Wazushi mtandaoni. . .

Kigarama nilikua naifikiria hii ishu mapema kweli kwasababu nilishaona kipindi kile cha msiba Regia. . .
Ila hii ya YM kwakweli imezidi. Kuna wengine hata kama sio hapa hua wanasababisha wenzao wanapoteza kabisa kujiamini, na wale wadogo wadogo wanafikia hata kujiua.

Suicide teen Natasha MacBryde was bullied online even after her death | Metro.co.uk
Nimekisoma Lizzy kisa cha Natasha nakuishia kushangaa hii mitandao itatupeleka wapi. Watu wazima kama mimi huwa tunajua kudili na hisia zetu, lakini huwezi kujua nyuma hizi avatar ni mtu wa aina gani.

Mwingine anaanzisha mada ili ajifunze kutoka kwa wengine lakini mwisho wa siku anaishia kugeuzwa kituko. Natasha binti mdogo kabisa alikuwa, lakini alisongwa songwa hadi akajiu. "unajifanya wewe ni bomba na wanaume wote wanakuzimikia..." haya ni maneno ya watu dhaifu.
Mzee mmoja alinifunza kwamba watu dhaifu ni pamoja na Hittler kwani wanatumia sana mabavu kuwasilisha ujumbe wao kwa sababu hawajiamini!
 
prrrrrrrr!!hawana lolote hao lizzy,...sura zao kama avatar za watu fulani humu...nitonye, mphamvu na wengine wafananao na hao....
wangekua km preta cjui ingekuwaje!?!loh!!
Hahaahha. . kaaaaazi kweli kweli!!!
 
Humu mtandaoni mbona ni kama jadi kwa baadhi ya watu!
Wako watu hodari sana kuwakandia wenzao, wao michango yao ipo zaidi kuwaponda watu..mara kabila fulani hawana shape, mara fulani mbaya, mara fulani yuko hivi na vile.Unatamani umfuate umpige picha uje kuiweka humu ili achambuliwe vizuri!
Mara nyingi watu kama hawa wana matatizo - utakuta wao hawajiamini kwa lolote na hupata raha kuwaponda wengine kama njia ya kulipa kisasi! Huwa siku zote nasema, hakuna mtu aliyemuomba Mungu amuumbe alivyo.Unazaliwa unajikuta uko ulivyo na hata kama ni nini unafanya kujenga kile kilichopo kupitia elimu, kujipamba etc. Pia tabia njema huongeza haiba ya mtu.Kuwasema wengine vibaya hakukufanyi wewe ujenge haiba nzurI. Nadhani wahusika wamesikia na watajifunza.SHAME!
 
Nimekisoma Lizzy kisa cha Natasha nakuishia kushangaa hii mitandao itatupeleka wapi. Watu wazima kama mimi huwa tunajua kudili na hisia zetu, lakini huwezi kujua nyuma hizi avatar ni mtu wa aina gani.

Mwingine anaanzisha mada ili ajifunze kutoka kwa wengine lakini mwisho wa siku anaishia kugeuzwa kituko. Natasha binti mdogo kabisa alikuwa, lakini alisongwa songwa hadi akajiu. "unajifanya wewe ni bomba na wanaume wote wanakuzimikia..." haya ni maneno ya watu dhaifu.
Mzee mmoja alinifunza kwamba watu dhaifu ni pamoja na Hittler kwani wanatumia sana mabavu kuwasilisha ujumbe wao kwa sababu hawajiamini!

Inasikitisha ehhh!!!?
Sasa fikiria hata mdada tu ambae hajiamini amini alafu apate na watu wakumchamba na kumchambua hivyo kama hatofikia kutamani mauti. Yani watu wanawanyima wenzao raha kwa madhaifu yao wenyewe.

Huyo mzee ni mzee haswa. . . ndo kama hawa wanautimia maneno, wengine wanatumia mikono yani alimradi ajisahaulishe kuhusu udhaifu wake kwa kumuonea mtu mwingine.
 
Watu km hawa dawa ni kuwapotezea tu,
Kwan kwa namna yoyote huwa hawapunguzi au kuongezea chochote maishan,
Isitoshe labda ndio huwajui hawakujui wanajichosha tu kuumiza keybodi kwa kubonyeza kwa hasira,
Wengine wameubwa na vismat na bahati zao wala haihitajiki promo lol!

On top of that km mungu akiamua kukuweka juu hakuna wa kukushusha hata wakipita mitaani na spika kukuchafua,
Siku zote utakuwa juu tuu!!!
 
Yaani wamenishambulia hadi nimekosa raha! Hii dunia tabu tupu
Pole sana....lakini wewe umeyataka mwenyewe! kwanini uuze sura yako hku mtandaoni? Ulikuwa una nia gani kufanya hivyo?
Mimi nimeshawazoea kushambulia Avatar yangu...but i wish wangeniona live!!!
 
Uzoefu unanionesha kwamba kama unajiamini hutapoteza muda wako kuponda ama kukejeli watu wengine, halikadhalika kama unajiamini hutapoteza muda wako kufikiria critics za watu dhidi yako.. Use that confidence in you guys, and live your life. Coz life goes on anyway!
 
Mimi nipo kimpango wangu
sina time na mtu

We Smiley unajiamini ila kuna wengine hawawezi vumilia kwa muda mrefu. Watajikaza na kuvumilia ila eventually wanajikuta wameanza kukosa raha maishani.
 
Pole sana....lakini wewe umeyataka mwenyewe! kwanini uuze sura yako hku mtandaoni? Ulikuwa una nia gani kufanya hivyo?
Mimi nimeshawazoea kushambulia Avatar yangu...but i wish wangeniona live!!!
Hahaha. . . wangekuona mbona wangenuna bila sababu!!
 
Yaani wamenishambulia hadi nimekosa raha! Hii dunia tabu tupu

Huna sababu ya kukosa raha. Hata siku moja huwezi kuwafurahisha binadamu tena usiowafahamu. Watu wana uhuru wa kuandika chochote wanachojisikia kutegemeana na tabia zao au mazingira yanayowazunguka. Wengine wana- frustration zao. Cha maana simamia msimamo wako, jiamini na furahia siku zako za kuishi.
 
Uzoefu unanionesha kwamba kama unajiamini hutapoteza muda wako kuponda ama kukejeli watu wengine, halikadhalika kama unajiamini hutapoteza muda wako kufikiria critics za watu dhidi yako.. Use that confidence in you guys, and live your life. Coz life goes on anyway!

TANMO sio wote tumejaaliwa kuwa na confidence na tunatakiwa tuwasaidie wasiyonayo waipate angalau kidogo badala ya kuendelea kuwashusha.
 
Bora mm nazomea na ninawazomea haooooooooooooooooooooooooooooo
 
Come on Lizzy.....

Usiniambie uzi wa Young Master umekutouch namna hii mpaka umekuja kuufungulia thread...... Hii ni Chit Chat watu tunajiexpress tutakavyo. Hakuna anayeuza sura humu, Na wala mi siamini kama ile ni picha ya kweli ya YM.

Isitoshe kuna mashindano ya kuuza sura humu? Over My Dead Body!
 
we smiley unajiamini ila kuna wengine hawawezi vumilia kwa muda mrefu. Watajikaza na kuvumilia ila eventually wanajikuta wameanza kukosa raha maishani.
haya mambo ya avatar haya? Acha tu lizzy? Watu hawalali eti?
 
Back
Top Bottom