Wazulu katika historia ya TANU na ukombozi wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,887
30,233
BI. MAUNDA BINTI LUKOYO MKE WA AFANDE PLANTAN NA WANAE

...kwa kweli jina la Kizulu la Affande Plantan lilikuwa Shangaan. Hili jina lilitokana na kijiji katika Inhambane Msumbiji, walikotoka Sykes Mbuwane na Affande Plantan. Chini ya Herman von Wissman Wajerumani waliwaajiri Wazulu 400 kutoka Msumbiji kama mamluki na kujanao ndani ya manowari hadi Pangani ili wapigane na Abushiri na Chifu Mkwawa. Hii ilikuwa katika miaka ya mwisho ya 1800...''

2016%2B-%2B1

Bi Maunda Binti Lukoyo mke wa Affande Plantan kabila Mmanyma, Mkusu kutoka Belgian Congo
Mama yao na Thomas, Schneider na Mashado Plantan

(Picha kwa hisani ya Bi. Maunda Plantan mjukuu wa Affande Plantan na Maunda Binti Lukoyo)
''...pamoja na Kleist katika mji wa wa Dar es Salaam walikuwepo ndugu wa mbali watatu, Mwalimu Thomas Plantan, (hilo jina Mwalimu alipewa kwa sababu alikuwa Mwalimu wa shule), Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan.

Hawa Wazulu waliweza kutambulika kwa urahisi kutokana na majina yao ya Kikristo ingawa wao wenyewe walikuwa Waislam. Majina hayo yalikuwa na mchanganyiko wa majina ya Kijerumani, Kireno na Kiingereza; kama vilevile Kleist na Schneider ni majina ya Kijerumani; Mashado ambalo ni jina la Kireno na Thomas ni la Kiingereza.

Wote hao, Kleist, Mwalimu Thomas, Schneider na Mashado baadaye walifanya kazi kubwa katika kupiga vita ukoloni na katika kuupeleka mbele Uislamu, kabla na baada ya uhuru. Bahati mbaya majina haya ya Kiislamu ya wazalendo hawa hayakujitokeza sana na badala yake walijulikana zaidi kwa majina yao ya Kizungu waliyoyarithi kutoka Wajerumani kupitia wazee wao wa Kizulu...''

qc_J5OZpZ8C4MNZ9CY-eEuXj3hF0z8DyZ9yqU0rqhtgDUAuPfOF3MTTZYncu9pH4Te5IpjGZRFeBiw6S1tXpXablsTIaZhKC-wNlBBFdT6w4UrGxmQRzBiynbshw2lp_GHHwxrzH2OwCNxvQIUKpVrkNSF5CdarxN2jPRVuFv0lUghdsP_J5zA4wumMd1zyUIzhcHnSyRwUjwiBEl9LR30wBcPXxfKcKElsFP-l62FsQtJUojhA5cuFadKA8D-_YQqkQFfVgH5MMWhi8kAhHUWVH8aJi6d3Q42bU6HbdN5CB2CtQSdMr9mgpFeZY8WR3dyBCXBTPZGi9uaaIYLXbyxkIHYYa7QaTcNYQr46uVEoGtDTLD7LC3XqaRkViDbpoxy6e7MzFdJaAxgEoxwOvilJrMtVaSICyZB8zRroKP9cdIuJIJkgwkncYl0x9tQINahMcZQxq7Lpm13y2qu5_nUxrAqytMf9ELU-bXTLlalubn2oDtiEkbOWaHzDCprQjx1bg5WKYL3TVWOnS-Yr28l965RmfESypuTiDUUEM7wr6QW9CSfBiP7biWV5fQms-bZISF2B_wYI0NNh7ZsoHs2QZt4GbWIzAASF8P7u4S_hNIW1Z8w=w480-h360-no

Mwandishi akizungumza na Bi. Maunda Plantan nyumbani kwa Bi. Maunda
Magomeni Mikumi Bi. Maunda ni mwanamke wa kwanza kutangaza Sauti
ya Dar es Salaam radio ilipoanzishwaTanganyika 1952

''...baada ya kuwashinda wananchi wa Tanganyika, Wissman alitunzwa na serikali yake na akafanywa Gavana wa German East Africa kati ya mwaka wa 1895 na 1896. Wazulu nao kwa kuwa walichangia katika ushindi huo na wao hawakutoka mikono mitupu, Wajerumani walitunza. Kwa kuwa Mohosh hakuweza kudai uchifu ugenini alifanywa kuwa mkubwa wa jeshi la polisi la Wajerumani (Germany Constabulary) katika mji wa Dar es Salaam na hapo ndipo alipopata jina hili la Affande Plantan.

Wazulu katika jeshi la Wajerumani walikuwa wakilipwa mishahara mizuri na hali zao zilikuwa bora ukilinganisha na wenyeji. Wenyeji wengi waliajiriwa na serikali katika jeshi kama vibarua. Hii ndiyo sababu hasa iliyomfanya Kleist apate malezi ya hali juu yaliyompelekea kupata elimu, kazi nzuri na mwishowe kuwa mmoja wa watu mashuhuri katika mji wa Dar es Salaam.

Kleist alipelekwa kusoma shule ya Wajeruman iiliyokuwa OceanRoadHospital ambako alijifunza Kijerumani, kupiga chapa na hati mkato, ujuzi adimu na wa thamani sana kwa Mwafrika enzi zile. Katika nyumba ya Affande Plantan, Kleist alilelewa pamoja na watoto wa Affande Plantan mwenyewe, Schneider Abdillah, Ramadhani Mashado na Thomas Saudtz mtoto wa ndugu yake wa mbali kidogo.

Watoto hawa wote walipata elimu nzuri ambayo iliwawezesha kuwa watu muhimu. Mashado Plantan alikuja kuajiriwa kama askari akiwa na cheo kilichomtabulisha kama ''English Speaking Policeman,'' yaani askari anaezungumza Kiingereza, na baadae alikuja kuwa mhariri wa magazeti aliyoyamiliki mwenyewe. Gazeti lake la kwanza likiitwa ''Dunia.''

Hii ilikuwa kabla ya 1938 na. wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia mwaka wa 1938 akaanzisha gazeti lililoitwa ''Zuhra.'' Thomas Saudtz alikuja kuwa mwalimu wa shule, Schneider alikuwa mkulima na katika siku za mwisho wa uhai wake aliungana na Sheikh Hassan bin Amir kama katibu wa Daawat Islamiyya (Mwito kwa Waislam).

Vita ya Kwanza ya Dunia (1914-1918)
''...ilikuwa wakati bataliani ya Schneider na Kleist ipo Korogwe, mji uliopo maili chache kutoka Tanga, katika kijiji kiitwacho Semanya ndipo Kleist alipopokea habari kuwa Affande Plantan, baba yake Schneider amefariki Dar es Salaam. Plantan alikuwa amekufa kwa homa ya matumbo tarehe 11 December 1914. Wajerumani walisimamisha vita kwa siku saba kwa heshima ya Affande Plantan...

Waarabu waliungana na Waingereza kuwatimua Wajerumani Tangayika. Bado baadhi yao walikuwa na kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha Wajeruani kwa shujaa wao Abushiri ambae walimnyonga mwaka 1889. Historia ikajirudia upya; Kleist na Schneider waliingia katika mapigano Mwele Ndogo dhidi ya adui wa zamani wa baba yao na adui wa Wajerumani ñ Waarabu.

Mapambano haya yalifanyika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka wa 1915 katika sehemu ile ile ambayo Sykes Mbuwane na Affande Plantan mamluki wa Kizulu waliteremka kwenye meli kuja kuwaongezea nguvu Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waarabu na Abushiri bin Salim na Mkwawa...

Mashado Ramadhani Plantan alikuja Tanganyika kutoka Mozambique akiwa mtoto mdogo mwaka 1905 wakati nchi ipo katika vita vya Maji Maji dhidi ya Wajerumani. Mwaka 1924 alirudi Msumbiji na alisafiri kwenda Lisbon kwa pasi ya Kireno. Wale waliomfahamu wanasema kwa kiwango cha miaka ya 1950, Mashado Plantan alikuwa mtu mjuzi wa mambo. Alikuwa miongoni mwa wanachama wa mwanzoni wa African Association ilipoanzishwa mwaka 1929 na miongoni mwa wanachama wa awali kujiunga na TANU pale ilipoasisiwa mwaka 1954.

Vita Kuu ya Pili 1938-1945
Askari wa zamani waliopigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza katika ardhi ya Tanganyika wakati wa Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia kati ya mwaka 1914-1918 walimuunga mkono Hitler, ingawa si wazi wazi kwa kuwa kufanya hivyo kungekuwa usaliti na uhaini dhidi ya Himaya ya Waingereza. Hata hivyo hilo halikumzuia Schneider, askari wa Kijerumani wa Vita Kuu ya Kwanza vya Dunia, kutembea huku na kule katika mitaa ya Dar es Salaam akiwachochea watu wasimuunge mkono Winston Churchill katika vita vyake dhidi ya Adolf Hitler. Schneider alikamatwa na kuwekwa kizuizini huko Mwanza, na hakufunguliwa hadi mwisho wa vita mwaka 1945...''

TANU 1954
''...John Hatch wa Labour Party ya Uingereza alipokuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa TANU Nyerere alikuwa kwao kijijini. Tutaona hapo baadae kidogo jinsi mgeni huyu Mwingereza alivyomgutusha Schneider kuhusu TANU kuwashirikisha wanawake katika harakati za kudai uhuru.

Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani wa Hatch. Denis Phombeah pamoja na katibu mkuu wa TANU, Oscar Kambona vilevile walihutubia halaiki ile. Hatch akiwa anaunga mkono ukombozi wa watu weusi aligundua kuwa TANU haikuwa na tawi la akina mama. Katika dhifa ya chai iliyoandaliwa na TANU kwa heshima yake, Hatch alilieleza tatizo hili kwa Schneider Plantan na John Rupia. Hatch alimwambia Schneider kwamba ili kuwa na chama chenye nguvu TANU isiwaache akina mama nyuma.

Hatch alimwambia Schneider kwamba huko Uingereza Chama cha Labour kilikuwa kimejikita kwa wanawake kama moja ya nguzo yake kuu. Schneider alimwendea Bibi Tatu binti Mzee akamwomba kuanzisha tawi la akina mama kwa ajili ya TANU. Bibi Tatu binti Mzee alimpendekeza Bibi Titi Mohamed ndiye afanye kazi hiyo kwa sababu ya tabia yake ya ucheshi na kupenda kuchanganyika na watu...''

Ingia hao chini kwa nyongeza na kuangalia picha:
Mohamed Said: BI. MAUNDA BINTI LUKOYO MKE WA AFANDE PLANTAN NA WANAE

(Taarifa za enzi ya Wajerumani na Vita ya Kwanza ya Dunia ni kutoka mswada alioandika Kleist Sykes kabla hajafariki 1949)
 
Kumbukumbu kama hz ni muhimu sana japo zinafichwa sana ktk kizazi hiki.
Kwa nini unasema kumbukumbu zinafichwa? Kwanza zinafichwa na nani? Mleta mada amezipataje? Usikimbilie kulsumu kila kitu. Labda nikujulishe tu kuwa all history is hidden until it is uncovered by historians. Hakuna historian yoyote inayoelea tuu huu. Ni jukumu la watu kama mleta mada, wewe, mimi na wengine "kuichimba" hiyo historian na kuileta huu!
 
Zikomo...
Historia ya Tanganyika imefichwa na kuvurugwa kwa makusudi.
Hili tumeshalizungumza hapa na mimi kutoa ushahidi.
 
Inawezekana, lakini nasisitiza kuwa bado mtu mwenyewe nia ya kuitafuta ataipata tu. Official records kama chanzo muhimu kinaweza kufichwa lakini oral traditions na watu walioona/wenye ufahamu wa matukio baadhi yao wapo. Kwani wewe unapata wapi hizi historia?

Kimsingi siikatai hoja yenyewe bali najaribu tu kuhoji tufanyeje sasa? Tuendelee kukaa kimya na kusema historia imefichwa?
 
Maneno yako ni sawa kabisa.

Mimi nimeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na nimegundua
kuwa ''records,'' nyingi zimo mikononi mwa watu binafsi.
 
Jambo la busara na lenye heshima ni kuziandika kumbukumbu kama zilivyokuwa. Shida inakuja pale zinapoegemea maeneo ambayo tunafaida nayo tu...kama dini au siasa binafsi za anayeandika
 
BI. MAUNDA BINTI LUKOYO MKE WA AFANDE PLANTAN NA WANAE

...kwa kweli jina la Kizulu la Affande Plantan lilikuwa Shangaan. Hili jina lilitokana na kijiji katika Inhambane Msumbiji, walikotoka Sykes Mbuwane na Affande Plantan. Chini ya Herman von Wissman Wajerumani waliwaajiri Wazulu 400 kutoka Msumbiji kama mamluki na kujanao ndani ya manowari hadi Pangani ili wapigane na Abushiri na Chifu Mkwawa. Hii ilikuwa katika miaka ya mwisho ya 1800...''

2016%2B-%2B1

Bi Maunda Binti Lukoyo mke wa Affande Plantan kabila Mmanyma, Mkusu kutoka Belgian Congo
Mama yao na Thomas, Schneider na Mashado Plantan

(Picha kwa hisani ya Bi. Maunda Plantan mjukuu wa Affande Plantan na Maunda Binti Lukoyo)
''...pamoja na Kleist katika mji wa wa Dar es Salaam walikuwepo ndugu wa mbali watatu, Mwalimu Thomas Plantan, (hilo jina Mwalimu alipewa kwa sababu alikuwa Mwalimu wa shule), Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan.

Hawa Wazulu waliweza kutambulika kwa urahisi kutokana na majina yao ya Kikristo ingawa wao wenyewe walikuwa Waislam. Majina hayo yalikuwa na mchanganyiko wa majina ya Kijerumani, Kireno na Kiingereza; kama vilevile Kleist na Schneider ni majina ya Kijerumani; Mashado ambalo ni jina la Kireno na Thomas ni la Kiingereza.

Wote hao, Kleist, Mwalimu Thomas, Schneider na Mashado baadaye walifanya kazi kubwa katika kupiga vita ukoloni na katika kuupeleka mbele Uislamu, kabla na baada ya uhuru. Bahati mbaya majina haya ya Kiislamu ya wazalendo hawa hayakujitokeza sana na badala yake walijulikana zaidi kwa majina yao ya Kizungu waliyoyarithi kutoka Wajerumani kupitia wazee wao wa Kizulu...''

qc_J5OZpZ8C4MNZ9CY-eEuXj3hF0z8DyZ9yqU0rqhtgDUAuPfOF3MTTZYncu9pH4Te5IpjGZRFeBiw6S1tXpXablsTIaZhKC-wNlBBFdT6w4UrGxmQRzBiynbshw2lp_GHHwxrzH2OwCNxvQIUKpVrkNSF5CdarxN2jPRVuFv0lUghdsP_J5zA4wumMd1zyUIzhcHnSyRwUjwiBEl9LR30wBcPXxfKcKElsFP-l62FsQtJUojhA5cuFadKA8D-_YQqkQFfVgH5MMWhi8kAhHUWVH8aJi6d3Q42bU6HbdN5CB2CtQSdMr9mgpFeZY8WR3dyBCXBTPZGi9uaaIYLXbyxkIHYYa7QaTcNYQr46uVEoGtDTLD7LC3XqaRkViDbpoxy6e7MzFdJaAxgEoxwOvilJrMtVaSICyZB8zRroKP9cdIuJIJkgwkncYl0x9tQINahMcZQxq7Lpm13y2qu5_nUxrAqytMf9ELU-bXTLlalubn2oDtiEkbOWaHzDCprQjx1bg5WKYL3TVWOnS-Yr28l965RmfESypuTiDUUEM7wr6QW9CSfBiP7biWV5fQms-bZISF2B_wYI0NNh7ZsoHs2QZt4GbWIzAASF8P7u4S_hNIW1Z8w=w480-h360-no

Mwandishi akizungumza na Bi. Maunda Plantan nyumbani kwa Bi. Maunda
Magomeni Mikumi Bi. Maunda ni mwanamke wa kwanza kutangaza Sauti
ya Dar es Salaam radio ilipoanzishwaTanganyika 1952

''...baada ya kuwashinda wananchi wa Tanganyika, Wissman alitunzwa na serikali yake na akafanywa Gavana wa German East Africa kati ya mwaka wa 1895 na 1896. Wazulu nao kwa kuwa walichangia katika ushindi huo na wao hawakutoka mikono mitupu, Wajerumani walitunza. Kwa kuwa Mohosh hakuweza kudai uchifu ugenini alifanywa kuwa mkubwa wa jeshi la polisi la Wajerumani (Germany Constabulary) katika mji wa Dar es Salaam na hapo ndipo alipopata jina hili la Affande Plantan.

Wazulu katika jeshi la Wajerumani walikuwa wakilipwa mishahara mizuri na hali zao zilikuwa bora ukilinganisha na wenyeji. Wenyeji wengi waliajiriwa na serikali katika jeshi kama vibarua. Hii ndiyo sababu hasa iliyomfanya Kleist apate malezi ya hali juu yaliyompelekea kupata elimu, kazi nzuri na mwishowe kuwa mmoja wa watu mashuhuri katika mji wa Dar es Salaam.

Kleist alipelekwa kusoma shule ya Wajeruman iiliyokuwa OceanRoadHospital ambako alijifunza Kijerumani, kupiga chapa na hati mkato, ujuzi adimu na wa thamani sana kwa Mwafrika enzi zile. Katika nyumba ya Affande Plantan, Kleist alilelewa pamoja na watoto wa Affande Plantan mwenyewe, Schneider Abdillah, Ramadhani Mashado na Thomas Saudtz mtoto wa ndugu yake wa mbali kidogo.

Watoto hawa wote walipata elimu nzuri ambayo iliwawezesha kuwa watu muhimu. Mashado Plantan alikuja kuajiriwa kama askari akiwa na cheo kilichomtabulisha kama ''English Speaking Policeman,'' yaani askari anaezungumza Kiingereza, na baadae alikuja kuwa mhariri wa magazeti aliyoyamiliki mwenyewe. Gazeti lake la kwanza likiitwa ''Dunia.''

Hii ilikuwa kabla ya 1938 na. wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia mwaka wa 1938 akaanzisha gazeti lililoitwa ''Zuhra.'' Thomas Saudtz alikuja kuwa mwalimu wa shule, Schneider alikuwa mkulima na katika siku za mwisho wa uhai wake aliungana na Sheikh Hassan bin Amir kama katibu wa Daawat Islamiyya (Mwito kwa Waislam).

Vita ya Kwanza ya Dunia (1914-1918)
''...ilikuwa wakati bataliani ya Schneider na Kleist ipo Korogwe, mji uliopo maili chache kutoka Tanga, katika kijiji kiitwacho Semanya ndipo Kleist alipopokea habari kuwa Affande Plantan, baba yake Schneider amefariki Dar es Salaam. Plantan alikuwa amekufa kwa homa ya matumbo tarehe 11 December 1914. Wajerumani walisimamisha vita kwa siku saba kwa heshima ya Affande Plantan...

Waarabu waliungana na Waingereza kuwatimua Wajerumani Tangayika. Bado baadhi yao walikuwa na kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha Wajeruani kwa shujaa wao Abushiri ambae walimnyonga mwaka 1889. Historia ikajirudia upya; Kleist na Schneider waliingia katika mapigano Mwele Ndogo dhidi ya adui wa zamani wa baba yao na adui wa Wajerumani ñ Waarabu.

Mapambano haya yalifanyika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka wa 1915 katika sehemu ile ile ambayo Sykes Mbuwane na Affande Plantan mamluki wa Kizulu waliteremka kwenye meli kuja kuwaongezea nguvu Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waarabu na Abushiri bin Salim na Mkwawa...

Mashado Ramadhani Plantan alikuja Tanganyika kutoka Mozambique akiwa mtoto mdogo mwaka 1905 wakati nchi ipo katika vita vya Maji Maji dhidi ya Wajerumani. Mwaka 1924 alirudi Msumbiji na alisafiri kwenda Lisbon kwa pasi ya Kireno. Wale waliomfahamu wanasema kwa kiwango cha miaka ya 1950, Mashado Plantan alikuwa mtu mjuzi wa mambo. Alikuwa miongoni mwa wanachama wa mwanzoni wa African Association ilipoanzishwa mwaka 1929 na miongoni mwa wanachama wa awali kujiunga na TANU pale ilipoasisiwa mwaka 1954.

Vita Kuu ya Pili 1938-1945
Askari wa zamani waliopigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza katika ardhi ya Tanganyika wakati wa Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia kati ya mwaka 1914-1918 walimuunga mkono Hitler, ingawa si wazi wazi kwa kuwa kufanya hivyo kungekuwa usaliti na uhaini dhidi ya Himaya ya Waingereza. Hata hivyo hilo halikumzuia Schneider, askari wa Kijerumani wa Vita Kuu ya Kwanza vya Dunia, kutembea huku na kule katika mitaa ya Dar es Salaam akiwachochea watu wasimuunge mkono Winston Churchill katika vita vyake dhidi ya Adolf Hitler. Schneider alikamatwa na kuwekwa kizuizini huko Mwanza, na hakufunguliwa hadi mwisho wa vita mwaka 1945...''

TANU 1954
''...John Hatch wa Labour Party ya Uingereza alipokuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa TANU Nyerere alikuwa kwao kijijini. Tutaona hapo baadae kidogo jinsi mgeni huyu Mwingereza alivyomgutusha Schneider kuhusu TANU kuwashirikisha wanawake katika harakati za kudai uhuru.

Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani wa Hatch. Denis Phombeah pamoja na katibu mkuu wa TANU, Oscar Kambona vilevile walihutubia halaiki ile. Hatch akiwa anaunga mkono ukombozi wa watu weusi aligundua kuwa TANU haikuwa na tawi la akina mama. Katika dhifa ya chai iliyoandaliwa na TANU kwa heshima yake, Hatch alilieleza tatizo hili kwa Schneider Plantan na John Rupia. Hatch alimwambia Schneider kwamba ili kuwa na chama chenye nguvu TANU isiwaache akina mama nyuma.

Hatch alimwambia Schneider kwamba huko Uingereza Chama cha Labour kilikuwa kimejikita kwa wanawake kama moja ya nguzo yake kuu. Schneider alimwendea Bibi Tatu binti Mzee akamwomba kuanzisha tawi la akina mama kwa ajili ya TANU. Bibi Tatu binti Mzee alimpendekeza Bibi Titi Mohamed ndiye afanye kazi hiyo kwa sababu ya tabia yake ya ucheshi na kupenda kuchanganyika na watu...''

Ingia hao chini kwa nyongeza na kuangalia picha:
Mohamed Said: BI. MAUNDA BINTI LUKOYO MKE WA AFANDE PLANTAN NA WANAE

(Taarifa za enzi ya Wajerumani na Vita ya Kwanza ya Dunia ni kutoka mswada alioandika Kleist Sykes kabla hajafariki 1949)

Ndugu Mohamed Said kuna mahali katika nyuzi zako nilisoma kuwa Mkwawa alikuwa muumini wa dini la Kiislamu. Hebu toa ushahidi Zaidi. Ilikuwaje mpaka akawa Muislamu, ilipata kwa kuzaliwa kwenye familia ya Kiislamu yaani Baba yake Mwinigumba alikuwa Muislamu au alislimu ukubwani...?
 
Kokola,
Ushahidi gani nikupe kama Mkwawa ni Muislam?

Muislam ni Muislam na ukitaka kumjua Muislam
angalia kaburi lake kazikwaje.

Sina taarifa kuhusu baba yake lakini najua kuwa
mmoja wa majemadari wa Mkwawa alikuwa ni
ndugu yake akiitwa Yusuf.

Mkwawa mwenyewe alikuwa akisaidiwa silaha na
rafiki yake kutoka Zanibar akijulikana kama Rumaliza
ingawa jina lake khasa ni Muhammad bin Khalfan
Barwani.

Lakini kuwa Mkwawa alikuwa ni Muislam au vinginevyo
isikupe shida sana.

Songea Mbano ni Muislam lakini wanahistoria wetu wana
hofu ya kutaja jina lake la Kiislam kwa hiyo siku zote yeye
hutambulishwa kama Songea Mbano.

Lakini Songea Mbano jina lake ni Sultan Abdul Rauf
bin Songea Mbano.

Chief Mkwawa
analo pia jina lake la Kiislam na linafahamika
ila wapo wanaotishika na jina hilo kwa hiyo haliandikwi popote.

Hebu soma maneno niliyoandika hapa JF miezi michache iliyopita:

JUN
22

CHIEF ABDUL RAUF BIN SONGEA MMOJA WA MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI NDIYO HUYU SONGEA MBANO?

Khalidoun,
Haijapata kutokea mnakasha kama ule katika JF.

Hivi ndivyo nilivyofahamishwa na wenyeji walioipokea
barzani.
Wanamajlis,
Naona ukumbi umepoa.
Yuko aliyesema ana maswali kuhusu Nyerere anataka kuniuliza.

Kapotea sijamsikia.

Yuko aliyekuja na mpya kuwa Waislam sio walioanza harakati dhidi
ya ukoloni akataja Maji Maji.

Nikaweka jibu.

Hakuridhika akadai kuwa majibu nimejinukuu mwenyewe kwa hiyo
ni ajua.

451px-Chief_Songea_Mbano.jpg

Chief Songea Mbano

Nikaja na jibu kutola nyaraka za Wajerumani wenyewe waliopigana
na Chief Abdul Rauf bin Songea.

Najua kapata mshtuko kwa kuwa hajapatapo kumsikia Chief Abdul
Rauf bin Songea
katika Vita Vya Maji Maji ingawa inawezekana kuwa
kasikia Chief Songea Mbano.

Najua ametatazika kama wengi wanavyotatazika hivi sasa wakinisoma.
Hawa ni watu wawili au ni mtu mmoja?

Abdul Rauf bin Songea ndiyo huyu Songea Mbano?
Kuchakachua historia kuna hatari zake na hii ni mojawapo.

Hakuwa anajua kuwa Vita Vya Maji Maji Waislam walisimama dhidi ya
Wajerumani.

Majemadari 60 Waislam walinyongwa na kuzikwa kaburi moja Mahenge,
Songea na kumbukumbu ya iko hapo kwenye kumbukumbu ya Maji Maji
Songea.

Katika kaburi la peke yake amezikwa Songea Mbano.
Je huyu ndiye yule Abdul Rauf bin Songea?

Kuna mahali Abdul Rauf bin Songea anaitwa kwa jina la ''Chief Songea
Luwafu Mbano.''
 
Mohamed Said mimi nashukuru sana kwa kunijibu na wala usiwe na wasiwasi. Mkwawa kuwa Mwislamu sio jambo la ajabu ni sawa na mtu kushangaa kuwa katika nchi ya Kiislamu kama Irag lakini kiongozi wake mmoja wa ngazi za juu sana Taliq Aziz alikuwa Mkristo. Kinachofanya nivutiwe na kipengele hiki ni vipi Mkwawa alikutana na Imani ya Kiislamu wakati huo lakini naona kama Mohamed hukuona umuhimu wa kuliangalia hilo. Inawezekana aliingia Uislamu baada ya ndoa (kuslimishwa), au alikuwalia familia ya Kiislamu au aliamua yeye kuwa Mwislamu sio jambo la ajabu ila pia wewe kama mwana historia hayo pia ungeyamulika kuliko kuonekana kama unataka kushabikia kuwa kwake Mwislamu. Kuwa wa Imani Fulani ya dini sio tatizo lakini inapokuja kwenye historia usichague cha kuwakilisha elezea kikamilifu. Kama huna hizo data za jinsi alivyopata kuwa muumini wa dini ya Kiislamu basi si mbaya pia ukasema hujui. Lakini kuwa kwake Mwislamu si tatizo kabisa mkuu.
 
Kuna hofu kubwa katika jamii yetu kuhusu Uislam.

Mimi sifikiri kama ni jambo kubwa kwani Uislam umeingia huku kwetu
zaidi ya miaka 1000.

Ndiyo maana nikakupa hilo jibu kuwa Mkwawa alikuwa Muislam kwa
kuwa najua alikuwa Muislam na jina lake Abdallah.

Kwangu mimi jibu hilo lilitosheleza.

Lakini ili kukupa habari zaidi jinsi Uislam unavyowatisha baadhi ya watu
nikakuwekea kisa cha Sultan Abdul Rauf bin Songea Mbano ambae
ingawa wanahistoria wetu wanalijua fika jina lake hili lakini hawapendi
kuliandika wao wanatosheka na kumuita Songea Mbano.

Hili jina Abdul Rauf linawatia hofu.
Lakini juu hayo yote wakaligeuza jina hili likawa, ''Luwafu.''

Sasa ''data,'' ndiyo hizi za majibu ya swali ulilouliza.
 
Back
Top Bottom