We need facts mgao unaisha lini?

Micho

JF-Expert Member
Apr 12, 2009
1,122
1,246
Jamani wasomi, wafanyakazi serikalini na wadau wote kwa ujumla..kama kuna mtu yupo karibu na decision makers wa nchi hii....ebu mtujuze Mgao unaisha lini maana hata juzi sikumpata vizuri mkuu wetu alikuwa anasema nini alipotembelea wizara ya Nishati na Madini kuhusu mgao......
 
mgao utaisha 2014 ili wajiandae na kampeni za uchaguzi wa 2015 huku wakisema mnaona sasa tatizo la umeme tumelipatia ufumbuzi wakipata tena unaendelea
 
Kwa mujibu wa katibu mkuu nishati na madini makali kupungua baada ya serikali kutoa hela ya mafuta kwa ajili ya mitambo ya IPTL wameongeza uzalishaji toka 10MW hadi 80MW

Hela ya mafuta imetoka kutokana na pendekezo/ shinikizo la kamati ya makamba!!!
 
Jamani wasomi, wafanyakazi serikalini na wadau wote kwa ujumla..kama kuna mtu yupo karibu na decision makers wa nchi hii....ebu mtujuze Mgao unaisha lini maana hata juzi sikumpata vizuri mkuu wetu alikuwa anasema nini alipotembelea wizara ya Nishati na Madini kuhusu mgao......
Mkuu.
Decision makers wameshahama katika kutatua tatizo la umeme.Hili litajitatua wenyewe kwa "uwezo wa mungu". serikali haina suluhisho zaidi ya mitambo ya Dowans, Songas na Kiwira.

Sasa wamehamia katika ahadi ya reli ya kisasa ya kimataifa ambayo haijawahi kuwepo duniani... na viwanja vya ndege vya kimataifa katika kila kijiji...

Kuna wakati meneja wa bonde la rufiji alisema TZ na Brazil watajenga dam na kuzalisha umeme ambao utaondoa tatizo la umeme. Sasa sijui huu mradi umefikia wapi.. na sijui kama wale wakorea wameshaanza kulima mpunga huko.

Mkuu watu hawataki kutatua matatizo, watu wanataka 10% tu. Halafu utawasikia wanasema tatizo hili litakuwa ni historia....usisahau kuna msemo usemao wa kuwa historia hujirudia.
Ni vyema ukajitayarisha kwa maumivu ya muda mrefu.
 
Jamani wasomi, wafanyakazi serikalini na wadau wote kwa ujumla..kama kuna mtu yupo karibu na decision makers wa nchi hii....ebu mtujuze Mgao unaisha lini maana hata juzi sikumpata vizuri mkuu wetu alikuwa anasema nini alipotembelea wizara ya Nishati na Madini kuhusu mgao......

unataka kujua mgao unaisha lini? kwani wewe ni mgeni Tanzania? kama ni mgeni basi mgao utaisha leo na utaanza tena kesho
 
ccm itakapoondoka madarakani mgao utaisha!maana wao wanawaza mitambo ya kukodisha tuu
 
Mgao wa umeme Tanzania utaisha mara tu baada ya kukiondoa madarakani Chama Cha Mafisadi/Majambazi.
 
mgao utaisha wakisha fanya mikataba yao ama sivyo inabidi ukawaombe wake zao wawabembeleze waume zao, lakini najua wataambiwa hizo hereni za dhahabu nk zinatoka wapi si mpaka tupate pesa za kusaini mkataba au tuwekeze kwenye umeme
 
kwa mfano sasa baada ya kashi kashi za maandamano na kuwekwa wazi wamiliki halali/haramu wa dowans mwenye nchi kaamka usingizi wa miaka sita anasema tuwe waangalifu wa richmond nyingine, hapo hapo mgao umepungua kwa sasa maeneo yetu
 
Mgao utaisha pale tu CCM itaondoka madarakani,otherwise tutaendelea kuingia katika giza la ajabu sana
 
Back
Top Bottom