Well, hata naogopa kuuliza!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Mali za vigogo sasa zaanza kukamatwa
::Ni wale waliokopa Mfuko wa Pembejeo

na mwandishi wetu (Mtanzania)

SERIKALI imeanza kukamata na kuuza mali za wadaiwa sugu waliokopa mabilioni ya shilingi kutoka kwenye Mfuko wa Pembejeo wa Taifa. (it sounds like mfuko wa NSSF)

Hatua hiyo imekuja baada ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, kupitia Mfuko huo, kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari, ukitaka marejesho ya fedha hizo yafanywe haraka.

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. David Mathayo, alizungumza na MTANZANIA jana na kuthibitisha kuwapo kwa operesheni kali ya urejeshwaji wa fedha hizo.

Dk. Mathayo alisema wadaiwa wameanza kuonyesha ari kubwa ya kurejesha mikopo hiyo ambayo inapaswa ilipwe ili wengine waweze kukopa. Zaidi ya Sh bilioni 2 ziko mikononi mwa wakopaji. (compared to 15 million)

Alisema mawakala wa kukusanya madeni hayo wameshapelekwa mikoani kote, kuwafuatilia wadaiwa.

“Mawakala wapo mikoani tayari, tunafurahi kuona kuwa wengi wameitikia wito wa kulipa madeni, kwa kweli hatutatulia hadi fedha hizo zirejeshwe.

“Tangu tangazo litolewe, hali imebadilika, lakini nakuhakikishia kuwa tunakusanya madeni hayo kistaarabu, mteja anayedaiwa, hutakiwa mwenyewe asema lini atamaliza kulipa deni, kauli yake inachukuliwa na kuandikwa kama commitment,” alisema. (of course, wengine wanaandikwa magazetini kwanza)

Alisema kuna mali kadhaa zimeshakamatwa, yakiwamo matrekta, na kwamba pale inapobidi, hupigwa mnada ili kuokoa kiasi cha fedha kinachodaiwa. “Matrekta tunayakamata, kadi zake tunazo, kwa hiyo wale wanaoshindwa kabisa, tunayapiga mnada, hatuna namna nyingine, isipokuwa kuhakikisha kwamba fedha zinarudi na kutumika kuwakopesha watu wengine waaminifu,” alisema Dk. Mathayo, na kuahidi kutoa taarifa zaidi kuanzia leo.

Uchunguzi unaonyesha kuwa miongoni mwa wadaiwa sugu ni wanasiasa na watu wenye “majina makubwa.”
(no that can be true!, kuna mwenye jina kubwa kuliko Mbowe?)

Mfuko wa Pembejeo, kwa miaka kadhaa umekuwa ukitumiwa kuchota fedha kupitia mikopo, lakini marejesho yameendelea kuwa mabaya.(say whaaaaaaaaaaaat!)

Mafanikio yanayoonekana sasa ni sehemu ya mkakati wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, katika kuitikia wito mapambano dhidi ya ufisadi.

My Take:
Magazeti ambayo yaliandika "Mbowe Aifilisi NSSF" wameshindwa kumtaja hata mtu mmoja aliyekopa mfuko wa Pembejeo na ambaye hajarudisha? Au hawajulikani?

Kwa vile wao wameshindwa nimejitolea kutumia resources zangu, kupata majina ya viongozi wote wanaodaiwa na mabenki, kampuni binafsi, mifuko ya fedha n.k ili warudishe fedha za Watanzania! Ni lazima tuwajue walikopa kiasi gani, wamerudisha kiasi gani, na kwanini wamechelewa kurudisha. Huu ni wakati wa uwazi!!
 
Hata huu utaitwa 'ufisadi'. Let's grow. Let's unite against ujinga wa wazi. Tuangalie taifa linaenda wapi na watu gani wanataka kutupotezea muda tusiwaguse.

Kuna nyingine mpya nimeisikia lakini naianzishia mada sasa hivi
 
Mmmmh, hapo ndipo ulipo utamu. Kila aliyekopa serikalini au katika mashirika ya umma bila kuonyesha dhamira ya kulipa mkopo huo lazima alazimishwe kulipa. Kama hiyo operation ni maalumu kwa ajili ya kumdhalilisha Mbowe sidhani kama itafanya kazi maana issue yake iko mahakamani. Haimati umekopa wapi cha msigi ni dhana yenyewe MKOPO WA SERIKALI, kwa maana hiyo hata wale waliojikopesha nyumba za serikali kwa bei nafuu lazima nao either warudishe hizo nyumba au walipe thamani halisi za hizo nyumba na hata magari. Mie binafsi nitajaribu kufuatilia kwa ukaribu hiyo operation nione kama watu ninaowafahamu waliochukuwa mikopo hiyo wakiwa bado ni vigogo serikalini wamerudisha. Na ningeshauri zoezi hilo kuwa la wazi zaidi maana michezo ya kujuana na waziri wa wizara husika unaweza ukajitokeza na deni lisilipwe vilevile. Mali ya serikali lazima irudishwe serikalini.
Naamini kuna watu wengine walikopa hizo fedha kwa nia nzuri ili kujiendeleza lakini wengine hawakukopa bali walichukuwa kutokana na loophole iliyoko ndani ya mashirika na serikali.
 
Back
Top Bottom