Wazungu wamedanganya sana juu ya Africa na mwafrica

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Wazungu wamedanganya sana juu ya Africa na mwafrica kwa makusudi kabisa.John Hanings Speke 1860,anamweleza mwafrica hivi..kama alivyofanya baba yake huko nyuma ndivyo afanyavyo hadi leo,humtumikisha mkewe na huridhika kufia juu ya nchi nyingine,ni goigoi kama dume la nyani..
Jean Jaques Rouses anasema,mwafrica hawezi kufikiri..
Na bado wanaendelea kutudharau na wakati huo huo viongozi wetu wanaenda kuwekeza huko...
 
Kwani ni uwongo, angalia mabakuli tunayotembeza huko ulaya wakati tuna rasilimali za kutosha!

Angalia miaka 50 ya uhuru bado badget ya nchi inategemea wafadhili!

Angalia tunavyo hogwa hovyo hovyo ili tununue rada na ndege ya rais kisha hongo hizo tunaziweka huko huko ulaya!

Angalia Mwafrika akishindwa urais anavyo ng'ang'ania madarakani!

Angalia demokrasia yetu ya kuunga unga na kuwapotezea wote wanaojitokeza kuwapinga!

Angalia kiongozi akikwapua mapesa ya wananchi hukumu anayopewa na mwizi wa kuku uswahilini anavyohukumiwa!

Angalia Maprofesa na Madoctor watu wanavyo kimbia taaluma na kukimbilia kwenye siasa! Wakishapata shahada zao hawajishughulishi tena na reseach!

Angalia matokeo baada ya muda mfupi tukikabidhiwa kiwanda tukiendeshe!

Angalia tunavyo weka mikataba ya kilaghai na ujambazi kwa madini na uwekezaji!

Marais wengine hawajui hata chanzo cha umasikini wa watu wake wakati wana rasilimali kibao!

Mifano ni mingi mpaka inatia hasira!
 

Tatizo sio mzungu....tatizo ni sisi wenyewe

Hatuwezi ukataa ukweli huu kwa maneno tu bali ya kuonesha matendo.......by far, wanayotusema nayo ndio ukweli ulivyo

Kazi kujishika maeneo utafikiri ndiko tunakokutumia kufikiri, wakati wenzetu wanaumiza mbongo zao kufanya vitu vya maana kwa nchi zao

Ni kweli wako wengi tofauti lakini generally wengi ni aibu tupu
 
Tubadilike! Tufanye maamuzi yetu kwa kuwatumia wasomi wetu wenyewe. Tukatae ushauri wa kilaghai tuwaenzi hawa wataalamu wetu. Hapo ndiyo watajua sasa hatudanganywi na plastic smile zao!
 
Yeyote atakayeweza kutengeneza hata sindano atakuwa ameokoa mamilion ya waafrica,it is our time,let us play our part
 
Hata Katika lugha ya kiswahili wazungu waliweka maneno yao ilikuonekana wao ni badala ya muumba.
Wakajiita wao
"MZ-UNGU" na aliewatuma afrika anaitwa "M-UNGU"
hivyo bado kifikra na kila kitu tupo nyuma
 
Back
Top Bottom