Wazungu wajipanga kuimaliza Simba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
HOMA ya Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeanza kupanda kwa timu zote 12 zinazoshiriki ligi hiyo ambapo makocha wazungu wa Yanga na Azam FC wamekamia kuisambaratisha Simba na kuipora ubingwa.
Tayari makocha wa timu hizo wameanza kujipanga kwa kuziandaa timu zao kwa ajili ya kinyang'anyiro hicho kitakachoanza kutimua vumbi kuanzia Januari 16 katika viwanja mbalimbali vya Tanzania Bara.

Wakati homa hiyo inapanda mabingwa watetezi, Simba wliomaliza ligi wakiwa wanaongoza kwa pointi 27 wakifuatiwa na Yanga yenye pointi 25 na Azam yenye pointi 20 wako kwenye kibarua kigumu mbele ya wazungu wawili ambao wamepanga kuivua ubingwa timu hiyo.

Wazungu hao ni Mserbia Kostadin Papic ambaye ni kocha wa Yanga na Muingereza Hall Stewart wa Azam FC ambao wamejipanga vyema kwa kumuweka mtu kati kocha wa Simba, Patrick Phiri kuhakikisha hachukui tena ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.

Papic aliyeimarisha kikosi chake kwa kumuongeza mshambuliaji Davies Mwampe kutoka zambia, tayari yuko chimbo uwanja wa Uhuru Dar es salaam akiliandaa jeshi lake kwa ajili ya vita hiyo ya ubingwa kwa kuwafundisha mbinu za uwanjani namna ya kuwakabili wapinzani wao na kupachika magoli.

"Tuko nyuma kwa pointi 2 kulinganisha na timu inayoongoza, Tunahitaji kuanza kwa kasi na kuhakikisha tunapanda kileleni na kukaa moja kwa moja. Lazima tupambane kiume," alisema Papic.

Naye Stewart ambaye ameingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Azam, anasema kuwa anaanza kazi kwa kazi moja tu, kuhakikisha kuwa anaipa ubingwa timu yake.

Stewart ambaye kwa mara ya kwanza alitua nchini kama kocha wa timu ya Taifa ya Zanzibar, anasema kuwa anakuja kwa kazi moja tu, ya kupambana na vigogo wa soka nchini, yaani Simba na Yanga.

"Nimesikia habari zao. Najua simba na Yanga ndiyo timu zinazotamba hapa Tanzania, lakini mimi nimekuja kwa kazi moja tu, ya kumaliza tambo zao hasa Simba kwa kuwashusha kileleni mwa ligi," alisema.

Kocha huyo alisema kuwa ana matumaini makubwa ya kutimiza malengo yake, hasa kutokana na ukweli kuwa timu yake ina nguvu nje na ndani ya uwanja.

Phiri yeye alikuwa na kazi ya kutengeneza stamina ya wachezaji wake kwenye ufukwe wa Coco Beach na kwenye gym iliyopo maeneo ya VETA chang'ombe jijini Dar es salaam.

Kocha huyo anasema kuwa baada ya kumaliza dozi hiyo ya kujenga stamina, kesho anaanza rasmi kuwapa mbinu za mauaji ya mzunguko huo wa pili.

"Leo (jana) na kesho (leo) tunamalizia programu yetu ya gym na ufukweni na jumatatu tunarudi uwanjani. Tutaanza kufanya mazoezi uwanja wa Uhuru kuanzia saa 12 za asubuhi na jioni," alisema Phiri.

Akizungumzia suala la kutetea ubingwa wake, Phiri alisema kuwa alipoingia mkataba wa kuinoa simba mapema mwaka jana, aliwaahidi viongozi wa Simba kuwa atawapa ubingwa mara mbili, ameshawapa mara moja na sasa anamalizia.

"Nahitaji kukamilisha ahadi yangu, kwa hiyo kwa mara nyingine tena ubingwa unabaki kwetu na wanaofikiria ubingwa wasahau kabisa," alisema Phiri.
 
Kuongea si kutenda, Papic tuko naye, tumemzoea na tunamjua yeye SIMBA ndiyo kikombe, hatuna wasiwasi naye.

Huyu Hall aizoee ligi kwanza ndo azungumzie ubingwa,size yake ni JKT Ruvu, Kagera Sugar hao ndo wa kupambana nao. Simba hatujalala tupo macho na tunajua kuwa wazungu hao nao hawalali.

SIMBA NGUVU MOJA.
 
katika pitiapitia yangu ratiba ya klabu bingwa afrika mwakani,nimeona simba inaanza raundi ya awali na timu kutoka Comoro,mshindi wa mechi hiyo anacheza na TP Mazembe ktk raundi ya kwanza
 
Back
Top Bottom