Sawa tuseme basi alishindwa kutengeneza hiyo website kwa sababu moja au nyingine. Wewe kama Mtanzania, huoni kuna sababu ukajitolea kutengeneza Website ya Ikulu, na itakufanya pia ujulikane zaidi ya Utanzania wako! Jitolee bwana usiwe kama hao walioshindwa kama unavyosema.
Dr.WHO, hizo website hapo hata moja sio ya Serikali.Muwe munaelewa mada inayoongelewa. Nilizungumzia kama Balozi XX mteule alishindwa kuanzisha Website, na kwa kuwa unaona kuwa na Website ni kitu muhimu sana kwa maisha ya Watanzania, basi ujitolee kuanzisha moja. Wewe ukapost a series of Jambo Forums.
Afadhali mwenzio WORM aliyejitolea kujenga Website ya Serikali bure na hataki ajulikane na anataka ajue amuone nani ili afanikishe. Kwa kuwa bado thread inaendelea, na kuna wajuzi wanaotoa hoja ya kusema bwana WORM asifanye kazi ya bure ya kujitolea, basi malizeni kwanza majadiliano, mtapofikia muafaka, kama kuna haja ya kujitolea, basi nitawashauri nani wa kumouna.
Kama sababu zenyewe zakuwa na website nikujitangaza bila shaka haihitajiki. Rais wetu anakwenda mwenyewe huko huko waliko hao watumiaji wa website na kuwaaambia ana kwa ana hayo mambo ambayo yangewekwa kwenye mtandao.YES Mwanakijiji,
Wanaodhani internet ni anasa wana-lag behind. Na ulivyojibu almost ndiyo majibu ya Mheshimiwa Lwama Papa! Lakini wajue kuitangaza nchi worldwide na hasa leo tukiwa tunaadhimisha uhuru wa vyombo vya habari ni pamoja na kutumia njia za mitandao na kuitangaza nchi kwa mazuri iliyo nayo.
Haya bana, mie nshakata tamaa!
Mzee Mwanakijiji, he umekuwa msemaji wa wOrM? Malizeni mjadala halafu mseme bayana msimamo kama kulipwa au bure? Ni lini mtatoa mchango nchini kwenu kama mmeamua kuishi kibepari kwa maana chochote kinachofanywa, kiwe na consideration? Hebu kumbukeni "Kijana aliyepewa chakula na Kijiji kilichokuwa na njaa, ili apate nguvu ya kwenda kutafuta chakula mbali arudi nacho kuwasaidia aliowaacha Kijijini kwake maana, wangekigawa pale Kijijini kisingewatosha na wasingefika huko kupata chakula kingine- Kijana akala akashiba akaenda na akapata hicho chakula alichikifuata, badala ya kukirudisha Kijijini kwa wengi aliowaacha na njaa akaamua kubaki huku huko". Sasa na nyie msiwe kama huyo kijana kwa kusingizia eti mmeamua kuishi Kibepari. Lazima mkumbuke mlikotoka!