Wazo tete la dr. Olomi

Dandaj

Member
Apr 16, 2009
73
2
Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza kukuomba mchango.
Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti na makatibu wa sherehe hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?
Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda. Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi, ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.
Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi wanaamini kuwa tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi kujitoa mpaka upepo uje ubadilike wenyewe!.
Mimi nafikiri wasomi tuna jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko pale ambapo mazoea yenye madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo cha ufukara na kuviza maendeleo.
Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi napendeleza na kuanza kutekeleza. Kuanzia Januari 2011, nitapunguza michango ninayotoa. Nitatoa tu kwa mtu wa karibu sana, na nitachanga kidogo. Usishangae nikakuchangia 20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia July 2011, nitaacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa nachangia elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo na pia nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.
Je waniunga mkono? Kama ndiyo sambaza huu ujumbe kwa mtandao wako.

Dr. D.R.Olomi
Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania
 
Ni ngumu sana kuacha kuchangia, na hasa ukizingatia ya kwamba ni culture iliyojengeka katika jamii yetu! Labda uwe ni mtu unayejitosheleza kwa kila kitu na humtegemei ndugu au rafiki yako kwa lolote au labda huwe unaishi nje ya Tanzania! Lakini kama unaishi hapa kwetu na bado una marafiki, ndugu pamoja na majirani mnaotegemeana kwa shida na raha inakuwa ngumu kutokuchangia.

Mimi nitam-support Dr. Olomi kwenye suala la kiasi ( nitakuwa natoa kidogokidogo), lakini sio niache kuchangia kabisa. Nitakosana na watu wa karibu, na wataanza kusema ooh naringa au nimeamua kujitenga! mambo ya culture ni magumu sana!
 
Hii culture mbovu tumeilea ndo hadi imefika hapa. Watu wako katika nafasi ambapo kuomba michango imekuwa jambo la kawaida mno japo kwa mambo ambayo hayana ulazima.

Acha wanaoomba kuchangiwa kwenye harusi, kuna wengine wanataka wachangiwe kipaimara cha mtoto, mwengine birthday ya watoto, wengine kutizama mechi ya mpira.

Toa mchango kwa mtu wako wa karibu na sio kwa kuombwa kwa mapenzi yako tu, kwa watu wa mbali usiwape labda liwe suala linalohusu elimu au afya. Inawezekana tukiamua
 
Mimi nlishamua sichangii harus hata iwe ya ndugu wa kuzaliwa tumbo1. Maana hata ikifika ya kwangu sitaomba mchango wao.
 
Back
Top Bottom