Wazungu wanamtaka mwanangu!!

Kuhusu maslahi yake ya baadaye nakubalina na wewe wape tu washikaji. Mikataba muhimu sana usije ukajuta baadaye.
 
yap, this is true .hao jamaa kama wana claim wana academy ubaloz wao utakuwa unajua so fuatilia kwa uhakika ujiridhishe mkuu. maisha ni popote jitahid kwenda kiubaba zaid na kisheria kwa sanaaaa. Mengine yatajileta
 
Wakurya bwana! Kumbe ngumi ziko ktk damu. Iko siku hata baba yake atapigwa ngumi! Amang'ana gasarikile tata! Strike the hammer while iron is still hot!
Hivi huu ulimbukeni wa ukabila unawapa faida gani??? Kumbe kina Matumla wote, Cheka, Tyson, Evander,Mayweather na wanamasumbwi wengineo ni Wakurya?! Shame on you all wagonjwa wa ukabila.
 
Wakuu nina mtoto wa kiume ambaye ndiye first bone wangu mwenye miaka9,huyo dogo nilikua nikiishi nae hapa dar,lakini nilikua nikipata kesi nyingi za ugomvi every day,mwaka jana nikakata shauri nikampeleka kwa bibi yake yaani mamangu mzazi kijijini kwetu Musoma.......wiki iliyopita nilipigiwa simu na mamangu kwamba dogo kampiga dogo mwenzie mwenye miaka 12 mpaka kamng'oa meno kwahiyo kuna kesi na inatakiwa elfu70 ya matibabu,nikatuma hiyo pesa.Leo asubuhi nimepigiwa simu tena kwamba jana kulikua na mashindano ya box(ngumi)kuanzia watoto wa miaka 10-15,bcoz my soon ni mdogo aliamua kudanganya umri kwamba ana11 na anauwezo wa kupigana then akaruhusiwa kupigana,mdogo wangu ndiye aliyetoa ruksa hiyo kwa lengo la kumkomesha dogo ili adundwe aache ugomvi mtaani,cha ajabu dogo alipafom mpaka jukwaa zima wakawa wanamshangilia,alipigana pambano1 na alishinda kwa round ya kwanza tena kwa kumpiga ngumi6 tuu adui yake,na akapata zawadi ya tsh150,000 cash,sasa kuna jamaa wa holland wana academy ya box kenya wamempenda dogo wanataka wamchukue waende nae kenya na baadae holland wamesema nikiwakabidhi wao watamuhudumia kila kitu mpaka atakapofikisha umri wa kujitegemea na akifikisha miaka 12 wataanza kumlipa some amounts,nimewambia waje dar tuonane na watakuja ijumaa this week.Nipo tayari kumwachia but mamake hataki kusikia habari hiyo ya ngumi,pls ushauri.

Wewe mzazi, mwanao is a minor tena kabisa. Wana haki ya shule na mambo mengine ili wakuwa kama watoto wasije wakawa kama malezi ya marehemu Michael Jakson na baba yake.

Pili wewe ni mzazi na mtoto kuwa na tabia ambazo si zake solution si kumpeleka kwa bibi. Yaani mama yako akuzae wewe akulee hadi uwe na mji wako halafu leo hii unampelekea mzigo wa mtoto mtukutu? Usikwepe majikumu. Ishi na mwanao ili uweze kumfahamu vyema na kumpa malezi. Mama yake ndiye mwenye uchungu naye!!!

Huko aliko anasoma? Na kama anasoma ni shule gani na ubora upi wa elimu? Usipoangalia utampoteza huyu mtoto. Tena mtoto mtukutu anatakiwa aishi na wazazi maana ndiyo wanatakiwa wamvumilie na wana upendo wa dhati kuliko uncle or grands or aunt.

Masuala ya ngumi, achana nayo, kamchuku mtuto, mpe counselling asome shule nzuri na akifikia 18 yrs ataamua the best na wazungu wamchukue na si kwa sasa.

Du nimechoka. Malezi mengine ya familia ni magumu sana.
 
Wakuu nina mtoto wa kiume ambaye ndiye first bone wangu mwenye miaka9,huyo dogo nilikua nikiishi nae hapa dar,lakini nilikua nikipata kesi nyingi za ugomvi every day,mwaka jana nikakata shauri nikampeleka kwa bibi yake yaani mamangu mzazi kijijini kwetu Musoma.......wiki iliyopita nilipigiwa simu na mamangu kwamba dogo kampiga dogo mwenzie mwenye miaka 12 mpaka kamng'oa meno kwahiyo kuna kesi na inatakiwa elfu70 ya matibabu,nikatuma hiyo pesa.Leo asubuhi nimepigiwa simu tena kwamba jana kulikua na mashindano ya box(ngumi)kuanzia watoto wa miaka 10-15,bcoz my soon ni mdogo aliamua kudanganya umri kwamba ana11 na anauwezo wa kupigana then akaruhusiwa kupigana,mdogo wangu ndiye aliyetoa ruksa hiyo kwa lengo la kumkomesha dogo ili adundwe aache ugomvi mtaani,cha ajabu dogo alipafom mpaka jukwaa zima wakawa wanamshangilia,alipigana pambano1 na alishinda kwa round ya kwanza tena kwa kumpiga ngumi6 tuu adui yake,na akapata zawadi ya tsh150,000 cash,sasa kuna jamaa wa holland wana academy ya box kenya wamempenda dogo wanataka wamchukue waende nae kenya na baadae holland wamesema nikiwakabidhi wao watamuhudumia kila kitu mpaka atakapofikisha umri wa kujitegemea na akifikisha miaka 12 wataanza kumlipa some amounts,nimewambia waje dar tuonane na watakuja ijumaa this week.Nipo tayari kumwachia but mamake hataki kusikia habari hiyo ya ngumi,pls ushauri.

Mkuu mandieta, Vipi dogo alishaenda Holland? Kama bado je anaendeleaje kwasasa akiwa na 11yrs? Tupe mrejesho kaka!
CC: Mwana kinyonga ; dandabo; Zogwale; kazikubwa
 
Kaka katika kukusoma nimeona umejijali mwenyewe kwanza Kabla ya mwanao umefikiria mengi kuhusu wewe mwenyewe kuliko mwanao, Mie nakushauri 1.mwanao hakikisha elimu yake nzuri Hiyo ngumi iwe Kama hobby tu kwake ya kujiendeleza jioni ili mumkwepeshe kwenye mabalaa ya kupiga wenzake mtaani. 2 Mtoto bado mdogo so usimsifie kuhusu kupiga wenzake mfahamishe lipi baya na lipi Zuri na kusikia mwanao anapiga watoto wa watu kwa sifa si nzuri uzuri ni kuona kipaji mpe kipaji ila Elimu usimtupie mbali mwanao. 3. mama naye ni mzazi kaa naye vizuri naye sikiliza ushauri wake naye mpe ushauri kwa maisha ya mwanao yawe vipi Mbele. 4.Kaka chunguza au yafuta watanzania wanaoishi Holland wakuchunguzie hao watu wa Boxing ni kweli na miakataba ichunguzwe na Wanasheria na balozi ya tanzania huko Holland. 5. tanzania pia chama cha ngumi na michezo wakuchunguzie Kabla hujamtoa mwanao ukaanzisha Mada jamiiforum ya namtafuta mwanangu. kaka dunia sio mbaya au Tambara bovu ila wanadamu ndio wabaya Kabla ya kufurahisha roho yako kaa chini fikiria future ya mwanao Mfano West Africa Wazee wengi wamepoteza watoto wao nje kwa ma Agency waongo wampira wa miguu. human Traffic ni kubwa so Elimu na Nizamu kwa mwanao muhimu na fikiria pia watoto anowapiga mtaani fanya Kama wako pia Boxing muendeleze ila mtengeneza awe na heshima pia la sivyo hata maisha yake yaBoxing yatakwenda vibaya nakutakia kila la kheri na mwanao Kaka najua unampenda mwanao ndoma ukaomba ushauri namalizia usifikirie nafasi ya mwanao itapotea fikiria pia usije kumpoteza mwanao.
 
Hata mama Hasheem alimkabidhi mwanae kwa Wakenya sasa anakula bata tu. Nawewe mkabidhi
 
Nilikuwa sijatizama hii Kumbe ni yatoka mwaka 2012 ? Nilijua mada ya huu mwaka hata Mie ningependa kujua kafikia wapi Dogo ?

Hopefully, kwavile mandieta bado yupo basi sasa atakumbuka kutupa mrejesho ili jamvi lijue....
 
tumia kiswahili tu. sema mwanangu/mtoto wangu. my soon ndo nini? na wewe ulikimbia shule kwa sabau ipi?at least mwanao ngumi. wewe nini?mademu? soon= son

Mtani nilikua nina 100% kwamba my soon atakua mtu wa football maana hiyo mi surprise ya jezi na njumu niliyokua namnunulia usipime,badala yake upepo umegeuka,kwa kweli mtani huyu dogo ni mbavu kishenzi,maana ata mamake alishashindwa kudhibiti kwa stick that's why nikampeleka bush.Maana nilihisi labda picha za kichina zimemuharibu.
 
Kuna kaka tunafahamiana, mwanae wa kujifunzia alichukuliwa kwa staili hii. Kumbe akawa anatumika kusafirisha madawa ya kulevya. Alikuja kufia China, in a hotel baada ya vidonge kupasukia tumboni. Mamake hakuweza hata ku-claim mwili kwa hofu.

Kuwa extra careful aisee!
Mhhh inatisha.
 
Back
Top Bottom