Wazungu wezi wa ATM wamkataa mkalimani

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
Wazungu wezi wa ATM wamkataa mkalimani


na Happiness Katabazi

UPANDE wa mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ulishindwa kuwasomea mashitaka raia wawili wa Bulgaria ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa tuhuma za wizi wa sh milioni 70 mali ya Benki ya Barclays.

Mwendesha Mashitaka Mfawidhi, Edger Luoga, mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Nedkolazarous’ Standaev (35) na Stela Peteva Nedelcheva (23).

Luoga alipokuwa akijiandaa kuanza kuwasomea mashitaka huku mkalimani aliyetafutwa na serikali kwa ajili ya kutafsiri lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Bulgaria, ndipo mshitakiwa wa pili, Nedelcheva, alinyosha mkono na kuiambia mahakama hiyo kwamba hawana imani na mkalimani huyo (jina tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama).

Nedelcheva alidai kuwa wamefikia uamuzi wa kumkataa mkalimani huyo kwa sababu haifahamu vyema lugha ya Bulgaria na kwamba hata walipokamatwa hivi karibuni, mkalimani huyo aliletwa polisi na wakati wakihojiwa, alikuwa akitafsiri lugha yao isivyostahili.

“Mheshimiwa hakimu, mkalimani huyu hatumtaki, atafutwe mkalimani mwingine kwa sababu hatuna imani naye kwa kuwa hata tulivyokamatwa na kuchukuliwa maelezo na polisi, alikuwa akitafsiri tofauti na maelezo yetu tuliyokuwa tukiyatoa kwa lugha yetu ya Bulgaria,” alidai Nedelcheva ambaye alijifunga kanga aliyopewa na wasamaria wema baada ya kutinga mahakamani hapo akiwa na kaptula fupi iliyokuwa ikionyesha maungo yake.

Aidha, Hakimu Lema alisema amesikia ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 27, na kuamuru washitakiwa hao wakahifadhiwe kwenye mahabusu ya polisi. Mapema wiki hii, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari kwamba wanawashikilia watuhumiwa wakiwa na kadi maalum zilizowawezesha kuiba kwenye ATM ya benki ya Barclays.
 
Kumbuka bado ni watuhumiwa halafu hakimu anayajua mazingira ya mahabusu zetu. Hawahitaji kuteswa bado, ngonja tusubiri kama hukumu ikija ikawa ni kufungwa jela kama hakimu ataamuru wapelekwe wapi labda hoteli mojawapo DAR!!!!!!
 
"Mheshimiwa hakimu, mkalimani huyu hatumtaki, atafutwe mkalimani mwingine kwa sababu hatuna imani naye kwa kuwa hata tulivyokamatwa na kuchukuliwa maelezo na polisi, alikuwa akitafsiri tofauti na maelezo yetu tuliyokuwa tukiyatoa kwa lugha yetu ya Bulgaria," alidai Nedelcheva ambaye alijifunga kanga aliyopewa na wasamaria wema baada ya kutinga mahakamani hapo akiwa na kaptula fupi iliyokuwa ikionyesha maungo yake.


Kwa kuangalia hiyo nyekundu hapo juu, Bwana PDiddy heading yako inatofautiana na contents .
Lakini nadhani wale watu walishikwa wakiwa wamevalia vile, na ndio wanavyovaa katika hali ya kawaida kabisa, hivyo sioni kama hii ingekuwa ni ishu ya kukustua sana...
Huyo aliyejipendekeza kuwapa kanga ninamlaani , maana ameingilia hukumu!
 
Mi mpaka sasa jamani nimeshindwa kuelewa walielewa vipi kama mkalimani hatafsiri ipasavyo kama hawaelewi lugha ya Kiingereza?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom