Website katika bango la Chuo cha Takwimu (Eastern Africa Statistical Training Centre)

Sinkala

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
1,773
683
Jamaa hawa wa EASTC hawako serious. Chuo kile kina wanafunzi wengi wa kigeni kutoka South Africa, Zimbabwe, Zambia, Sudan na nchi nyingine zinazotuzunguka, na kina nafasi ya kuwavutia wanafunzi wa kigeni wengi zaidi kwa kupitia mtandao wa internet hivyo kuwekeza fedha za wageni humu nchini, na ni vizuri website yake ikawa na maelezo sahihi. Katika address za internet, kosa katika herufi au tarakimu moja linasababisha ufungue kitu kingine kabisa au usipate unachotaka. Sasa hapa jamaa wa EASTC wameweka website ambayo TLD yake inasomeka .as badala ya .ac , ambayo ni country-code top-level domain designated for American Samoa. Cha ajabu pande zote mbili za bango kuna kosa hilo hilo! Sasa sijui huwa hawaoni au wamekosa washauri! Nimeweka picha ya bango na kuonyesha kosa lao kwa mshale mwekundu. Biashara ni matangazo, sasa kama matangazo yenyewe ndo haya, hatutafika !

sinkala-albums-sinkala-picture658-eastc3.jpg
 
Last edited:
Back
Top Bottom