We are good pretenders, good disguisers, good puppets of leadership

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Kwa takribani muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia thread mbalimbali humu Jf. Baada ya kutafakari kwa muda mrefu juu ya mambo mbalimbali kuhusu harakati zetu sisi watanzania nimekuja kutambua kwamba tuna matatizo makubwa sana kama taifa. Lakini moja ya jambo nililojifunza ni kwamba: WE ARE GOOD PRETENDERS, GOOD DISGUISERS, GOOD PUPPETS OF LEADERSHIP AND GOOD FOLLOWERS BUT VERY BAD LEARNERS.

Lakini hoja ya msingi hapa ni kwamba mfumo mzima wa elimu hapa Tanzania hautufanyi kuwa na hazina kubwa ya vijana ambao ni GREAT THINKERS kwa maana ya kutambua mahitaji ya nyakati. Our minds ziko configured na zinatumia hizi configuration za kimagharibi. Nimewahi kuona mitihani ya wanafunzi wa UDOM ya kuchagua A,B,C katika mtindo huu sidhani kama tunaweza kupata vijana ambao wanaweza kudevelop intellectual and moral ideas ambazo zina tija katika kujenga taifa letu zaidi ya ku "copy" and "paste" ideas za kina Marx, Nurkse n.k. Tumenakili mfumo wa kingereza kwenye mfumo wa elimu yetu ambao haumjengi kijana wa kitanzania kuweza kulitumikia taifa kwa ufanisi badale yake kuwatumikia wenzetu wa nchi za kimagharibi. Waingereza wanaanza kuwa "configure" vijana wetu kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu ni hivyo kufuata configaration za kiingereza badala ya kitanzania.

Lakini vilevile tuna viongozi ambao ni "Idealistic" na sio "realists" kutokana na kuwa na jamii dhaifu ambayo haina utamaduni wa kupata habari kwa maana ya kupata maarifa.

The foundation of knowlerge is information na ili uwe na skills lazima uwe na knowlerge, wakati jamii za wenzetu zikihubiri mipango ya kiuchumi na kiteknolojia sisi tunaendekeza majungu ya udini na ukabila katika harakati zetu za kisiasa. Tumeendekeza siasa za majungu badala ya mipango yenye tija na hapa namaanisha practicable plans sio nadharia za mipango. Tuna BBC Leaders(Born Before Computers) ambao hata hiyo teknolojia ninayoongea imepita pembeni.

LACK OF VISION. Fikra za baadhi ya viongozi wetu zimeelekezwa kwenye misaada lakini cha kushangaza zaidi hata hao wanaotupa misaada wanashangaa inakwenda wapi? Wanachoshindwa kutambua kwa dhati viongozi wetu ni kwamba dunia ipo kwenye riadha, ni mashindano yasiofuata taratibu, ni mashindano yaliyojaa rafu na bila kuwa na viongozi wenye upeo na maono taifa litaangamia. Viongozi wengi wa Tanzania wamezoea kuimba na kujisifia kuwa tuna rasilimali nyingi mithili ya vijana wa bongofleva wanaojisifia na kujifanya ni wanamuziki kumbe ni waimbaji.

Mwanamuziki hutumia midundo halisi kupiga muziki wake na ndivyo ilivyo kwa viongozi makini wanaotumia fikra pevu na busara kujenga Tafa lao bila kutegemea midundo ya kibeberu. Rasilimali hazina maana kama hazitumiki ipasavyo kwa maendeleo ya wazalendo. Ni sawa na mkichaa anayekufa kwa kiu wakati yupo kwenye maji mengi.

Tumedhihirisha msemo wa wahanga kwamba “Kwenye miti mingi hakuna wajenzi”, viongozi wetu wa kisiasa wanapenda kutukuzwa kwa kile wanachikiita “tumepiga hatua kubwa sana” kwa sababu wanaamini wananchi hawana habari juu ya yale wanayoyaita maendeleo makubwa kwa kuwa hawana utamaduni wa kutafuta habari kwa ajili ya kupata maarifa ya wenzetu duniani. Kwa kuwa wao wamekula basi wanajua kila mtu amekula.

Kutambua ukweli ndio njia ya kuamsha fikra na kuamini matendo chanya, kukubali ukweli wa maisha na kupambana kubadilika kuelekea kwenye mafanikio zaidi. Wakati tunaelekea kusherekea miaka hamsini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuelekea miaka mingine hamsini ya Tanganyika lazima kwanza tukiri tuna matatizo makubwa na sio changamoto na kubatiza taifa letu upya na kupata viongozi wenye upeo, maono na uadilifu. Taifa letu linahitaji fikra za mabadiliko kuanzia kung’oa mfumo wa utawala unaolinda mafisadi kuelekea fikra za uzalendo zinazong’a dhulma za uaribifu wa mali za umma, uhuru ulio huru unaozingatia haki za raia kulinda tunu za taifa ikiwepo uzalendo na uwajibikaji, kueneza fikra na njia mwafaka zenye tija (practical and workable solutions) pamoja na kujenga jamii yenye filkra pana.


Nimedhamiria kuyaweka kwenye kijitabu yale ninayaofikiria ndani ya ubongo wangu kama silaha ya ukombozi . Hivyo baada ya kusoma maneno haya jiandae kupata kijitabu kutoka kwangu kwa maombi maalum kitachojulikana kwa jina "FIKRA ZA MABADILIKO". Kwa mahitaji nitumie maombi kupitia barua pepe: germa86@rocketmail.com
 
Asante sana kwa point zako!
Naona thread yako ilipitwa siku nyingi sana, but the beauty of the internet is that your words will live forever.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom