiki mbili tangu mwanamuziki Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ alipomvisha pete ya uchumba ‘mpenzi’ wake Wema Isaac Sepetu, visa vimeanza ambapo habari zilizoenea kitaani zinadai kuwa ndoa ya wawili hao imebaki stori kwani kuna uwezekano isiwepo[/FONT]


[FONT=Georgia,"Times New Roman",serif] Akizungumza na MPEKUZI wetu huku akitoa sauti iliyoambata na kwikwi kama anayeomboleza msiba, Wema alifunguka kuwa kinachofanya achanganyikiwe na kuwa katika wakati mgumu ni kutokana na mama mzazi wa Diamond, Sandra Sammy ambaye anahisi anamchukia.[/FONT]


[FONT=Georgia,"Times New Roman",serif]“Diamond anajua fika kuwa mama mkwe wangu ananichukia na kila siku ananichachamalia niachane na mwanaye, nimeamua kunyanyua mikono juu na kumshukuru muumba kwa hapa tulipofikia kwani sina jinsi.[/FONT] ALISEMA WEMA SEPETU HUKU MACHO YAKE YAKIJAA MACHOZI


CHANZO: <<KIPO HAPA>>


SINA MAANA YA KUMTETEA DIAMOND AU WEMA SEPETU. TATIZO LINALOTUPONZA NI KUWA SIKU HIZI TUMEYAGEUZA MAPENZI KUWA

"GAZETI" KWA MAANA YA KWAMBA,LEO ATASOMA HUYU NA KESHO MWINGINE!!!!!!

PENGINE NI KWELI KABISA WEMA KAMPENDA MSHIKAJI.MI NADHANI MAPITO YAKE NDO YATAKAYO MPONZA MAISHANI MWAKE

LAKINI PAMOJA NA HAYO,JE KWANI DIAMOND HAKUMJUA WEMA HATA KABLA HAJAMVISHA PETE?
 
Natoa tamko: Wewe!! .. Mambo wa watu waachie wenyewe.. Mpekuzipekuzi tu.. Sukununu flan.. Mind mambo yako bwanaa.. Inakera.. All days kuongelea inshu za vitandani mwa wenzenu.. Shit?
 
Kama ni kitu ambacho wazazi wa Wema watajutia ni kumruhusu ashiriki shindano la Miss TZ,Wema kwa wanaomjua alikuwa mtoto safi,muadilifu,mcha Mungu,hanywi,hadoo,n.k lakini baada tu ya kushiriki akazaliwa wema mpya kabisa na hili ndo linaloumiza wazazi kama si miss tz huenda saa hz wema angekuwa mbali sana na hata kuwa na familia yake siku nyiiiinguii!!
 
Kama Mungu ameandika hakuna atakae pinga si mkwe wala shemeji,awe na skendo kuliko za maraisi sikuikifika ataolewa tuu.
 
Pdidy, ingekuwa Wema (mwanamke) kamkataa Diamond (mwanaume) ungetoa ushauri gani kwa wanaume?

Au ungewageukia wazazi kwa kuwaamulia maisha watoto zao? Huyo Diamond alikuwa virgin before Wema?

Anyway ningesema mengi lkn naona inatosha haya!
 
Na Shakoor Jongo

IKIWA ni takribani wiki mbili tangu mwanamuziki Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ alipomvisha pete ya uchumba ‘shugamami’ wake Wema Isaac Sepetu, visa vimeanza ambapo habari zilizoenea kitaani zinadai kuwa ndoa ya wawili hao imebaki stori kwani kuna uwezekano isiwepo, Risasi Mchanganyiko lina maelezo kamili.
Akizungumza ‘exclusively’ na vuvuzela wetu juzikati jijini Dar es Salaam akiomba ushauri afanye nini ili kunusuru uchumba wake huku akitoa sauti iliyoambata na kwikwi kama anayeomboleza msiba, Wema alifunguka kuwa kinachofanya achanganyikiwe na kuwa katika wakati mgumu ni kutokana na mama mzazi wa Diamond, Sandra Sammy ambaye anahisi anamchukia.

“Nilipoanza mapenzi na Diamond nilikuwa naelewana sana na mama yake, lakini sijui nini kimetokea kwani naona kama amebadilika.
UVUMILIVU WATAKA KUMSHINDA WEMA
“Binafsi naona kama uvumilivu unataka kunishinda. Yaani hadi hapa nimeshakata tamaa ya ndoa kutokana na maisha kutawaliwa na ‘timbwilitimbwili’ za hapa na pale,” alisema Wema.

Mnyange huyo alisema hivi karibuni waliitwa Zanzibar na baba yake mzazi kwa ajili ya utambulisho rasmi na kuweka mipango ya ndoa sawa lakini kwa jinsi anavyoona hakuna kitu kama hicho kwani kila akimpigia simu mchumba wake huyo haipokelewi na hata akituma ujumbe mfupi ‘sms’ hazijibiwi.

WEMA MTUMWA WA MAPENZI?
“Nahisi nimekuwa mtumwa wa mapenzi, utadhani nililetwa duniani kuteswa na mapenzi.
“Hebu fikiria leo ni siku ya nne Diamond hapokei simu wala hajibu sms, najua sina la kufanya, nimeamua kumwachia Mungu kwa sababu mwenzangu anamsikiliza zaidi mama yake.

“Diamond anajua fika kuwa mama mkwe wangu ananichukia na kila siku ananichachamalia niachane na mwanaye, nimeamua kunyanyua mikono juu na kumshukuru muumba kwa hapa tulipofikia kwani sina jinsi.
“Najua jamii itaniona mkorofi na sistahili kuwa mke wa mtu, lakini ukweli mimi si mkorofi na nampenda Diamond kwa dhati,” alisema.

ETI PANDE ZOTE MBILI HAZITAKI NDOA
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa wakwe wa pande zote mbili hawataki kuona ndoa hiyo inafungwa, wanawachukulia wapenzi hao wanafanya mambo yao kujifurahisha tu na kwamba hawapo ‘siriasi’.

DIAMOND NA MAJIBU YA MKATO
Baada ya kusikia upande wa Wema, gazeti hili lilimtafuta Diamond ili kupata mzani wa habari hiyo ambapo staa huyo wa ngoma ya Moyo Wangu alitoa majibu ya mkato.

Risasi Mchanganyiko: Diamond harusi yako na Wema ni lini?
Diamond: Siku yoyote Mungu akipanga.

Risasi Mchanganyiko: Lakini kabla Mungu hajapanga, wewe unategemea itakuwa lini?
Diamond: Unajua mimi namuamini sana Mungu hivyo yeye ndiye anayejua.

Risasi Mchanganyiko: Kuna taarifa kuwa mama yako hampendi Wema, je, ni kweli?
Diamond: Sijui chochote.

Risasi Mchanganyiko: Pia inadaiwa kuwa hata mama yake Wema hataki umuoe Wema, je, hili likoje?
Diamond: Sijui chochote mimi nasikia tu maneno ya mtaani.

Risasi Mchanganyiko: Inadaiwa kuwa leo ni siku ya nne hupokei simu wala kujibu sms za Wema, je ni kweli?
Diamond: Siyo kweli.

Risasi Mchanganyiko: Nimemaliza kuzungumza na Wema sasa hivi (Jumatatu saa 4:00 asubuhi) anasema una siku ya nne hupokei simu yake wala kujibu meseji zake?
Diamond: Mimi namuamini sana Mungu ndiyo maana naswali sana.

Risasi Mchanganyiko: Hilo la kuswali sana limetokea wapi? Naomba ujibu swali uliloulizwa!
Diamond: Unajua mimi nafanya kazi sana, hivi sasa natokea Ifakara (Morogoro) kufanya shoo.

Risasi Mchanganyiko: Kwa hiyo kufanya kwako kazi nyingi ndiyo kunakokufanya usiwasiliane na mchumba wako?
Diamond: Unajua mimi niko ‘bize’ sana.
Hali hii iliendelea hadi mwisho ambapo Diamond hakuwa tayari kuzungumzia ishu hiyo kiundani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom