Wekeza wilaya mpya ya kilindi

MAKOLA

Member
Jun 5, 2010
46
16
E bwana nimefika kilindi wilaya mpya mkoa wa tanga, wilaya hii inaendelea kwa kasi ya ajabu nawashauri wajasiliamali wafike kuangalia opportunities, ardhi yao ni bomba mbaya wanalima na hawatumoii mbolea na wanavuna ile mbaya
viwanja vinapimwa bei yao inaanzia laki sita hadi milioni, wanatoa hati miliki bilalongolongo. Unaweza kutoka kimaisha kupitia hii wilaya,

wilaya haina guest ya ukweli
haina petrol station ya ukweli
haina duka lolote la hardware
hakuna duka lolote la ukweli ambalo linauza vitu vya ujumla
 
Asante sn mkuu, tutafika siku si nyingi kungalia mazingira ya uwekezaji.
 
Potentials ziko kwenye nini hasa? Kilimo au hata biashara? Vipi miundombinu? Wingi wa watu including wageni? Need to visit you one of these days.
 
Nini hali ya miundombinu na huduma nyinginezo huko? kuanzia barabara, maji, umeme, mitandao ya simu, internet n.k n.k
 
miundombinu ipo bomba watu wangu, maji yapo, umeme upo, biashara zinaenda, benki ipo japo ni NMB peke yake. hali ya hewa safi, wakazi ni wafugaji na wakulima.ukitaka kujua ukweli tuma email kwanzamen@yahoo.com
 
mashamba ekari moja laki 3 then kama kawa hawatumii mbolea, wanalima tumbaku kwa wingi, na ina fanya vizuri sokoni.
 
Hii safi...... na vipi kuhusu mashamba makubwa kama heka mia na kuendelea yanapatikana? Na bei zake zimekaa vipi?
 
mashamba ekari moja laki 3 then kama kawa hawatumii mbolea, wanalima tumbaku kwa wingi, na ina fanya vizuri sokoni.

Mkuu laki 3 kwa eka kwa Tanzania ya sasa ni ghali sana kwa mkulima. Sio ghali kwa wawekezaji wengine kama petrol station, guest house etc.
 
Big thx Makola.
Nakubaliana nawe sana Wilaya ya Kilindi ni pakuwekeza. Najua Kuna maeneo yana machibo ya dhahabu.
Hivyo baada ya muda mfupi mji utakuwa na pilika sana za kibiashara.
Kuna jamaa aliniambia Kuwa niwahi huko, nikaangalie cha kufanya kama ni kilimo au biashara.
 
e bwana shwari nitafute kwa email yangu. kwanzamen@yahoo.com wilaya hii bomba viwanja vipo vinauzwa na halmashauri ekari moja iliyopimwa laki 6-9.jamaa wa ardhi niliwauliza wakanambia hivyo. kuna dogo mmoja yupo ardhi nitamcheki pale wilayani then nikimhoji nitaweka javini mazungumzo
 
Umeenda Kilindi masika ukaona segere lake?
Utarudi Dar es Salaam kwa miguu, aikudanganye mtu.
Laki tatu heka bei za mjini hizo mnaoibiana elfu 15 unapata heka ya shamba zuri.
 
shamba heka laki3 ni wizi,makola,unafikiria kama mtu wa dar,ardhi dar in gharama kwa kuwa wahitaji ni wengi na pia sio kwa ajili ya kilimo,ardhi ya kilimo bei bado iko chini,takwimu zinaonyesha kuwa kilimo ni 35% ya matumizi ya ardhi tz,iliyobaki bado hijatumika kwa kilimo.UPO DUNIA IPI?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom